UFAFANUZI KUHUS
FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.
Kumb. Na.
AE/164/334/Vol.II/2
Makamu wa Rais,
Corporate Affairs
Barrick Gold
S.L.P 1081
Dar-es-Salaam
UFAFANUZI KUHUS FAO LA
KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA
MIFUKO YA HIFADHI YA
JAMII.
Ufuatao ni ufafanuzi
mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao
la kujitoa.
20 JULAI, 2012
1. Kama
mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya
Mamlaka zimefanyiwa
marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili,
2012. Sheria hiyo tayari
imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza
kutumika rasmi.
Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini
mwetu bila kubagua sekta
yoyote ile.
2. Kwa mujibu wa
marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits)
yamefutwa na kuanzia
sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa
pale mwanachama
alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko
atapata mafao yake pale
atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55)
au kwa lazima (miaka 60)
au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
3. Kwa kuzuia fao la
kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya
nyumba kwa kutumia
dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa
kwenye
Sheria ya SSRA kipengele
cha 38.
4. Marekebisho hayo
kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza
lengo na madhumuni ya
hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa
mwanachama anapostaafu
anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu
maisha ya uzeeni wakati
ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.
Mafao ya kujitoa
yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi
pale anapoumia kazini au
anapofika uzeeni.
5. Tunawaomba
muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya
hifadhi ya jamii.
Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia
1
wafanyakazi kuendesha
maisha yao
wakati wanapokuwa wameishastaafu
tayari. Umasikini wa
kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu
kukabiliana nazo kwa mtu
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena
muelimishe wafanyakazi
kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na
Mamlaka pale ufafanuzi
zaidi utakapohitajika
6. Kwa kuwa marekebisho
hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama
sheria, mafao ya kujitoa
hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha
kazi kwa sababu ya
marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea
haki wao wenyewe na pia
itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa
kanuni za mafao ambayo
lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama,
kanuni hizo zitajadiliwa
na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri
ili kupata maoni yao .
7. Tafadhali
muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa,
mafao mengine ambayo ni
muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa
ulemavu
8. Tumesikia kwamba
tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na
fao la kujitoa.
Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo
kinyume cha Sheria kwani
katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda
kusisitiza kwamba
wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.
9. Tunapenda
kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama
yatalindwa na hakuna
mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.
Mamlaka imepanga
kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la
kwanza la mwezi Agosti
2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.
Tunatanguliza shukrani
za dhati kwa ushirikiano.
Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
No comments:
Post a Comment