Tamasha la Utamaduni Handeni kufanyika Desemba 14
Na Mwandishi Wetu, Handeni
TAMASHA la Utamaduni lililopewa jina
la ‘Handeni Kwetu 2013’ linatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani
Handeni, mkoani Tanga, likiwa na lengo la kutangaza sekta ya utalii na
utamaduni wilayani humo.
Handeni Kwetu
linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa wilaya hiyo inayoongozwa kwa
sasa na Mkuu wa wilaya Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza jana wilayani
Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wameamua kuandaa
tamasha hilo ili kushirikiana na wadau wote kutangza utamaduni nchini Tanzania.
Alisema kadri siku
zinavyozidi kusonga mbele, jamii nyingi zimekuwa zikiiga tamaduni za watu hasa
kutoka nje ya nchi, jambo linaloleta mkanganyiko wa kiasi kikubwa.
“Tumeamua kuandaa
tamasha hili kwa kupitia kampuni ya Raha Company and Entertainment, ambapo
lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio makubwa.
“Mipango kabambe
inawekwa kulifanya tamasha letu liwe na mguso wa aina yake, ukizingatia kuwa
linafanyika mwishoni mwa mwaka, hivyo tunaamini watu wengi watashiriki na sisi,
hasa wale waliokuwa kwenye kipindi cha mapumziko ya mwisho wa mwaka,” alisema
Mbwana.
Mbali na kufanya tamasha
la Utamaduni wilayani humo, pia kutafanyika mchezo wa riadha kwa ajili ya
kuzindua hamasa katika mchezo huo wilayani Handeni, mkoani Tanga.
HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
24 Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment