Huyu ndie mtangazaji, muuza nguo, mchoraji wa katuni za kipanya, na mwanzilishi wa Maisha Plus.
SHINDANO maalum lililotamba miaka nyuma la Maisha Plus, ambalo
washiriki wake hukaa kwa miezi miwili kijijini, linatarajiwa kuanza hivi
karibuni kwa kushirikiana na shirika la Oxfam.
Kiongozi Mtendaji wa
kampuni ya DMB, Masoud Ali ‘Masoud Kipanya’ alisema kuwa shindano hilo la aina yake
linakuja tena kwa msimu wa tatu, likiwa na utofauti kabisa, huku mambo
mbalimbali yakiboreshwa, ikiwemo mshindi kuibuka na kitita cha sh milioni 20.
Kipanya alisema
kuwa, kwa kushirikiana na wadhamini wakuu, Oxfam Tanzania ,
kupitia program yao ya ‘Mama shujaa wa chakula
ambako watapata fursa ya kuwaweka wanawake kwenye shindano, kwa kukaa ndani ya
jumba hilo la
Maisha Plus huko kijijini kwa wiki mbili.
“Kwa
kushirikiana na Oxfam, shindano hili tumeborsha na litakuwa la aina yake,
ambapo washiriki watakaobahatika kushiriki, watafurahia na watajifunza mengi na
safari hii Mama shujaa wa chakula nao watabahatika kukaa kwa wiki mbili, kisha
watatoka na washiriki wa Maisha Plus kuendelea na kinyang’anyiro cha kuwania
kitita hicho cha milioni 20, alisema Kipanya.
Aidha,
aliwataka vijana wa kitanzania, kuchangamkia fursa hiyo, ambako wanatarajia
kuanza kufanya usaili mkoani Arusha, Agosti 3 na kisha kuendelea kwenye mikoa
mingine 14, ikiwemo ya Bara na viswani Zanzibar.
Pia, alitoa
wito kwa wadhamini wengine, kutumia nafasi hii kujitokeza ili kupata kujitangaza,
kwani shindano hilo
licha ya kufanyika misimu miwili ya 2009 na 2010, huku 2011 likishindwa
kufanyika kutokana na kukosa udhamini, limejizolea sifa na kupendwa na watu wa
rika mbalimbali.


No comments:
Post a Comment