Thursday, January 31, 2013

Waswahili hawajakosea waliposema kwenye fungu huenda nyongeza...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
  Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.
  Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha,
Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini. Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.
  Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.
  Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013. Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
  Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013

Gharama za kupiga simu zapungua Tanzania..



GHARAMA za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu za mikononi kwenda mwingine nchini kuanzia Machi Mosi, mwaka huu, zitashuka kutoka Sh. 115 hadi Sh. 34.92 kwa dakika moja.

Uamuzi huo umefanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa kampuni za simu nchini wa mwaka 2013, pia kuanzia Januari Mosi, mwakani, gharama hizo zitapungua hadi Sh. 32.40.

Vilevile, Januari, 2015 gharama hizo zitashuka hadi Sh. 30.58; Januari, 2016 zitashuka hadi Sh. 28.57 na Januari, 2017 zitashuka hadi Sh. 26.96 kwa dakika moja.  Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma pichani, alisema umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2003 Sura 172.

Profesa Nkoma alisema viwango hivyo ni vya kikomo cha juu na pia ni elekezi, lakini akasema kampuni za simu zina uhuru wa kukubaliana kibiashara ili mradi makubaliano yao yasizidi gharama zilizoelekezwa na TCRA. Alisema gharama hizo zitatumika kwa mawasiliano ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na simu za kimataifa zinazoingia katika mitandao nchini. 

Hivyo, ameziagiza kampuni zote za simu kufanya makubaliano mapya baina yao na kuwasilisha nakala ya makubaliano kwa TCRA ifikapo Machi 31, mwaka huu. Alisema gharama hizo zimeshushwa ili kuwafanya watumiaji wa simu kuwa huru kupiga simu kwenda mtandao wa kampuni yoyote ya simu na kuwaondolea mzigo wa kubeba ‘laini’ nyingi za mitandao tofauti ya simu kwa wakati mmoja.

Pia alisema ana imani kuwa uchangiaji wa matumizi ya miundombinu na matumizi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (Ucaf) na mkongo wa taifa wa mawasiliano, ndiyo suluhisho la kushuka kwa gharama za uendeshaji na kuenea kwa mawasiliano vijijini.

Alisema watumiaji wa simu za mikononi wamekuwa wakilazimika kubeba ‘laini’ za mitandao tofauti, ambazo kila moja huitumia kupiga simu kwenda kwenye mtandao unaofanana nayo.
 Profesa Nkoma alisema wamekuwa wakifanya hivyo ili kukwepa kutozwa gharama kubwa za kupiga simu kutoka mtandao mmoja wa simu za mikononi kwenda mwingine.

 Alisema uamuzi wa kushusha gharama za mwingiliano wa mawasiliano ya simu za mikononi utakuwa sheria, ambayo kampuni zote za simu zitalazimika kutii.

 “Sasa hivi tuna mitandao kama saba ya simu. Ni bughudha kwa wananchi kutembea na mzigo wa ‘sim card’ (‘laini’) ili kukwepa gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine,” alisema Profesa Nkoma na kuongeza:

 “Sisi kama mdhibiti tunaona hali hii si nzuri. Tunataka mtu awe huru kupiga simu mtandao wowote.”  Hata hivyo, alisema kama itatokea sababu ya bei hizo kuangaliwa upya, TCRA itafanya hivyo.  Alisema suala la kushuka kwa gharama za mwingiliano wa mawasiliano ya simu kutoka mtandao wa kampuni moja kwenda mwingine, hivi sasa linatumika duniani kote, zikiwamo nchi jirani, kama vile Kenya, Uganda na Rwanda. 
Chanzo: Nipashe.

Natamani kuwa wa kwanza kupata picha ya msanii Lulu akiwa katika kaburi la Kanumba.

Hapa Elizabeth Michael aka Lulu akizungumza na wanahabari baada ya kupata dhamana katika mahakama kuu Dar es Salaam juzi, dhidi ya kesi inayomkabili baada ya kuwa mtu wa mwisho kushuhudia Steven Kanumba akiwa hai.

Wanawake wengi wanapenda urembo, ila urembo unaishia kuwatesa....

                          It can't be just a coincidence that all of them became the victims of high hills...

Brighter than a thousand suns: Eyes that have seen a nuclear blast.




She is called Hibakusha, the girl witnessed the explosion of atomic bombings of Hiroshima and Nagasaki in Japan 1960's. America are behind this, they were called uncle Tom because the plane dropped the bombs named toms.

Wednesday, January 30, 2013

Mungu niepushie kuomba...


Kusema nisaidie, kwangu neno takilifu
Mola wangu nepushie, kulisema menikifu
Hekima nizidishie, moyo usiwe dhaifu
Kuomba kwaniumiza, madhali ninazo nguvu

Japo mimi masikini, nafsi yangu naisifu
Sitoranda mitaani, jina liwe maarufu
Nikaitwa maluuni, kwa kukodolea sefu
Za matajiri wachoyo, wanaosimanga watu

Mungu amenipa nguvu, na viungo kamilifu
Roho yangu si legevu, naushika msahafu
Naapa kwa wapumbavu, waliojipanga safu
Wakingoja nianguke, waruke wakinicheka

Kusimbuliwa sitaki, sipendi hiyo harufu
Bora kukosa riziki, kuliko kujikashifu
Mola ndie mstahiki, kwa yoyote mausufu
Hutenda cha madhukura, kisha akabaki kimya

Ni bora nikalimbika, kesho nipate sufufu
Watu watanikumbuka, si nyinyi wababaifu
Wanangu wakinizika, warithi mali nadhifu
Haitokuwa ya wizi, wala ya kudhulumiwa

Ninausulubu mwili, kwa kula mlo hafifu
Ili nitafute mali, kwa hasira kama pofu
Kuepuka udhalili, wa kuomba kiudufu
Mola aniepushie, kuwa mfano mbaya

Kaditama beti saba, tungo hii maarufu
Meandika kwa mahaba, si tambo na majisifu
Kuiandika katiba, hako wa kunikashifu
Iwe mbaya kwa kusoma, na maudhui sharifu

HAFIDH KIDO
Dar es Salaam, Tanzania
30/01/2013

Tuesday, January 29, 2013

Soma msimamo wa chadema kuhusu gesi uliowekwa wazi na Mnyika leo makao makuu...

John Mnyika Mbunge wa Ubungo na waziri kivuli Nishati na madini.


Maelezo kuhusu maamuzi ya Baraza Kuu nimeyaambatanisha. Lakini pia unaweza kunukuu kutoka majibu ya nyongeza niliyoyatoa mbele ya wanahabari leo tarehe 29 Januari 2013 wakati wa mazungumzo yangu nje ya maelezo niliyoyambatanisha kutokana na habari za leo kuwa CCM kupitia kwa Kinana na Nape imesema kwamba madai ya wananchi wa Mtwara ni ya msingi.
Kinana hana uhalali wa kuwatetea wananchi kuhusu gesi kwa kuwa yenye ni mmoja watuhumiwa wa kuwakosesha wananchi wa Mtwara manufaa ya Gesi, alikuwa alikuwa ni sehemu ya uongozi wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Artumas na alishiriki kuwakosesha wananchi wa Mtwara fursa ya umeme wa MW 300 zilizopaswa kuzalishwa Mnazi Bay toka mwaka 2009. Hatua ambayo kama ingefanyika toka wakati huo mgogoro wa gesi usingekuwa kwa kiwango cha sasa. Kinana badala ya kujifanya kuwatetea wananchi wa Mtwara awaeleze alilipwa kiasi gani na kampuni hiyo na kwanini hakutetea maslahi ya wananchi toka wakati huo.
Kinana na Nape wazingatie kuwa CCM haina uhalali wa kuwatetea wananchi wa Mtwara kwa kuwa mgogoro huo ni matokeo ya sera bomu na uongozi mbovu chini ya chama hicho ambao umeruhusu ufisadi katika sekta hiyo na kukosesha wananchi  manufaa ya gesi hiyo katika miradi ya toka mwaka 2004 hali ambayo imefanya wananchi kuandamana kutaka manufaa ya sasa. Kinana na Nape badala ya kuisukumia Serikali mzigo wa kwenda kukutana na wananchi, CCM ijieleze ni kwa nini kwa miaka mingi imetoa ahadi za uongo kuhusu uendelezaji wa miradi ya gesi kwa wananchi wa Lindi na Mtwara na pia sababu za kushindwa kuisimamia Serikali kutekeleza miradi ya gesi na umeme Mtwara ikiwemo wa MW 300 wa Mnazi Bay.
Kauli za Kinana na Nape kuhusu gesi Mtwara ni za kinafiki kwa kuwa msimamo wa Serikali na CCM ulishatolewa na Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa kuyapinga madai hayo ya wananchi. Kikwete alizungumzia  hayo kwenye hotuba yake kwa taifa tarehe 31 Disemba 2012 na kuyapinga tena katika kauli zake mwezi Januari mwaka 2013.
Mara baada ya Kikwete kuyakataa madai ya wananchi, wananchi waliendelea kuwa na msimamo na wengine wakitaka kupata msimamo wa CCM sio wa Serikali na hatimaye mwanzoni mwa mwezi Januari 2013 Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula alisema CCM haikubaliani na madai ya wananchi na akawaita wanaCCM wachache na wananchi wengi wenye madai hayo kuwa ni ‘waasi’.
Hivyo, Kinana na Nape ambao sio wasemaji wakuu wasitoe kauli za kinafiki za kujikosha baada ya kauli za Rais  Kikwete, Mangula na viongozi wengine wa CCM na Serikali kuchochea vurugu.
Kauli za kujikosha za Kinana na Nape haziwezi kurudisha nyuma vuguvugu la wananchi kufanya mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani kupitia chaguzi za mwaka 2014 na 2015 na kuiunga mkono CHADEMA katika mwaka 2013 na kuendelea kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za taifa pamoja  na kuwa na sera sahihi zenye kuwezesha maendeleo endelevu ya wananchi na nchi kwa ujumla.
John Mnyika (Mb)

Monday, January 28, 2013

Kombe la mataifa Afrika lilianza na timu tatu mwaka 1957...





Kombe la Mataifa ya Afrika lililoanzishwa mwaka 1957 limeongezeka umaarufu katika macho ya wapenda soka si barani Afrika tu bali dunia nzima, kwani vilabu vya mpira wa miguu hasa barani Ulaya hutumia michuano hii kuchukua wacheaji wa kuwasaidia kwenye timu zao.

Kombe hili lilianza kwa kushirikisha timu tatu tu nchini Sudan lakini sasa kuna timu 16 zinazowania kombe hilo linaloshikiliwa na timu ya Zambia lililobeba kwa mara ya kwanza mwaka 2012.

Nchi ya Misri ndiyo ya kwanza kunyanyua kombe hilo nchini Suda baada ya kuwafunga Ethiopia magoli 4-0 katika fainali, na hiyo imekuwa kama nyota njema kwa nchi ya Misri kuendeleza ubabe wa soka barani Afrika kwa kuchukua kombe hilo mara saba tangu kuanzishwa kwake mwaka huo wa 1957.

Orodha ya timu zilizochukua kombe la mataifa ya Afrika ni kama ifuatavyo:

1957: katika timu nne zilizothibitisha ushiriki Afrika Kusini ilijitoa katika mashindano na kuzibakisha timu tatu za Misri, Sudan na Ethiopia. Misri wakawa mabingwa wa kwanza wa kombe hilo kwa kuwachapa Ethiopia 4-0 katika fainali.

 1959 : Misri walichukua ushindi kwa mara ya pili mfululizo wakiwa nyumbani katika michuano hiyo iliyoshirikisha timu tatu tu za Sudan, Ethiopia na wenyeji Misri. Katika fainali Ethiopia walikubali uteja kwa mara ya pili kwa kulazwa 4-0.

1962 : Ethiopia waligoma kugeuzwa kichwa cha mwendawazimu na Misri kwa kutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kuichapa Misri 4-1 katika muda wa nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kuisha kwa suluhu. Mchezaji wa Ethiopia Menguistu Worku, ndie alieiwezesha nchi yake ya Ethiopia kuwa wafalme wa soka barani Afrika kwa mara ya kwanza kwa kuingiza magoli mawili peke yake katika dakika za nyongeza. Tunisia na Uganda zilishiriki kwa mara ya kwanza na kufanya idadi kutoka tatu mpaka tano

1963 : Wenyeji Ghana waliutumia vema mji wa Accra kwa kunyakua kombe hilo mara ya kwanza kwa kuichapa 3-0 Sudan katika fainali. Mwaka huo timu ziliongezeka na kufikia sita,

Kadhalika fainali za mwaka hu rikodi ya mabao 6-3 iliyowekwa na Misri dhidi ya Nigeria ndiyo idadi kubwa ya magoli iliyowahi kufungwa katika mechi moja ya michuano hiyo ya kombe la Afrika mpaka sasa.

1965: Ghana waliendeleza ubabe kwa kuwaaibisha wenyeji Tunisia kwa mabao 3-2 kwenye fainali katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kuisha kwa suluhu. Mwaka huu wa 1965 timu mbili za DRC Congo na Ivory Coast ziliongezeka.


1968 : Congo DRC walinyakua ubingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia kwa kuifunga Ghana walioingia kwenye hatua ya fainali kwa mara ya tatu mfululizo tangu kuanza kushiriki mwaka 1963, bao pekee la Pierra Kalala ndilo lililozamisha ndoto za Ghana kuchukua kombe hilo mara ya tatu mfululizo.

1970: Kwa mara nyingine tena Ghana walinyang’anywa tonge mdomoni na Hassabou el Saghir katika fainali iliyoisha kwa Ghana kulala bao 1-0. Hii ilidhihirisha kuwa kwa kipindi hicho Ghana ndiyo ilikuwa timu bora ya Afrika inayocheza soka la hali ya juu mpaka kufanikiwa kuingia fainali za Afrika mara nne mfululizo na kufanikiwa kushinda mara mbili mfululizo, yaani mara ya kwanza waliposhiriki na mara ya pili kushiriki


1972:  Kwa mara ya kwanza na mwisho nchi ya Congo Brazzaville kuchukua kombe la Afrika ni mwaka huo wa 1972 nchini Cameroon katika mji wa Yaounde ambapo mchezaji wa Congo Brazzaville Micahel M’Bono alitumbukiza wavuni mabao matatu peke yake na kuitoa kichwa chini Mali kwa mabao 3-2.

1974: Huu ndiyo mwaka pekee katika historia za michuano ya kombe la Afrika mchezo wa fainali kurudiwa, ambapo katika mchezo wa kwanza DRc Congo walifungana 2-2 na Zambia nchini Misri, kutokana na sababu zisizozuilika mchezo uliahirishwa na kuchezwa siku mbili baadae.

Katika mchezo wa pili Zambia walilala kwa mabao 2-0 hivyo DRC Congo kuwa mabingwa kwa mara ya pili tangu walipochukua kwa mara ya kwanza mwaka 1968 nchini Ethiopia. Mchezaji wa DRC Congo Mulamba Ndaye ndie alieibuka kidedea kwa kuweza kuifungia mabao yote ya usindi katika mechi zote mbili, yaani ile ya kwanza iliyoisha kwa 2-2 na ya pili iliyorudiwa ya mabao 2-0.

1976: Haya ndiyo mashindano ya pili na ya mwisho kuamuliwa kwa mfumo wa ligi na Morocco kushinda kwa point moja mbele ya Guinea baada ya timu hizo kutoka suluhu ya 1-1 katika mechi ya mwisho nchini Ethiopia. 

1978: Ghana walichukua kikombe kwa mara ya tatu nyumbani kwao Accra, baada ya mchezaji wao Opoku Afriyie kutumbukiza mabao mawili katika fainali dhidi ya Uganda walioingia hatua ya fainali kwa mara ya kwanza hivyo kuoshia nafasi ya pili kwa kufungwa 2-0.

1980: Nigeria walitumia vema uwanja wa nyumbani kwa kuichapa Algeria mabao 3-0 katika fainali iliyotawaliwa na mchezaji wa Nigeri Segun Odegbami kufunga mabao yote matatu, na kuwa washindi wa kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

Itakumbukwa katika mwaka huu Rais wa TFF Leodger Tenga aliongoza kikosi cha Taifa Stars nchini Nigeria kushiriki kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho michuano hii.


1982: Ghana walifanikiwa kuchukua kombe hili kwa mara ya nne dhidi ya Libya kwa mikwaju ya penalt 7-6 na kuweka historia kuwa fainali za kwanza  za kombe la Afrika kuamuliwa kwa mikwaju ya penalt. Katika fainali hizo ndipo jin ala Abedi Pele alietokea ‘benchi’ na kuonyesha kipaji cha hali ya juu mbali ya umri wake mdogo hivyo kuwa nyota wa soka barani Afrika na dunia kuanzia mwaka huo.

1984:  Kwa mara ya kwanza Cameroon walichukua kikombe hicho katika fainali iliyowakutanisha na Nigeria ambapo walishinda 3-1.

1986: Cameroon walifanikiwa kuingia fainali kwa mara ya pili lakini wakafungwa na Misri kwa mikwaju ya penalt mbele ya mashabiki 100,000 nchini Misri kwenye uwanja wa Cairo Stadium.

1988: Kwa mara ya tatu mfululizo Cameroon waliingia fainali lakini walionyeshwa upinzani mkubwa na Nigeria kabla ya mchezaji wa Cameroon Emmanuel Kunde kuifungia timu yake kwa penalt pekee hivyo Nigeria kulala 1-0 mjini Casablanca.

1990: Algeria iliifunga Nigeria 5-1 hivyo kutawazwa mabingwa wa soka barani Afrika kwa mwaka huo wa 1990.


1992: Kombe la Afrika liliongeza mwamko na kufikia timu 12, kichekesho kilikuwa siku ya fainali ambapo Ivory Coast iliilaza Ghana kwa penalt 11-10 baada ya muda wa kawaida na muda wa nyongeza kuisha kwa suluhu nchini Senegal.

1994: Zambia walifika fainali ingawa walipoteza karibu kikosi chote katika ajali ya ndege miezi kadhaa nyuma nchini Gabon, lakini Nigeria haikuwaonea huruma baada ya kuwatundika goli 2-1 katika fainali hiyo ambapo goli zote mbili za Nigeria ziliingizwa kimiani na Emmanuel Amunike aliekuwa akiwika sana kwa miaka hiyo.

1996: Kwa mara ya kwanza fainali za kombe la Afrika lilishirikisha timu 16 cha kutia matumaini nchi ya Afrika Kusini ilirudi katika michuano baada ya matatizo ya ubaguzi wa rangi nchini mwao kuwatoa katika fainali za kwanza kabisa mwaka 1957.

Mark William wa afrika Kusini aliwakatili Tunisia kwa kutumbukiza goli mbili peke yake hivyo Tunisia kulala 2-0 na afrika kusini kuchukua kikombe kwa mara ya kwanza.




1998: Kuonyesha wana kiu ya michuano hiyo Afrika Kusini waliingia fainali kwa mara ya pili mfululizo lakini Misri waliwatuliza na kuwachapa 2-0 mjini Ouagadougou.

2000: Nigeria kwa mara ya kwanza waliondoa kasumba ya wenyeji kufungwa katika fainali baada ya kuichapa Cameroon kwa mikwaju ya penalt 4-3 baada ya suluhu ya 2-2 katika dakika za kawaida na nyongeza.
 

2002: ilikuwa ni nchini Mali ambapo Cameroon walitawazwa mabingwa wa Afrika kwa mikwaju ya penalt dhidi ya Senegal iliyokuwa na vinara wa soka kama El-Hadji Diouf.

2004: Wenyeji Tunisia walibeba kikombe cha Afrika baada ya kuwachapa Morroco 2-1.

2006: Misri walitawazwa mabingwa kwa mara nyingine baada ya kuwachapa Ivory coast waliokuwa na kikosi imara kilichoongozwa na Didier Drogba.

2008: Misri waliendeleza ubabe na kunyakua ushindi wa Afrika tena baada ya mshambuliaji wao hatari Mohammed Aboutrika kuwainua mafarao hao dakika 13 kabla ya mchezo kuisha hivyo Ivory Coast kulala 4-1 dhidi ya Misri kwa mara ya pili mfululizo.

2010: Ilikuwa ni mwaka wa maajabu katika michuano hii baada ya
Misri kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo kwa mara tatu  mfululizo ilikuwa ni mjini Luanda dhidi ya Ghana na kuifanya Misri mababa wa soka la Afrika kwa kuchukua kikombe hicho kwa mara ya saba.

2012: Zambia walinyakua kikombe hicho kwa mara ya kwanza baada ya tambiko lao mjini Gabon katika eneo walilopoteza wachezaji wako kwa ajali ya ndege. Mikwaju ya penalt 8-7 dhidi ya Ivory Coast iliamsha furaha ya wapenzi wa soka barani Afrika kwani watu wengi walikuwa wakiwaonea huruma Wazambia kutokana na dua walizokuwa wakiomba ili kuweka historia ya michuano hiyo.


Hafidh Kido
Dar es Salaam, Tanzania
29/01/2013

CHADEMA wajigawa kimajimbo kuonyesha umuhimu wa kuwa na serikali ya majimbo.

 Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika ni miongoni mwa viongozi vijana wa chama hicho wenye mvuto kwa wananchama wengi wa chadema.

 Chadema NEC wakisema peeeoopleeee poweeerrr katika ukumbi wa Diamond Jubelee jana.

 Aliekuwa naibu katibu mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na diwani wa Babati vijijini Lawrence Tara akikabidhiwa kadi ya CHADEMA kuashiria kujiunga na chama hicho jana.


Zitto Zuberi Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA ambae pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho pia ni miongoni mwa viongozi wenye mvuto sana. Hapa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho jana.


Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono wananchi wa mikoa ya kusini kuhusu suala la gesi na kuweka wazi kuwa ifike wakati kila mkoa ujivunie rasilimali yake.

Akizungumza katika mkutano wa dharura wa baraza kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam jana Mbowe aliweka wazi msimamo wa chama chake na kusisitiza suluhisho la matatizo ya ugawanyaji finyu wa rasilimali za taifa ni kuleta serikali ya majimbo.

Kwa kudhihirisha hayo Mbowe amekigawa chama chake katika majimbo kumi ambayo yatakuwa yanafanya maamuzi kwa kujitegemea bila kuingiliwa na makao makuu.

Tumeamua kuwa mfano kwa serikali, tunagawa majimbo ili kuondoa dhana kuwa makao makuu yanaamualia mambo ya msingi mikoa. Kwa kufanya hivyo tutaondoa dhuluma inayofanywa na serikali kuu kwa kuwa watu wachache wa Dra es Salaam ndiwo wanaofaidi rasilimali nyingi zilizopo hapa nchini kwa kukaa tu Dar es Salaam wanavuna rasilimali mikoani na kuzuleta hapa halafu wanazichakachua.

“Angalia mkoa wa Geita, mgodi wa Geita unazalisha dhahabu nyingi kuliko migodi yote Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika, lakini Geita ndiyo mkoa maskini kuliko mikoa yote. Watu wa Mtwara na Lindi wana haki kufanya walichofanya kwani ni haki yao,” alisema Mbowe.

 Akifafanua mpango mkakati wa kuchukua nchi mwkaa 2015 mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Mbowe alisema chadema imelenga kufanya mabadiliko ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa kwenda katika majimbo na kukipanga upya chama hicho kwa mustakabali wa taifa. “Mtakumbuka kwamba wakati tunakianzisha chama chetu, tulizungumzia sera ya majimbo na kuainisha kazi zake…sasa tumeanza kupanga kazi zenyewe kwa kugawa majukumu katika kanda kumi. “Tunataka tuishi vile tunavyosema kwa kuwa katika miaka mingi ya kuwa chini ya uongozi wa serikali ya CCM, wananchi wamekuwa wakiamriwa mambo yao na kundi dogo la watu wanaojikusanya sehemu moja ya nchi, hilo kwetu si mfano bora wa uongozi,” alisema.

Mbowe aliongeza kuwa katika miaka 20 ya kuhimili misukosuko ya kisiasa chama hicho kimejifunza mengi na sasa kiko tayari kushika dola ndio maana wameanza kugawa majukumu kwa wananchi kupitia uongozi wa kikanda. Alisema kuwa wamejiandaa kwa mashambulizi ya aina zote na sasa jukumu kubwa la kila kanda litakuwa ni kuhakikisha kila mwananchi anaiunga mkono CHADEMA katika eneo atakalokuwa.
Mwenyekiti huyo alitaja kanda hizo na mikoa husika kuwa ni
1.    Kanda ya Ziwa Magaharibi (Mwanza, Geita, Kagera),
2.    Ziwa Mashariki (Mara, Simiyu, Shinyanga),
3.    Ziwa Magharibi (Kigoma, Tabora, Katavi)
4.    Kati (Singida, Dodoma, Morogoro).
5.    Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Ruvuma, Iringa),
6.    Kusini (Lindi na Mtwara),
7.    Mashariki (Pwani, Dar es Salaam na Tanga),
8.    Kaskazini (Kilimanjaro, Manyara, Arusha),
9.    Pemba na Kanda ya Unguja.

Mbowe alisema katika kuhakikisha vikosi hivyo vinafanya kazi zake vizuri, kila kanda itajengewa ofisi, kununuliwa magari, pikipiki na vifaa vyote vya ofisini na za mikutano. “Lengo la mkakati huo pia ni kuhakikisha CHADEMA inasimama katika chaguzi zote bila kupingwa…tunataka CCM ndiyo ipingwe katika chaguzi na hili tutalifanikisha,” aliongeza.

Katika suala zima la Muungano, Mbowe alisema uwepo wa serikali tatu hauepukiki kwa kuwa tayari Tanzania Visiwani wameshakuwa na serikali yao hivyo ni jukumu la Watanzania Bara kupata serikali ya Tanganyika na kisha kuwepo na serikali ndogo ya Muungano. Alisema serikali tatu inawezekana ikiwa viongozi wataacha unafiki wa kusema muungano utavunjika huku tayari wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais, bendera na wimbo wao ya taifa. Tunawaunga mkono wenzetu Wazanzibar katika kupigania uhuru kamili na kwa sasa sisi ndio tunaoonekana wa ajabu kushindwa kuuliza serikali ya Tanganyika,” alisema.

Mbowe pia aligusia tume huru ya uchaguzi akisema serikali ihakikishe Watanzania wanapata tume hiyo kwa kuwa tayari hata viongozi wa chombo hicho wameshatoa maoni na kutaka wapewe uhuru wa kufanya kazi.
Alisema serikali kama inafikiri kuwa CHADEMA itaingia katika uchaguzi wa 2015 ikiwa chini ya tume iliyopo sasa watakuwa wanajidanganya na badala yake watalazimisha upatikanaji wa tume hiyo.
Hafidh Kido
Dar es Salaam, Tanzania
kidojembe@gmail.com
29/01/2013



CORD presidential candidate Raila Odinga launches his manifesto, pledging to transform Kenya into an economic power house.


GUARANTEEING A NEW CONSTITUTION AND AN ETHICAL GOVERNANCE AGENDA
FOSTERING PROSPERITY AND ERADICATING POVERTY
INVESTING IN INTRASTRUCTURE
CREATING OPPORTUNITIES FOR EMPLOYMENT
FIGHTING CRIME,DRUGS & INSECURITY
ADVANCING QUALITY EDUCATION
DELIVERING UNIVERSAL HEALTH CARE
EMPOWERING WOMEN
HARNESSING THE POTENTIAL OF OUR YOUTH
ENHANCING MANUFACTURING,ICT,TRADE AND SERVICES FOR ECONOMIC GROWTH
INCREASING VALUE IN AGRICULTURE,FISHERIES AND LIVESTOCK
CONSOLIDATING AND EXPANDING TOURISM
BUILDING AFFORDABLE HOUSING & IMPLEMENTING LAND REFORM
ENSURING CLEAN WATER,EFFICIENT SANITATION AND EXPANDING IRRIGATION
DEVOLVING POWER
AVING OUR ENVIRONMENT
ENSURING DISABILITY RIGHTS
PROMOTING OUR HERITAGE,CULTURE,MEDIA & SPORTS
MAXIMIZING THE POTENTIAL OF OUR DIASPORA
PURSUING A PROGRESSIVE PAN-AFRICAN AND FOREIGN POLICY

No Women no cry... really?


By Lance Guma dual
Mutsenhu confronted Ambassador Wharton during his brief tour of the American Corner at the Turner Memorial Library near the Civic Centre in Mutare. She took off her clothes leaving only her black undergarments.
“Our beautiful country is reeling under the effects of illegal sanctions imposed by the West, yet we have an Ambassador coming here to tour what they say are developmental projects,” she said parroting the Zanu PF line.
“How can they say they are developmental projects which employ a few people, yet the majority of Zimbabweans are wallowing in abject poverty due to the effects of sanctions?
“Poverty is well documented in most communities because of the sanctions, our hospitals have no medication and unemployment is rife everywhere, yet we have an ambassador who is doing nothing to have the sanctions lifted,” she said.
Last year in September the Zanu PF Manicaland Province was forced to disown Mutsenhu after she led violent clashes over the ownership of the new Sakubva flea market. She bussed in youths to take over the new flea market, but some other youths from Zanu PF resisted the move.
A party official at the Zanu PF provincial headquarters office said “she is a political chancer. She uses names of Zanu PF senior officials to arm twist her selfish gains. She is active wherever she feels that there are financial gains”.
“Where was she during the 2005 and 2008 elections? As a party we do not know her and if the senior party officials do not act on her, the party is going to regret it very soon because she is tarnishing the image of the party,” the Zanu PF official said.

Sikiliza Barwany gesi haiwezi kubaki Lindi, waambie wenzio waache tabu tutaelewana mezani... sawa?


Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.

Kumbe Lulu bado hajaachiwa, kuna mambo ya kidhamana yalikuwa hayajakamilika...


Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana huu, dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu atatimiza masharti aliyotengewa ambayo ni
·         Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
·         Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
·         Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
·         Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Pamoja na kwamba familia ya Lulu walikuwa wameshajiandaa kukabiliana na kutimiza masharti hayo, Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa serikali(Mahakama) ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo kutokana na kuwa safarini mkoani Pwani kikazi.

 Hata hivyo, kwa mujibu wa mawakili wanaomwakilisha Lulu, masharti yote ya dhamana wameshayatimiza na kinachosubiriwa ni huo uthibitisho na utaratibu wa kimahakama ili Lulu arejee nyumbani na kuendelea kukabiliana na kesi hiyo akiwa uraiani.

Kwa maana hiyo, uwezekano ni wazi kabisa kwamba Lulu ataachiwa rasmi kesho January 29, 2013.
Chanzo: mjengwa

Tuesday, January 22, 2013

Kiongozi wa msafara wa Yanga Uturuki, adhalilisha mwandishi wa habari Michael Momburi.


Na MICHAEL MOMBURI 
ACHANA na safari za ndani ya mipaka ya Tanzania. Nimesafiri na Yanga kwa miaka tofauti kwenye ziara za kikazi katika nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia na Misri. Zote hizo nilisafiri na Yanga kwa mafanikio na kupewa ushirikiano wa kiwango cha juu kutoka kwa viongozi. 

Lakini hakuna safari ya kipuuzi niliyowahi kusafiri nje ya nchi na timu ya Tanzania kama hii nilipokuwa na Yanga mjini Antalya, Uturuki. 

Nimetumia neno upuuzi kwa kuwa hakuna msamiati mbadala wa kuelezea majanga niliyokutana nayo Antalya ambayo yamesababishwa na mtu mmoja ambaye alikuwa na masilahi binafsi ikiwemo kujitafutia umaarufu kwa njia ya kugombana na watu, ingawa baadaye niligundua nikutojiamini kwake. 

Kama kawaida ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kupeleka waandishi wake kwenye safari mbalimbali katika kila kona ya Dunia ili kuwapa Watanzania wanachostahili. 

Kampuni yangu ya MCL ilinigharamia kila kitu na nikakwea ndege na Yanga kwenda Uturuki kufuatilia matukio mbalimbali. Lakini baada ya siku tatu nikaingia matatani na mtu anayeitwa Mohammed Nyenje, ambaye alijitambulisha kama kiongozi wa msafara wa Yanga. 

Sitaki kuingia kiundani historia yake kisoka kwa kuwa hata miaka yangu yote ya kufanya kazi jijini Dar es Salaam sikuwahi kumsikia zaidi ya kumkuta Uturuki. 

Ila nina uhakika ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa Mkuu wa Msafara wa timu kubwa kama Yanga. 

Pia ilikuwa mara yake ya kwanza kuongoza msafara wa timu kwenda barani Ulaya. 

Nyanje pia ni uhakika ni mchanga sana katika uongozi wa soka kwani ndio mara ya kwanza amejipenyeza kwenye duru hizi. 

Nilitua Uturuki, Desemba 31 siku moja baada ya Yanga kufika huko. Nikalazimika kufikia Elegance Palace karibu na Uwanja wa ndege wa Antalya kwa kuwa hoteli niliyokuwa nimepanga kufikia ya Asteria Sorgun haikuwa na nafasi siku husika. 

Kesho yake asubuhi nikachukua Taxi umbali wa dakika 30 kuifuata Yanga na hapo tayari nilishapata ripoti kwamba hawajafikia tena kule walikopanga kufikia awali hoteli ya Seonu ambako ni karibu na Asteria. Walikwenda Fame Residence ambako ni Kilomita tisa mbele. 

Ikabidi nihudhurie mazoezi nitume ripoti Dar es Salaam kisha nichukue Taxi kwenda Asteria kufuta mpango wangu wa kufikia hotelini hapo kwa kuwa waligoma kushughulikia suala langu kwa mawasiliano ya simu kwa madai kwamba nilikuwa nimechelewa vinginevyo nisingekwenda basi wangekata fedha kwenye kadi yangu ya benki. 

Nilipofika kutokana na umbali ikanilazimu kulala usiku mmoja kwa kuwa ni mbali na ilikuwa gharama kubwa kurudi mjini. Hoteli hiyo iko mkabala na Seonu ambako Yanga ilikuwa ifikie, hoteli hizo mbili zote ni maarufu kwa kupokea watu wa Ujerumani na Ufaransa. 

Usiku huo nikiwa mweusi pekee kwenye mgahawa na ufukwe uliokuwa umejaa Wajerumani zaidi ya 250 nikakumbana na manyanyaso na vituko vya ubaguzi wa rangi kutoka kwa Wajerumani hao, muongoza watalii wa Kituruki aliyeshuhudia ikamuuma akanipeleka kwa uongozi wa hoteli ambao ulionekana kunituliza na kuniomba yaishe kutokana na idadi ya Wajerumani hao kuwa wengi mno hotelini hapo na ndio wanamuingizia fedha asingeweza kufanya chochote. 

Nilipogundua kwamba hata Tanzania haina ubalozi Uturuki nikaripoti kwenye gazeti la Mwananchi kesho yake kwamba nimekumbana na vitendo vya kibaguzi kwenye eneo ambalo Yanga ilipanga kufikia. 

Nyanje alipoona habari hizo gazetini akakasirika akaanza kunifokea mbele ya kadamnasi ya wachezaji bila kuelewa chanzo. Akanishusha kidhalilishaji kwenye gari asubuhi nikielekea mazoezini mpaka wachezaji wakashangaa na wengine wakanitumia ujumbe baadae kunituliza na kuniambia hawajafurahishwa na unyama huo. 

Hapo tayari ameshakwenda kwa kocha na kumjaza maneno kwamba nimeripoti Yanga imefanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi kitu ambacho hakikuwa kilichoripotiwa. Kocha Ernest Brandts alikasirika baada ya kupotoshwa na Nyanje ambae alionekana kuwa na malengo yake binafsi kwani tangu mwanzo hakuonyesha ushirikiano alipokuwa akiulizwa mambo mbalimbali. 

Pengine alidanganywa kwa kuzozana na Mwanaspoti na Mwananchi yatampandisha chati kwa Wanayanga kitu ambacho hakikufanikiwa, ingawa baadae wachezaji watano wakubwa na baadhi ya wanachama maarufu wa Yanga walinipigia simu na kunitumia ujumbe wakinisisitizia kwamba hata Ofisa Habari, Baraka Kizuguto ambaye alijifanya rafiki yangu wa karibu sana aliongeza chumvi kwenye malumbano hayo ili awe chanzo pekee cha habari za Yanga na kuupa chati mtandao wa klabu. 

Jambo hilo halikumsaidia pia. 
Huo ulikuwa mgogoro wa kwanza wa kipuuzi na safari ikaonekana ya kipuuzi vilevile ingawa sikukata tamaa kutokana na uzoefu na upeo wangu kwenye kufanya kazi na watu aina ya Nyanje. 

Siku hiyo ambayo ilikuwa ni kama siku ya nne tangu Yanga ianze kambi akatangaza hataki kuniona kambini wala mazoezini na akatangazia ni walinzi wa pande zote mbili huku akizidi kumjaza upuuzi kocha kwa kumuonyesha habari zinazoripotiwa na magazeti ya Tanzania kwa kumnukuu bila idhini yake. 

Watu wa karibu na kocha wakanieleza kuwa anaamini mimi ndiye natuma habari hizo wakati hata magazeti yenyewe siyajui na hayana hata jeuri ya kunitoa Mwanaspoti. 

Bado upotoshaji wa bwana Nyanje unazidi kupata umaarufu na sipewi nafasi ya kukutana na kocha nimuelezee uhalisia na hata akikutana na mimi kwenye mechi hataki hata tuonane uso kwa uso. 

Wachezaji walichukizwa na Mwanaspoti kuzuiwa kuingia kambini huku wengine wakijaribu kuchokonoa uhasama huo ufutike kwa kusaidiana na wazalendo wengine lakini bado kocha akawa ameshiba propaganda za bwana Nyanje ambaye alizidi kujisikia aibu zaidi siku ya mwisho kwa jinsi wachezaji wote walivyonikuta uwanja wa ndege wa Antalya wakati timu inaondoka wakaja kunisalimia na kunitaka kupuuzia yaliyonikuta. 

Kituko cha Pili. Baridi. Siku mbili za awali Antalya ilikuwa na baridi kali na mvua ambayo ililazimisha wachezaji kufanya mazoezi na makoti asubuhi na jioni. 

Nikaripoti uhalisia, Nyanje hataki anataka niseme kuna Jua na hali ya hewa safi kitu ambacho ni uongo siwezi kutumwa na kampuni nije kudanganya Watanzania kwa masilahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu. 

Mimi sio Kanjanja elewa Nyanje. 
Mbona baadae hali ya hewa ilikuwa nzuri na tukaripoti kwamba hali imetangemaa kwa kiasi ingawa jua lilikuwa likiwaka kwa kuambatana na baridi ambayo wachezaji wote walikuwa wakishinda na makoti. 

Nyanje anataka Yanga isifiwe tu kitu ambacho kwa enzi hizi hakiwezekani ndio maana tunajifadhili wenyewe kila kitu tunapokuwa sehemu yoyote ile kuepuka utegemezi na tabia za Kikanjanja. 

Pengine kuna watu wamempotosha Nyanje na kumjaza upepo kwamba akisifiwa, basi akirudi Dar es Salaam atajipatia umaarufu. 

Upuuzi wa tatu. Mechi za kirafiki. Wakala wa Yanga aliwaahidi mechi tatu lakini siku za awali nilikaa na Ofisa wake akanieleza ugumu waliokuwa wakikumbana nao kupata mechi na Kocha wa Yanga pamoja na Nyanje walikuwa wanajua ukweli. 

Ukweli ni kwamba wakala aliwaambia timu zote kubwa za Ligi Kuu ya Uturuki zimewatolea nje hata baadhi za Ujerumani zilifanya hivyohivyo ndio maana wakaishia kucheza na timu za Daraja la Nne na zile za Daraja la Kwanza za Uturuki, Ujerumani na Uholanzi. 

Nyanje kusikia taarifa hizo zimefika Tanzania akazidi kuweka miiba mwandishi isivuke. 

Alitaka uminywe ukweli ukiwemo ule Arminia Bielefeld ya Daraja la Nne huko Ujerumani kudengua kucheza na Yanga ndio maana kipindi cha kwanza ikachezesha kikosi dhaifu cha watoto kabla ya kuingiza timu halisi kipindi cha pili ambao licha ya kucheza kwa kujifurahisha walisawazisha bao moja la Yanga kushambulia lango la Yanga kwa muda wote. Yanga wanataka Mwandishi atumike kuwajaza upuuzi na sifa za kijinga Watanzania. 

Baada ya kutokea kutoelewana kati yangu na Nyanje, uongozi wa Mwanaspoti ulijitahidi kuweka mambo sawa kwa kuanzia na viongozi wakuu wa Yanga walioko Tanzania ambao walichukulia kama changamoto za kawaida na kukubaliana na Mwandishi aendelee kuambatana na timu lakini Nyanje kwa chuki zake binafsi akazidi kuminya na kumzuia mwandishi kuingia kambini na mazoezini kwa kuweka ulinzi getini mpaka wachezaji wakawa wanashangaa. 

Mwandishi akataka kiwepo kikao cha kuelezana hali halisi ili tusigombane kwenye nchi ya watu kwa kuwa wote ni Watanzania lakini bado kiongozi huyo bila ya kujali gharama kampuni ilizoingia kusafirisha mtu mpaka Uturuki na ni chombo pekee cha Tanzania kilichopo Uturuki akazidi kugoma. 

Pengine alifanya hivyo akijua ndiyo njia pekee ya kutangazwa na kujulikana kwa kuwa pengine huenda asipate tena zali kama hilo la kusafiri na Yanga kama kiongozi. 
Nyanje umechemka. 

Unapaswa kujua kwamba huwezi kuwa maarufu au kupata cheo Yanga au kufanikisha mambo yako kwa kupambana na mwandishi wa habari. 

Tafuta njia nyingine kuuza jina lako kwa sera na kuifanyia Yanga mambo ya maendeleo, wenzako hawakutoka kwa njia za kibabaishaji. 

Ni upuuzi kulumbana na mwandishi kutoka chombo kimoja cha habari na kibaya zaidi mkiwa ugenini. 

Katika hali ya ubinadamu, wa kawaida hivi kweli watu wa taifa moja mnakorofishana. 

Hata Muasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Ukila mara moja huwezi kuacha. 

Haikusaidii zaidi ya kufunua upeo wako mbele ya watu wenye fikra chanya ambao wanakutafsiri hasi. 

Popote pale unapokuwa ugenini na Watanzania wenzako unapaswa kuonyesha uzalendo na ushirikiano kwa kuwa siyo watu wote tuko kwa ajili ya Watanzania ambao ni mashabiki na haohao wasomaji wa gazeti wana haki ya kupata ripoti ziwe chanya au hasi ili waelewe hali halisi. Kuna matukio mengi ya aibu yalikuwa yanajiri Uturuki. 

Yanga kwenye mechi ilikuwa haina daktari wake binafsi, wachezaji waliokuwa hawachezi ndio walikuwa wakisaidiana na meneja Hafidh Saleh kusaidia wachezaji waliokuwa wanaumia uwanjani na hakuna huduma waliyokuwa wakipata zaidi ya kusuguliwa na barafu. Mfano mzuri ni kwenye mechi na Arminia yalitokea matukio kadhaa ikiwemo Mbuyu Twite kuumia lakini alisaidiwa hivyo hivyo kimagumashi. 

Gari la wagonjwa lilikuwepo lakini hakukuwepo daktari wa kutoa huduma ya kwanza. Je Nyanje haoni hii ni kuhatarisha maisha ya wachezaji. Hayo tuliyamezea lakini Nyanje anathubutu kukurupuka na kuifukuza Mwanaspoti kambini kwamba inairipoti vibaya Yanga. 

Ingawa habari za awali zinasema ilikuwa hakuna jinsi zaidi ya kuifukuza Mwanaspoti kambini kulinda masilahi ya wakubwa akiwemo Nyanje ambao walipendekeza Yanga ipige kambi Uturuki. Ingebaki ingetibua ukweli wa mambo mengi yaliyokuwa yamejificha. 

Narudia tena sikuwahi kukutana na vitimbi nilivyokutana navyo kwenye kambi ya Yanga katika safari zote nilizowahi kusafiri na klabu za Tanzania pamoja na timu za Taifa nje ya nchi kwa miaka kumi mfululizo. 

Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingilia uhuru wa chombo cha habari ndio maana kwa kutaka kuwa huru zaidi Kampuni ya Mwananchi imekuwa ikigharamia kila kitu cha waandishi wake wanaokwenda popote Duniani na ndicho kilichonifanya kuishi kwa amani baada ya udhalilishaji wa Nyanje. Nyanje ana roho ambayo nashindwa kuielekezea. 

Yanga inasafiri kwa basi kubwa tu na ambalo lilikuwa halijaa kwenda kucheza mechi kilomita 60 mpaka 300 nje ya mji kabisa lakini anazuia hata mwandishi kuambatana kwenye basi moja inabidi kuchukua Taxi kwa gharama kufuata msafara nyuma mpaka utakapofika ndio uanze kupatana na dereva ambayo kwa maisha ya Ulaya ilikuwa ikigharimu fedha nyingi kwa kuwa madereva walikuwa wanataja fedha nyingi wakitumia mwanya wa mimi kutofahamu mazingira. 

Hakukuwa na athari yoyote ya mwandishi kupanda basi la Yanga kwenda umbali wa kama Dar es Salaam na Mikumi Morogoro tena kushuhudia mechi ya kirafiki ujue Nyanje ana roho ya aina gani na anatoa picha gani kwa Yanga mbele ya jamii. Lakini Watanzania walipata matokeo bila matatizo kupitia Mwanaspoti yao. 

Pengine ningekuwa nimesafirishwa kwa gharama za Yanga ningefia Uturuki kutokana na Nyanje alivyoonyesha kutokuwa na thamani utu na uzalendo pengine angenitelekeza kabisa mitaani na mwili wangu usionekane kabisa hasa ukizingatia Tanzania haina hata ubalozi Antalya. Mungu saidia nimetua salama Dar es Salaam jana alfajiri ila sijawahi kuona upuuzi kama huu wa Nyanje alionifanyia Uturuki. 

Hata Waisraeli na Wapalestina wanachukiana lakini si kwa kiwango hicho. Nyanje jifunze utu umaarufu hauji kwa kugombana na Michael Momburi shawishi Wanayanga kwa njia nyingine.
Chanzo: gazeti mwanaspoti

Unawafahamu waafrika waliodhulumiwa kwa kuipenda Afrika yao?


 
Patrice Lumumba akiwa amshikiliwa na waafrika wenzie baada ya Marekani na Ubelgiji kumtuhumu kuvuruga amani nchini Zaire. inasadikiwa mwili wake ulitumbukizw kenye pipa la asidi mpaka sasa kaburi lake halijaonekana.


Lumumba wakati wa harakati zake alipokuwa waziri mkuu nchini Zaire sasa inajulikana Congo DRC.

Patrice Emery Lumumba (2 Julai, 1925 – 17 Januari, 1961), alikuwa mpigania Uhuru wa Taifa la Zaire (Sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) na Waziri Mkuu wa Kwanza halali aliyechaguliwa na Wananchi wa Taifa hilo. Aliuawa kwa Ushirikiano Mkubwa wa Mataifa ya Ubelgiji, Marekani na Vibaraka wao waliokuwapo huko Zaire Wiki kumi tu mara baada ya Uhuru wa Nchi yake, Januari 17, 1961, miaka 51 na siku 3 iliyopita.

Lumumba alikuwa Mwanaharakati wa kweli aliyeondoshwa katika uso wa dunia hii kwa hila wakati akipambana kuupinga utumwa wa kifikra na kiutendaji, ni mfano wa kuigwa kwa vijana wa leo walioamua kuyageuza maisha yao kama "Mipira ya Kiume" Kutumika na kisha kutupwa kando madhalili. Vijana wa leo ambao wameamua kuyakabidhi maisha yao kwa wapenda mamlaka huku wakikisaliti kizazi chao cha kishenzi.

Wakati huu tukidurusu Maisha ya Simba huyu wa Afrika ya zamani, ni muhimu sana kutambua kuwa Afrika ya sasa ni dhalili zaidi ya kipindi cha ukoloni mkongwe, Afrika ya sasa haina tumaini kwani vijana na watoto kama vizazi vya leo na kesho kwa dhahiri hawajitambui, hawana walijualo, ujinga wanaita maarifa, wanajiita "wasomi" ambao hawana uhusiano na wala hawana majibu ya matatizo ya jamii zao, wamekuwa makasuku wakutumainiwa na mabwana zao (ubeberu), Afrika inayokwenda mrama ambayo tumaini la kurejea kwenye hadhi na Utu wake Limepotea.

Aliyofanyiwa Patrice Lumumba unaweza ukadhani ni yeye peke yake, Utakuwa unajidanganya ndani ya nafsi yako. Joseph Mobutu hakuwa peke yake barani Afrika, walikuwepo wengi na bado wanagalipo na wengine zaidi wanazidi kujitokeza, thamani ya damu ya wanaadamu haitambuliki kabisa ndani ya bara la Afrika.

Wale waliodharau athari za mwanzo za akina Mobutu na wenzake, na wao yaliwafika yaliyowafika kutokana na kudharau dhambi zilizofanywa na dhalimu Mobutu kwa kugeuzwa kibaraka walio mtuilia. Leo Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imerithishwa maradhi yale yale ya kutokujali uhai wa mwanadamu.

Maradhi kama hayo, tukambukizwa na sisi Tanzania kwa mambo mengine makubwa na madogo na mengine mithili ya hayo yaliyo fanywa huko Congo. Wengine wakajifanya vipofu ati hawayaoni, yakiwemo ya mauwaji ya wanasiasa, uwekwajwi ndani bila makosa, wizi na Ufisadi wa Mali za Umma, Ubinafsi, Udini na Ukabili, Ukibaraka na kushadadia Ukoloni Mamboleo.

KINA LUMUMBA WETU: HUZUNI NA MAJONZI YA KUWAPOTEZA HANGA, SHARIFF, SADALLAH NA ABDULAZIZ K. TWALA.

"Karume hakuwapenda Wasomi, na hakuwa akiwaamini kabisa, hata ukiangalia wengi wa Viongozi wa ASP waliofungwa na Karume walikuwa ni wale Wasomi, Kama Othman Shariff.

Othman Shariff na Karume walikuwa ni Mahasimu ndani ya siasa za ndani za ASP hata kabla ya Uhuru wa Zanzibar, baada ya Mapinduzi Shariff aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu kisha mara tu baada ya Muungano na Tanganyika akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Marekani.

Inasemwa kuwa wakati flani Shariff aliporudi nyumbani Tanzania kwa mapumziko aliwahi kuonekana akipiga picha katika maeneo ya Ikulu, hilo tu la kuonekana akipiga picha Ikulu lilitosha kulifanya 'Baraza la Mapinduzi' kumtuhumu Balozi Shariff kuwa ni 'shushushu' wa CIA aliyekuwa akipeleleza kwa ajili ya Manufaa ya Serikali ya Marekani.

Mamlaka za Usalama zilimkamata kwa tuhuma za 'Ushushushu na Ukibaraka' lakini zilimuachia mara baada ya Rais Nyerere kuingilia hilo. Alishushwa Madaraka yake kutoka Balozi mpaka kuwa Afisa wa Mifugo katika Mkoa wa Iringa, Tanzania Bara.

Baadaye Usalama wa Taifa wa Zanzibar kwa amri Maalum ya Baraza la Mapinduzi ulitumwa kwenda kumkamata Balozi Othman Shariff Mussa huko Iringa na kumrejesha Zanzibar, Mwalimu Nyerere alijaribu tena kuingilia kwenye hilo baada ya kuombwa kufanya hivyo na Wazee wa Iringa.

Baadaye Nyerere alikubali kumkabidhi Shariff kwa Mamlaka za Usalama wa Taifa wa Zanzibar baada ya kushawishiwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, mara baada ya kufikishwa Zanzibar huo ndio ulikuwa mwisho wa Shariff.

Abdallah Kassim Hanga alikuwa Msomi kutoka Urusi na mtu Mashuhuri sana Miongoni mwa Wanachama Vijana wa Chama cha Afro-Shiraz (ASP). Mara baada ya Mapinduzi alitangazwa kuwa Makamo wa Rais wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar chini ya Karume kabla ya kuhamishiwa Jijini Dar es salaam kwenye Serikali ya Muungano mara baada ya Muungano. 

Punde tu Hanga alimtumbukia nyongo Nyerere kwa sababu ya Ukaribu wake na Kambona, aliyekuwa Waziri wa Nyerere wa Mambo ya Nje na Ulinzi. Wakati wa Uasi wa Jeshi la Tanganyika (King's African Riffles) mwaka 1964, alikuwa ni Kambona aliyekwenda kuzungumza na Wanajeshi wale akijaribu kuwatuliza wakati Nyerere akiwa Mafichoni.

Mara baada ya Kambona kukosana na Nyerere na kwenda Uhamishoni, Hanga naye alitazamwa kwa Jicho baya kwa kuwa alikuwa karibu mno na Kambona. Punde aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri na akaamua kuhamia Conakry, Nchini Guinea kwa kuwa alikuwa ameoa Mwanamke wa Kiguinea.

Baada ya muda, Rais Nyerere alipeleka Ujumbe kwa Rais Ahmed Sekou Toure wa Guinea, ambaye ndiye aliyekuwa amempa hifadhi Hanga Nchini mwake, akimuomba akubali kumrudisha Hanga Nchini Tanzania na akimuahidi kuwa Hanga asingedhuriwa na angebaki salama.

Kwa bahati mbaya, Mara baada ya Hanga kurejea Tanzania alikamatwa na akadhalilishwa hadharani wananchi wote wakishuhudia. Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Nyerere alimleta Hanga Uwanjani hapo akiwa na Pingu mikononi.

Katika Hotuba yake aliyoitoa viwanjani hapo, Rais Nyerere alimdhalilisha na kumsema vibaya Hanga na kama haitoshi akakubali kumrudisha Zanzibar ambako aliteswa na kisha kuuawa kinyume kabisa na ahadi aliyoitoa kwa Rais Sekou Toure".

TUJIFUNZE KWA MAKOSA: FURAHA YA KUOKOLEWA KWA ALI SULTAN ISSA, PROFESA ABDULRAHMAN MOHAMMED BABU NA BAKAA YA MAKOMREDI WENGINE.

"Kesi ya kwanza ilikuwa ni kama Kuondoa Wapinzani, Ilionekana ni Kesi ya Kisiasa tu. Mamlaka za Utawala ziltaka tu kutuangamiza na kutupoteza Vigogo wote wa kilichokuwa Chama cha Siasa cha Umma Party.

Lakini Utawala wa Zanzibar ulikuwa na kikwazo kimoja katika nia na lengo lao hilo la kutuangamiza, Jijini Dar es salaam Nyerere alikuwa ameshamkamata Profesa Abdulrahman Mohammed Babu na akiwa amekataa 'kata kata' kuwarejesha Zanzibar akikhofia kuwa wangeangamizwa tu.

Wakati tulipogundua tukiwa Gerezani kuwa Babu naye alikuwa Gerezani huko Bara na kuwa tungefikishwa Mahakamani na sio kudhalilishwa tu hadharani na kuuawa kama walivyofanyiwa kina Hanga, tuliamini kwa dhati katika Nyoyo zetu kuwa hatutauliwa.

Aboud Jumbe, Mtu Msomi na Muelewa ndiye aliyekuwa Madarakani wakati huo, tofauti na Karume au Seif Bakari, na Babu akiwa hai. Kwa hili 'NAMSHKURU SANA' Nyerere.

Labda alijifunza kutokana na funzo la yaliyojitokeza alipoamua kuwakabidhi Hanga na Shariff kwa Serikali ya Zanzibar. kwa kukataa kwake kumkabidhi Babu na wafungwa wenzie waliokamatwa huko Bara kwa Baraza la Mapinduzi, Nyerere alituokoa sote tusiuawe. Kama angewakabidhi kina Babu, sote tungeangamizwa, sote tungeteketea.

Lakini Jumbe na Serikali yake walikaa chini na kufikiri kuwa 'Tunawezaje kuwaangamiza wote, ikiwa Kiongozi wa Mkasa huu yu salama huko Tanzania Bara'."

"HAKUNA ALIYE MBORA KWA WATU WOTE, NA WALA HAKUNA ALIYE MBAYA KWA WATU WOTE", FUNZO LA FUNGATE YA UHURU.

Maandishi haya (KINA LUMUMBA WETU na TUJIFUNZE KWA MAKOSA) ni sehemu tu ya Masimulizi ya Komredi Ali Sultan Issa wa Chama cha Umma Party, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Karume, Katika Ukurasa wa 206 wa Kitabu cha Mwandishi G. Thomas Burgess, kiitwacho "Race, Revolution and The Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad".

Kwa dhahiri maandishi yanaainisha mikasa, visa na masimango yafananayo na yaliyomkuta Komredi Patrice Lumumba yaliyowapata watu mbalimbali Nchini petu tofauti ikiwa kwa hapa yote hayo yalitendwa na Serikali yetu ya Kizalendo tofauti na aliyofanyiwa Lumumba ambayo yalikuwa na Nguvu na mkono mzito wa Mataifa ya Nje.

Maandishi haya ni funzo zito kwa Viongozi wetu walioamua kulala Usingizi Mzito wa Pono katika zama zao hizi za Fungate ya Uhuru wetu, wakiyatumia vibaya mamlaka na madaraka yao dhidi yetu, wakifanya ghiliba na hujuma za dhahiri juu ya rasilimali zetu na wakitumia kila nyenzo na silaha waliyonayo kwa kila aliyepaza sauti dhidi yao au kuwa tishio la Nafasi zao za kiutawala.

Maandishi haya ni wokovu na fursa ya mafunzo kwetu na kwa viongozi wetu kujifunza kutoka katika makosa ya mababa na mababu zetu kwa kuiga tu yale yaliyo mema na yenye tija kwa mustakabali wetu na kuacha yale Maovu yaliyofanywa na watangulizi wetu.

Ni maandishi yanayoonyesha Machungu, furaha, huzuni na shukrani, yakiainisha mikingamo, migongano, misuguano na makubaliano kati yetu na yakitupa wasaa wa kudurusu na kujenga namna bora ya miingiliano yetu. Zaidi ni maandishi yanayotuonyesha namna Wazee wetu walivyofanya Makosa na pia kujisahihisha, Kwa hakika ni funzo zito kwetu.

"KILA KIZAZI, KUTOKANA NA UTATA WA WAKATI WAKE, KINA WAJIBU. KIUTEKELEZE AMA KIUKATAE", FRANTZ FANON.

Hakuna jamii yoyote duniani ambayo ilishawahi kuendelea bila Uzalendo na Mapenzi ya dhati kwa Jamii (Watu) na Ardhi (Nchi) yao. Muhimu zaidi kutambua ni kuwa Uzalendo sio zao la Kinasaba bali ni zao la Utamaduni, Ustaarabu na Historia inayoishi na kufanya kazi. 

Kimsingi UZALENDO mtu hufunzwa, kizazi kilichopigania "Uhuru wa Bendera" wa bara hili kilirithi, kupata na kufungamana na Somo la Uzalendo kupitia madhila yaliombatana na Ukoloni Mkongwe, Mimi nauita Uzalendo wa Asili au utokanao na Mazingira.

Sisi kizazi cha sasa, ikiwa ni miongo kadhaa baada ya "Uhuru" hatukuweza kuwa na Fursa hizo za kupata nafasi ya kuwa na "Uzalendo wa Asili", na bahati mbaya ni kuwa hatuna pa kuupata na kujifunza uzalendo huo kwa kuwa tumeamua kuutupa Utamaduni, Ustaarabu pamoja na Historia inayoishi.

Muhimu kutambua ni kuwa Wajibu wa Kutekelezwa na Kizazi chetu hautuepuki kwa kuwa tu tumeamua kujikana, Kuepuka Maangamizi ni kuutekeleza wajibu wetu. Mpaka pale tutakapo rejea katika misingi ya uasili wetu, tukawa na "Cha kwetu" cha kuweza kukilinda na kukifia, kila nyanja ya maisha ikawa inasadifu Uafrika, hapo ndipo Uzalendo utakapomea na mapenzi ya Jamii na Ardhi yetu yatakapodhihiri kvitendo na hatimaye uhuru wa kweli kupatikana.

Mungu Ibariki Afrika Moja, Mlaze Pema Baba Lumumba na Mashujaa wetu wengine.

Makala haya kutoka ukurasa wa facebook : Watanzania mashuhuri