Rais Barack Obama na
mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia
mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko
colorado .
Obama
alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la
Aurora wakati
huu mgumu.
Alikiri
kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.
Mtu
mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi
watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la
filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.
Walioshuhudia
tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo
aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi
huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenyen ukumbi huo
mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.
Polisi
wanasaema kuwa walimtia mbaroni mtu mmoja katika eneo la kuegesha magari karibu
na eneo la tukio.
Alikuwa
na bunduki mbili.
Wanaamini
huenda silaha nyingi ziliachwa ndani ya ukumbi.
Mshukiwa
huyo alisema kuwa aliacha mabomu katika nyumba yake kwenye jumba moja.
Watu
wameamrishwa kuondoka kwa jumba hilo .
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:
Post a Comment