Balozi wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa Bi , Susan Rice, amesema Marekani itaimarisha juhudi
zake nje ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kushinikiza serikali ya Syria kuachia
madaraka.
Bi.
Rice, aliyasema hayo baada ya Urussi na Uchina kutumia kura zao za turufu
katika baraza hilo la Usalama kupinga vikwazo
zaidi dhidi ya serikali ya Syria ,
ikiwa haitasitisha utumizi wa silaha nzito nzito dhidi ya waasi na raia.
Urussi
ilisema kuwa azimio hilo
la baraza la usalama lililoungwa mkono na mataifa ya Magharibi halikubaliki kwa
sababu lingetekelezwa kwa kuwatumia wanajeshi.
Msemaji
wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ,
Kofi Annan, Ahmad Fawzi, alisema Bwana Annan, amesikitishwa sana
na hatua hiyo ya Urussi na Uchina ya kutumia kura zao za turufu kupinga azimio hilo .
Wakati
huo huo wapiganaji wa upinzani nchini Syria
wameuteka na kutwaa uthibiti wa vituo kadhaa vya kuvuka mpaka kuingia nchini Iraq na
Uturuki.
Naibu
waziri wa mambo ya ndani wa Iraq ,
amesema wapiganaji wa waasi wa Free Syrian Army, wametwaa uthibiti wa kituo
kinachotumiwa kuingia nchini humo kutoka Syria .
Katika
kituo kingine cha mpakani nchini Iraq ,
maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema wanajeshi wa waasi wamewauawa
takriban wanajeshi 20 wa serikali ya Syria .
Kituo
muhimu cha kuingia Uturuki kutoka Sria cha Bab al Hawa pia kilitwaliwa na waasi
hao, lakini wameanza kuondoka.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment