SERIKALI YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR
WIZARA YA HABARI
UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
Tel: 0255 24
2237325/0255 24 223 7313
Maelezo
Fax: 0255 24 2237314
E-mail:habarimaelezo@yahoo.co.uk,
maelezozanzibar@zanlink.com
maelezozanzibar@hotmail.com,
maelezozanzibar@gmail.com
TAARIFA YA SMZ KUHUSU AJALI
YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOLEWA
USIKU HUU JULAI 19,2012
Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imetoa taarifa usiku huu ikieleza idadi ya watu waliopatikana
wakiwa hai ni 146 na
kupata maiti 62.
Akitoa taarifa hiyo kwa
vyombo vya habari usiku leo,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Ali Juma Shamuhuna
alisema taarifa hiyo ndio sahihi na kuwataka wananchi kutoamini taarifa
zinazotolewa na watu
wengine zaidi ya Serikali.
Waziri Shamuhuna alisema
kwamba maiti 62 walipatikana ambao kati ya maiti hizo watoto ni
9 na kuna raia mmoja wa
kike wa kigeni ambaye hakuweza kutambulika Uraia wake,lakini
umeonekana picha yake
moja ndogo ya hati ya kusafiria.
Waziri Shamuhuna alisema
meli hiyo ilibeba jumla ya abiria 290 kati ya hao watu wazima 250,
watoto wadogo 31 na
mabaharia 9.
Waziri huyo aliwataka
wananchi katika sehemu mbalimbali hasa katika vijiji vilivyo
kandokando ya bahari
watakapoona maiti au mtu akiwa hai ambaye wanadhani ni wa ajali ya
Meli ya Skagit .
Aidha, Waziri Shamuhuna
alisema kwamba kwa wakazi wa Jiji la Dar
es Salaam ambao
watakuwa na wasiwasi wa
kutowaona ndugu na jamaa zao amewataka kufika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa
zaidi au kuripoti habari za kupotelewa kwa
ndugu au jamaa zao.
Kwa upande wa Zanzibar , Waziri huyo
aliwataka wananchi kufika kwa Masheha wao kutoa
taarifa kama hizo.
Serikali imewashukuru
makampuni binafsi za usafiri baharini kwa msaada wao na wasisite kutoa
msaada katika kazi
inayoendelea ya kutafuta watu au maiti wengine katika eneo la tukio.
Meli ya Mv. Skagit
ilizama Julai 18,2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe umbali wa maili sita
kuelekea Kusini mwa
Kisiwa kidogo cha Yasin Zanzibar
ikitokea Bandari ya Dar es Salaam
ilikoanza safari saa
5:30 asubuhi.
Meli hiyo inamilikiwa na
Kampuni ya Sea Guall Sea Transport Ltd, Kampuni ambayo Meli yake
nyengine ya Mv. Fatih
ilizama ikiwa Bandarini Malindi Zanzibar na kufariki watu sita mwaka
2009.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO)
ZANZIBAR
JULAI 19,2012

No comments:
Post a Comment