Tuesday, July 30, 2013

Anyimwa Viza ya New Zealand kwasababu ya ubonge.


Maafisa wa utawala nchini New Zealand , wamemwambia mwanamume mmoja raia wa Afrika Kusini ambaye pia ni mpishi kuwa ni mnene kupita kiasi kuweza kuruhusiwa kuishi nchini humo.
Maafisa wa uhamiaji walisema kuwa Albert Buitenhuis, mwenye uzani wa kilo 130 hana afya nzuri.
Sasa anakabiliwa na tisho la kufukuzwa kutoka nchini humo licha ya kupunguza uzani wake kwa kilo 30 tangu kuhamia mjini Christchurch miaka sita iliyopita.
New Zealand ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wenye unene kupita kiasi huku takriban asilimia 30 ya watu wake wakiwa waathiriwa.
Bwana Buitenhuis na mkewe walihamia nchini New Zealand, mwaka 2007. Wakati huo mwanamume huyo alikuwa na uzani wa kilo 160.
Hadi sasa wamekuwa wakipokea Viza zao zinazowaruhusu kufanya kazi nchini humo bila matatizo mengi kulingana na mkewe.
''Tumekuwa tukiomba viza hizo kila mwaka na hapajawahi kuwa na matatizo yoyote, '' alisema mkewe Albert
"hawajawahi kuzungumzia uzito wa Albert wala afya yake wakati hata alipokuwa mnene kushinda sasa.''
Lakini mapema mwezi Mei, wanandoa hao waliambiwa kuwa hawatapokea visa mpya kwa sababu ya unene wa bwana Buitenhuis.
"nimeshangazwa sana kwa sababu kwa sasa ameweza kupoteza kilo 30 tangu tuje hapa New Zealand, '' alisema mkewe Buitenhuis.
Wawili hao wamemuomba waziri wa uhamiaji wa nchi hiyo kuwaruhusu waendelee kuishi nchini humo kwani bwana Buitenhuis ameweza kupoteza kilo.
Msemaji wa uhamiaji alisema kuwa bwana Buitenhuis alinyimwa visa mpya kwa sababu ya tisho kwa afya yake kutokana na uzani wake, kuwa anaweza kupatwa na kisiukari, shinikizo la damu na maradhi ya moyo.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment