Sunday, July 22, 2012

Waislam wa Zanzibar wafanya maombi kwa waliotangulia. Nina Swali, hivi hawa na wale wa uamsho waliofanya maombi juzi tofauti yao nini?





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
 Shein,  leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar.

Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT,  iliyotokea hivi
 karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam
kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa

Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao
 wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la
 Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.

Picha zote na Habari ni kwa hisani ya blog ya Father Kidevu.

No comments:

Post a Comment