Monday, December 31, 2012

Tofauti Kati Ya Mifumo Ya Analojia Na Dijitali Ya Kurusha Matangazo Ya Televisheni.

Zamil Huyu akitafakari mabadiliko ya mfumo kutoka analojia kwenda dijitali leo usiku..


Na Zamil Khalfan

Leo (tarehe 31/12/2012) ikiwa siku ya mwisho kwa nchi yetu (Tanzania) kurusha matangazo kwa njia ya analojia (analogue TV) , na kuhamia mfumo wa dijitali (digital TV), bado watu wana maswali mengi sana kuhusiana na mabadiliko haya. 

Huu mfumo mpya wa dijitali ni nini? Mfumo uliopita wa analojia ukoje? Nini tofauti kati ya mifumo hii miwili ya kurusha matangazo ya televisheni? Kwa nini tumeamua kuhamia mfumo huu mpya wa dijitali na kuacha ule wa zamani wa analojia? Makala hii itajaribu kujibu maswali hayo kwa njia rahisi yenye kueleweka, kwa hiyo endelea kusoma.

Tanzania sio nchi ya kwanza kuhamia katika mfumo wa dijitali wa kurusha matangazo ya TV. Nchi ya Uholanzi ilizima mitambo yake ya analojia mwaka 2006, na nchi kama Ujerumani, Norway, Ubelgiji, Estonia, Latvia, Hispania, Marekani na nyinginezo zilifanya mabadiliko katika kipindi cha mwaka 2009/10. Hatimaye, hatua kwa hatua nchi zote duniani zitahamia katika mfumo huu mpya, na inategemewa kwamba zote zitakuwa zimefanya hivyo kufikia mwaka 2015.


Lakini kabla ya kuuangalia huu mfumo mpya wa dijitali unavyofanya kazi na faida zake, acheni tuuangalie kwanza mfumo unaomalizika wa analojia. Tofauti kati ya mifumo hii miwili inategemea jinsi mawimbi ya matangazo ya televisheni yanavyosafirishwa kutoka kwenye vituo vya kurushia matangazo mpaka kwenye televisheni yako.

Mfumo wa analojia wa kurusha matangazo ya televisheni hauna tofauti na jinsi matangazo ya redio yanavyorushwa. Vyote vinatumia masafa ya AM na FM. Kwenye matangazo ya analojia ya televisheni, picha na video vinarushwa kupitia masafa ya AM na sauti inarushwa kupitia masafa ya FM. Njia hii ya kurusha matangazo ina kasoro nyingi kwani kiwango cha picha na sauti kinakuwa cha chini sana. Pia, mwingiliano wa mawimbi unaweza kusababisha picha au sauti kuwa na chengachenga au kutosikika vizuri hasa siku za mvamvua, au kama unaishi mbali na kituo cha kurushia matangazo. 

Pia mfumo wa NTSC wa kurusha matangazo kwa njia ya analojia haukutengenezwa kwa ajili ya kuonyesha picha za rangi. Mfumo huo ulitengenezwa baada ya vita vya pili vya dunia, wakati ambapo televisheni zilikuwa hazionyeshi picha za rangi (black and white), hivyo mpaka leo mara nyingine televisheni za analojia zinakuwa na rangi ambazo si halisi, mara nyingine hata tofauti kabisa na ile iliyorushwa na kituo cha matangazo. (kwa mfano shati ya bluu inaweza kuonekana ya njano n.k.)

Kwa upande mwingine, mfumo wa dijitali unasafirisha matangazo katika njia inayofanana na jinsi kompyuta inavyosafirisha habari. Kwa maana hiyo, TV za dijitali hazina chenga kwa sababu chenga hutokana na mwingiliano wa mawimbi ya redio. Kama upo mbali na kituo cha kurushia matangazo, picha haitaonekana kabisa.

Mfumo huu wa dijitali umetengenezwa kusafirisha picha, video, sauti na habari nyingine kwa kiwango cha juu kabisa. Pia inawezesha vituo vya televisheni kuboresha matangazo yake kwa kutia ndani sauti katika lugha zaidi ya moja, maandishi n.k katika matangazo yake. Faida nyingine kubwa ya dijitali ni uwezo wa kurusha matangazo ya HDTV (High Definition Television). HDTV ni mfumo unaoonyesha video kwa kiwango bora kabisa. 

Kwa kuwa televisheni nyingi nchini zinatumia mfumo wa analojia, kifaa kinachoitwa king’amuzi (digital to analogue decoder) kinahitajiwa ili kubadili mawimbi ya dijitali kwenda katika mfumo wa analojia ambao televisheni nyingi zinaweza kuonyesha. Pia kwa wale wanaotumia simu za mkononi zenye antenna hawataweza kupokea matangazo hayo tena, labda wawe wanatumia simu mpya zinazoweza kupokea matangazo ya dijitali, au zinazopokea matangazo kupitia intaneti. (Internet Television).

Chanzo: zamil ‘ibn kathiir’ khalfan facebook wall…

Soma namna mhasibu wa Simba SC Erick Sekete alivyoporwa mapato ya Simba Vs Tusker ya Kenya...


MHASIBU wa Klabu ya Simba, Erick Sekete Jumamosi wiki hii ameavamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa zaidi ya Sh7 milioni.
Fedha hizo zilikuwa ni za mgao wa klabu hiyo ilizopata katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Sinza.
“Ni kweli, tukio hilo limetokea mhasibu wetu, Erick alivamiwa na watu waosiojulikana wakati akitoka Uwanja wa Taifa kwenye mechi yetu ya kirafiki dhidi ya Tusker Kenya.
“Ameporwa kiasi cha Sh7 milioni, mgao wa mechi ya kirafiki dhidi ya Tusker,” alisema Kamwaga.
“Wakati Erick akikumbwa na tukio hilo alikuwa pamoja na Stanley Philipo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yupo hapa Simba kwa ajili ya masomo kwa vitendo ya mawasiliono ya umma,” alisema.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kituo cha Polisi Magomeni ambapo sasa suala hilo linashughulikiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Polisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na watalitolea ufafanuzi baadaye.
“Tumepokea taarifa ya tukio hilo, tutalitolea ufafanuzi baadaye,” alisema Kinyela.
Wakati huohuo, aliyekuwa kocha wa Simba, Milovan Cirkovic amesema bado anaikumbuka klabu ya Simba na anaamini siku moja atarejea kuifundisha.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya mtandao wa Facebook, Cirkovic alisema yuko tayari kurudi kuinoa Simba wakati wowote endapo uongozi wa klabu hiyo utamhitaji.
“Simba ipo kwenye moyo wangu na ndiyo maana kila wakati naikumbuka, malengo yangu yalikuwa kuiacha ikiwa na rekodi mpya katika michuano ya kimataifa nasikitika sijafanikiwa.
“Mwaka jana tulikuwa na uwezo wa kufika mbali zaidi katika michuano ya Kombe la Shirikisho tukafanya uzembe tukaondolewa.
“Nilikuwa na ndoto ya kufanya vizuri katika michuano ijayo lakini yamekuja mambo haya kwa kweli nimesikitika sana,” alisema Cirkovic. “Unajua ili uweze kufanikiwa katika taaluma ya ukocha lazima uwe na maelewano mazuri na wachezaji wako jambo ambalo mimi nililifurahia Simba. Wachezaji walinipenda na mimi niliwapenda.”
“Siwezi kuichukia Simba kwa sababu mkataba wangu umesitishwa, ninasikitika kuondoka mapema na ndiyo maana, leo ama kesho nipo tayari kurudi kama watanihitaji,” alisema Cirkovic.
Cirkovic anayeishi katika Mji wa Cacak nchini Serbia pia aliushauri uongozi wa Simba kuendelea kuipa kipaumbele timu yao ya soka ya vijana akisema ndiyo dira ya mafanikio kama wanahitaji mafanikio ya kweli.
“Shomari Kapombe, Christopher Edward na Jonas Mkude ni matunda ya utaratibu mzuri wa kulea vijana, ushauri wangu waendelee kuitunza na mafanikio watayaona,” alisema Cirkovic.
 Chanzo: mwananchi.com

Kesi ya Sheikh Ponda yaahirihwa kwa kukosa mashahidi mahakamani leo.

 Katibu Mkuu  wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo pamoja na washtakiwa wenzake 49, hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa kutokana na mashahidi upande wa mashtaka ambao ni serikali kutofika mahakamani hapo.
 
 Wafuasi wa Sheikh Ponda wakiwa nje ya mahakama kuhakikisha sheikh wao anapata haki.

Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa na mshtakiwa mwenzake,  Mukadam Abdal Swalehe (kushoto).

Kulikuwa na ulinzi si wa kawaida leo katika mahakama ya Kisutu..

Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog.

Serikali yajipanga kukabiliana na ongezeko la watu, na kuwajali wazee na wasiojiweza.


Rais jakaya Kikwete, amewataka watanzania kufanya kazi kwa nguvu ili kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanaenda sawa na ongezeko la watu nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa matokeo ya sensa ya idadi ya watu na makazi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Kikwete amesema idadi ya watu Tanzania inaongezeka kwa asilimia 2.9 kutoka mwaka 2002 ilipofanyika sensa ya mwisho na kutoa matokeo ya watu milioni 34.4 ambapo alitabiri itakapofika mwaka 2016 idadi ya watu nchini itafikia milioni 51.

Aidha matokeo ya sensa kwa mwaka huu wa 2012 yanaonyesha Tanzania ina jumla ya watu Milioni 44,929,002 ambapo Tanzania Bara ni Milioni 43,625,434 na Tanzania Visiwani ni Milioni 1,303,568.

“Idadi hii inaonyesha dalili mbaya ambapo nchi itakuwa na mzigo mkubwa katika masuala ya kijamii na kiuchumi, idadi kubwa ya watu inamaanisha Serikali iongeze mikakati ya kimaendeleo ili kukabiliana na ongezeko hili la watu,” alisema Kikwete na kuongeza;

“Umuhimu wa kupanga uzazi uanze sasa, maana ushindani wa rasilimali chache tulizonazo utakuwa mkubwa sana miaka ya usoni, hivyo ni vema wananchi wakajulishwa umuhimu wa kupanga uzazi.”

Tangu Tanzania iundwe mwaka 1964 baada ya kuunganishwa Tanganyika na Zanzibar, hii ni sensa ya tano kufanyika ambapo sensa ya kwanza ya mwaka 1967 idadi ya watanzania ilikuwa ni milioni 12,313,54 (milioni 12.3). Tanzania bara ilikuwa na watu milioni 11,958,654 (milioni 11.9) na Tanzania visiwani kulikuwa na watu laki 3,544,00 (laki 3.5).

Hata hivyo sensa ya mwaka 2002 ilionyesha ongezeko kubwa la watu waliofikia milioni 43.625,434 (milioni 43.6) Zanzibar peke yake ilikuwa na wakaazi milioni 1.335,68 (milioni 1.3).

Katika hatua nyingine Rais Kikwete amesema haya ni matokeo ya awali ambayo yameonyesha idadi ya watu kwa ujumla. Lakini ikifika mwezi februari 2013 yatatolewa matokeo mengine yatakayoonyesha idadi ya watu kwa jinsia yaani wanawake wapo wangapi na wanaume wapo wangapi.

Mwezi Aprili 2013 yatatolewa matokeo mengine yatakayoonyesha idadi ya watu kwa umri kuanzia kata, wilaya na mikoa. Na ikifika mwezi June 2013 zitatolewa takwimu nyingine zitakazoonyesha watu wenye ajira, idadi ya kaya na masuala mingine ya kitakwimu.

Awali waziri mkuu Mizengo Pinda ambae ndie mwenyekiti wa kamati kuu ya sensa taifa amesema Serikali kwa mwaka huu imeendesha sensa kwa asilimia tisini (90%) na asilimia 10 (10%) ni wahisani, tofauti na mwaka 2002 ambapo serikali iligharamia zoezi la sensa kwa asilimia 70 (70%).

Aidha Pinda aliongeza kuwa kwa mwaka huu wataalamu wa ndani katika zoezi zima walitumika sana tofauti na mwaka 2002, ambapo kwa mwaka huu wataalamu wa kutenga maeneo ya sensa walikuwa 150, makarani 20,000 na wataalamu wengine wa takwimu 400 wote watanzania.

Pesa zilizotumika kuwalipa posho za kuendesha sensa ni milioni 90, ambapo waliweza kutoa zabuni 29 za kuendesha zoezi zima kwa kampuni za kizalendo zipatazo 29 na kuwalipa kiasi cha bilioni 11.7.

Mpaka matokeo ya awali ya sensa yanatangazwa leo serikali imetumia kiasi cha Sh bilioni 120 na kwa mujibu wa rais Kikwete ifikapo mwezi June 2013 yatakapotangazwa matokeo ya mwisho serikali itakuwa imetumia kiasi cha Sh bilioni 140 kwa zoezi zima.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
kidojembe@gmail.com
+255 752 593894/ +255 713 593894



naibu waziri sayansi na technolojia Januari makamba atoa ratiba ya kuzimwa mitambo ya analojia....


Ndugu Wananchi,
 Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.

Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

    (1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
    (2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
    (3) Mwanza-28 Februari, 2013;
    (4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;
    (5) Mbeya-30 Aprili, 2013.
 Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.
  
Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,
Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi
Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz
  
Ndugu Wananchi,
Nawashukuru kwa kunisikiliza.


Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan akiongoza mazoezi kwa vilabu vya jogging jijini Dar es Salaam kuukaribisha mwaka mpya...

 Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiongoza mazoezi kwa vijana wa Klabu 12 za jogging kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam  wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nane kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani.




Idd Azzan akivuta kamba.



Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za 12 tofauti za Jogging 12 jijini Dar es Salaam wakifanya mazoezi ya kukimbia jijini Dar es Salaam Kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 lililoandaliwa na Klabu ya Jogging Kawe jijini.

picha kwa hisani ya saidpowa bolg

Sunday, December 30, 2012

Machimbo ya chumvi haya mjini Bagamoyo.... siku hizi watu wengi hawatumii chumvi hizi....


TCRA kuanza kuzima mitambo ya Dar es Salaam kwanza.... Analogia kuenda Dijitali


WAKATI zimebakia saa 24 Tanzania kuungana na nchi nyingine duniani kuanza kurusha matangazo ya televisheni kwa mfumo wa Dijitali zikiachana na ule wa Analojia, imebainika kuwa mpango huo utaanzia Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Habari za ndani kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), zilizolifikia Mwananchi Jumapili, zinaeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam pekee, ndiyo litakuwa la kwanza kuingia kwenye mfumo huo kuanzia Januari mosi, 2013 na siyo mikoa mingine nchini.
TCRA, imeshatangaza kuwa itaufunga mfumo wa analojia ifikapo Desemba 31 mwaka huu yaani kesho.
Habari hizo zimeeleza kuwa mamlaka hiyo imeamua kuchukua hatua za tahadhari katika utekelezaji wa mpango huo muhimu, kwa kuanza na mji mmoja baada ya mwingine, ambapo  mwezi mmoja baada ya Dar es Salaam kuanza kutumia mfumo wa dijitali, utafuatia Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alipoulizwa aliliambia gazeti hili jana kwamba mamlaka yake itatoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.
“Hatuwezi kukurupuka katika suala hili, tuko makini, lakini kesho (leo), tutakuwa na mkutano wa wanahabari kwa ajili ya kueleza mikakati mbalimbali na jinsi tulivyojipanga katika jambo hili,” alisema Profesa Nkoma.
Tayari TCRA imetaja miji mingine mbali ya Dar es Salaam ambayo imeshaunganishwa katika mfumo wa dijitali kuwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Tanga, Mbeya, Moshi na kwa sasa mji wa Morogoro unajengewa miundombinu husika.
Habari zaidi zilieleza kuwa kwa utaratibu uliopo sasa itachukua miezi kadhaa kabla ya kuzimwa kwa mfumo wa analojia katika miji minane ya awali, ambapo pia itachukua muda mrefu zaidi kuzimwa mfumo huo nchi nzima.
Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU), limezitaka nchi zote duniani kuhamia kwenye mfumo huo wa kurusha matangazo ya televisheni wa dijitali kutoka mfumo wa analojia ifikapo Julai 2015.
Ikiwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Tanzania imeanza kutekeleza azimio la nchi hizo ilizozitaka kufanya hivyo mwaka huu wa 2012, badala ya kusubiri hadi tarehe ya mwisho iliyowekwa na ITU.  
Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele kuhamia kwenye mfumo huo wa dijitali, ingawa kwa mtindo wa awamu, nchi nyingine wanachama wa EAC hasa Kenya na Uganda bado hazijaingia katika mfumo huo.
TCRA imezikabidhi kampuni tatu kufanya kazi ya usambazaji wa mfumo huo wa dijitali, ambazo ni Basic Transmissions  inayoundwa na Kampuni za IPP Media na Sahara
Communications, Kampuni ya Ting ya Agape Associates na Star Media Tanzania Limited (Startimes) ambayo ina ubia na  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Communications and Technology ya China.
TCRA imekuwa ikielezea kuwa Tanzania ipo tayari kujiunga na mfumo huo kwa kuwa asilimia kati ya 22 kati ya 24 ya nchi ambayo inatumia analojia, tayari imefikiwa na mtandao wa mfumo wa dijitali, ikijumuisha miji minane ambayo kwa kiasi kikubwa kampuni ya Startimes imeifikia.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameshindwa kuzielewa takwimu hizo kwa kuwa mitambo ya analojia ipo katika mikoa kadhaa nchini, ambayo bado haijapata mfumo wa dijitali. Mikoa hiyo ni pamoja na Lindi, Tabora, Bukoba, Musoma, Kigoma na Singida.
Kampuni ya Startimes ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi ambapo hadi sasa inakadiriwa kufikisha wateja 350,000,  Kampuni ya Ting ikiwa na wateja 10,000, huku Kampuni ya Basic Transmissions ikitangaza kuanza shughuli zake hivi karibuni.
Bei ya king’amuzi ni Sh39,000 ingawa mnunuzi anapaswa kulipia fedha za ziada kwa ajili ya kifurushi atakachochagua.
Hata hivyo, utata bado unagubika urushaji huo wa chaneli za bure ambazo ni ITV, Star TV, TBC1, Channel Ten na Eat Africa TV ikielezwa kuwa wamiliki wa vituo hivyo hawataki zionyeshwe bure kwenye kila king’amuzi bali ving’amuzi vyao pekee.
TCRA imeeleza kuwa kwa sasa imefanikiwa kupata ufumbuzi wa muda, ambapo chaneli zote zinaweza kuonekana bure kwenye kila king’amuzi.
Wananchi wachangamkia ving’amuzi
Katika hatua nyingine, gazeti hili lilifika katika ofisi za makao makuu ya Startimes jijini Dar es Salaam na kukuta mamia ya wananchi wakiwa katika foleni ya kununua ving’amuzi hivyo.
Baadhi ya wananchi hao walionyesha masikitiko yao baada ya kufutwa kwa malipo ya mwezi ya Sh9,000, badala yake kubaki malipo ya Sh23,000 na 36,000 kwa mwezi.“Kwa sasa wametoa ofa, ukinunua king’amuzi kwa Sh39,000 utalipia malipo ya mwezi ya kati ya Sh13,000 au Sh23,000, kile kifurushi cha bei nafuu wamekifuta na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa,” alisema Hadji Jumanne mkazi wa Kijitonyama.
Naye Happy Lazaro alisema Serikali inatakiwa kuongeza muda ili kuwapa fursa wananchi kununua ving’amuzi hivyo kwa kuwa hivi sasa imekuwa vurugu na huenda mitambo ya analojia ikazimwa huku wengi wakiwa hawajapata ving’amuzi hivyo.
Hata hivyo, watendaji wa kampuni hiyo waligoma kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazotolewa na wateja wao ikiwa ni pamoja na ubovu wa baadhi ya ving’amuzi, mabadiliko ya bei ya vufurushi kwa maelezo kuwa siyo wasemaji.
Chanzo: Mwananchi.com

Mwili wa mwanamke aliedhalilishwa na kufariki wawasili India...


NEW DELHI, India
MWILI wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi umerejeshwa nchini humo kwa ndege maalumu ya kukodi.
Balozi  wa  India  nchini  Singapore, T.C.A Raghavan  aliwaambia waandishi wa habari jana, saa  kadhaa baada  ya  mwanamke  huyo kufariki kutokana  na  viungo  vyake  kushindwa kufanya  kazi katika hospitali nchini Singapore  ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu walisafirishwa kwenda India katika ndege maalumu ya  kukodi  mchana wa  jana Jumamosi, kwa mujibu wa Raghavan.
Waziri  Mkuu wa India,  Manmohan Singh alisema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mwanamke  huyo  ambaye alifanyiwa  vitendo  vya  kinyama  kwa kubakwa  na kundi  la  vijana na kwamba  maandamano  yaliyozuka  kutokana na kitendo  hicho “yanaeleweka”.
“Nimesikitishwa  mno  kufahamu  kuwa mwathirika huyo wa mashambulizi ya kinyama yaliyofanyika  Desemba 16 mjini New Delhi ameshindwa kunusurika kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata baada ya shambulio dhidi yake, “ aliandika waziri  huyo mkuu katika tovuti yake.
“Tumeshaona hisia na nguvu ambazo tukio hili limesababisha. Hii ni hali ambayo inaeleweka kutoka  kwa vijana wa India  ambao wanataka mabadiliko ya kweli.
“Nataka  kuwaambia, familia yake na taifa  kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure.”
India imetikiswa na maandamano makubwa tangu msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 aliposhambuliwa kinyama  katika basi mjini New Delhi na kundi la watu sita.
Serikali imekuwa ikijaribu kulituliza wimbi  la hasira kwa  kuahidi adhabu kali kwa uhalifu mkubwa unaohusiana na  ngono pamoja na kuunda tume maalumu ya uchunguzi kuhusiana  na jinsi ya kushughulikia kesi za ubakaji.
Wakati maofisa wakijitayarisha kwa ghasia zaidi mitaani, polisi waliongezwa katika eneo la kati la mji mkuu wa India kabla ya mwili wa msichana huyo kurejeshwa  nchini  humo jana.
Ofisa wa polisi wa mjini New Delhi, alihimiza watu kuomboleza  kifo cha  mwanamke  huyo kwa  amani  wakati  maeneo  kadha  ya  mji  huo mkuu  yamefungwa.
Singh, ambaye  hapo  kabla  alitoa  wito wa  utulivu , alisema kuwa  itakuwa, “Heshima  kubwa  kwa  kumbukumbu  yake  iwapo tutaweza  kuelekeza  hisia zetu hizi  na  nguvu  katika  kuchukua hatua  sahihi. Kwa muda huu tunahitaji mjadala wa maana na uchunguzi kuhusiana na mabadiliko ya lazima  na haraka ambayo yanahitajika katika mtazamo wa jamii.
“Ni  matumaini  yangu  kuwa  tabaka  lote  la  kisiasa  pamoja  na jamii yote  itatenga maslahi yao  finyu ya binafsi na ajenda  ili kutusaidia  kufikia hatima  ambayo tunaikusudia, na kuifanya  India kuwa mahali bora na salama  kwa wanawake kuweza  kuishi.

Tanzania nchi inayoongoza kwa kuomba misaada....

Na Zitto Kabwe
Tanzania imekuwa moja ya nchi kipenzi kwa mataifa ya nje yaliyoendelea. Mapenzi haya yameonyeshwa kwa sura nyingi, ikiwamo kumiminiwa misaada ya kifedha na hata uwekezaji mkubwa kupitia kampuni za kutoka nchi hizo.
Takwimu za misaada ambayo Tanzania imekuwa ikipata zimekuwa za kukanganya na wakati mwingine zinazotiwa chumvi kulingana na malengo ya mtoa takwimu.
Kuna kijitabu kinachoeleza kuhusu misaada hii na mambo mengine, kinaitwa Pocket World in Figures huchapishwa na jarida la The Economist. Tangu mwaka 2006 nimekuwa msomaji asiyekosa kusoma kijitabu hiki.
Mwaka huu pia kijitabu hiki, 2012 Edition, kimetoa takwimu za ‘wapokea misaada’ na ‘watoa misaada’ duniani.
Tanzania nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya tatu Afrika na ya sita duniani kwa kupokea misaada.Mwaka 2010 Tanzania ilipokea misaada ya jumla ya dola za Marekani bilioni 2.9.
Misaada hii ilikuwa chini ya nchi kama Afghanistan (dola bilioni 6.3), Ethiopia (dola bilioni 3.5), CongoKinshasa (dola 3.4bn), Haiti (dola 3bn) na Pakistan (dola 3bn). Hivyo katika nchi za Afrika, Tanzania ni taifa la tatu kwa kupokea misaada mingi zaidi na ni la kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki.
Hata hivyo, inabidi kusoma takwimu hizi kwa mapana yake kidogo kwa kuangalia, kwa mfano, katika mwaka huo kila Mtanzania alipata msaada wa dola ngapi.
Kijitabu hicho kinatoa takwimu hizo pia na msaada kwa kila kichwa (aid per head) kwa kila Mtanzania ilikuwa ni dola 64.
Hapa Tanzania ilizidiwa na nchi kadhaa za Afrika ikiwamo Congo – Brazzavile (dola 325), Namibia (dola 113.5), Msumbiji (dola 84), Mauritius (dola 98), Botswana (dola 78) na Burundi (dola75).
Hata kwenye kipimo hiki bado Tanzania imeshika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki katika kupokea misaada kulingana na idadi ya watu kwa kuishinda Burundi tu.
Ufisadi na misaada
Ni vema kuongeza kuwa nchi za Afrika Mashariki zinazoongoza kwa misaada, Tanzania na Uganda, ndizo pia zinaoongoza kwa ufisadi. Kwa mujibu wa taasisi ya Transparency International,Uganda inaongoza kwa ufisadi ikifuatiwa kwa karibu na Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Je, kuna uhusiano wa kisayansi kati ya ufisadi na misaada kutoka nje?
Inawezekana inahitajika utafiti kuonyesha uhusiano huo. Nchi zenye kupokea misaada mingi hufanya serikali zao kuwajibika kwa watoa misaada zaidi kuliko wananchi wake na hivyo kupuuza vita dhidi ya ufisadi inayoendeshwa na raia wa nchi husika.
Laana ya rasilimali (resources curse)
Asilimia 45 ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi inatokana na madini, na hasa dhahabu. Tanzania ni nchi ya nne Afrika, baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali, kwa uzalishaji wa dhahabu, mwaka 2011 iliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.3.
Tangu uzalishaji mkubwa wa dhahabu uanze nchini mwaka 1998, Tanzania imekwishauza nje dhahabu ya thamani ya dola za Marekani bilioni 11.3.
Katika kipindi hicho mapato ya serikali kutokana na vyanzo vyote vya mapato kwenye sekta ya madini ni dola za Marekani milioni 455 tu.
Licha ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini na kukua kwa uchumi kwa kasi ya zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, bado umasikini wa Tanzania umeendelea kuwa mkubwa zaidi.
Utajiri wa madini na misaada kutoka nje vimeshindwa kupunguza umasikini na badala yake zaidi ya Watanzania milioni wameingia katika dimbwi la umasikini katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 na 2010.
Laana ya misaada?
Nchi ambayo takribani theluthi ya bajeti yake inategemea misaada kutoka nje lakini ikiwa na ufisadi na umasikini mkubwa inakuwa imeathirika kwa laana ya misaada (aid curse).
Ingawa watafiti wengi wameandika kuhusu ‘laana ya rasilimali’, kuna haja ya kufanya tafiti kuona kama kuna uhusiano kati ya wingi wa misaada kwa nchi na kushindwa kuendelea kwa nchi husika. Licha ya misaada ambayo Tanzania imekuwa ikipokea bado ni miongoni mwa nchi 18 duniani zenye pato dogo zaidi kwa mtu (GDP per head).
Hata hivyo kwa kipimo cha maendeleo ya watu (human development index), Tanzania imejichomoa kutoka kwenye nchi 25 masikini zaidi duniani. Asilimia 35 ya Watanzania wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa kwa mujibu wa taarifa za serikali (PHDR 2011).
Uzoefu wa Tanzania unaonyesha kuwa misaada mingi kutoka nje sio suluhisho la maendeleo ya watu.
Tanzania bilamisaada
Tanzania iache kupokea misaada ili kujikita kwenye kuongeza mapato ya ndani na kujitegemea? Tanzania bila misaada inawezekana? Jawabu ni uwajibikaji tu. Tukijenga misingi ya uwajibikaji na kuwajibishana tutaweza kuendesha nchi yetu bila kutegemea misaada, kwa kuondoa matumizi ya hovyo kama posho, magari na safari za nje, kukuza mapato ya ndani kwa kupanua wigo wa kodi na kukusanya zaidi kama tunavyostahili kutoka sekta ya madini na kasha mafuta na gesi asilia na kuwekeza vya kutosha kwenye kilimo na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
Nchi tajiri ziache kutoa misaada kwa Tanzania kuanzia bajeti ijayo ya mwaka 2013/14. Hatutakufa.Tutajitegemea!
Chanzo: Raia Mwema

Saturday, December 29, 2012

mh......


Jembe hili Francis Cheka kutoka Morogoro...



Bondia Francis Cheka ndie bingwa wa ndondi uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI SERIKALI YAZUIA KUINGIZWA MAFUTA YA DIESELI YALIYO CHINI YA KIWANGO NCHINI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI



Mwezi Novemba 2012, Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi
ilishinda zabuni ya sita ya kuingiza mafuta kwa pamoja chini ya utaratibu
unaosimamiwa na Kampuni ya uagizaji mafuta kwa Pamoja (PICL).
Zabuni hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya mafuta ya Mwezi Desemba 2012 na
mwanzoni wa Januari 2013.

Utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja huzingatia pamoja na
mambo mengine viwango vya ubora wa mafuta kama vinavyoelekezwa na
Shirika la Viwango nchini (TBS). Aidha, TBS hukagua ubora wa mafuta
hayo kabla hayajaingia nchini.

Pamoja na aina nyingine za mafuta, Addax Energy SA ilipaswa kuleta
mafuta ya dieseli yenye ujazo wa MT 100,000 sawa na takriban lita
100,000,000 katika zabuni ya sita. Meli ya AL BURAG iliyobeba mafuta
hayo ilitakiwa kufika hapa nchini na kupakua mafuta kati ya tarehe 17
mpaka 20 Desemba 2012. Hata hivyo, meli hiyo ilifika tarehe 24 Desemba
2012 ikiwa imechelewa kwa siku nne kwa mujibu wa ratiba. Mafuta hayo
yalipimwa na TBS tarehe 26 Desemba 2012 na kugundulika kuwa yako
chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Aidha, tarehe hiyo hiyo,
Kampuni binafsi ya Intertek Testing Services iliyoajiriwa na PICL pamoja na
Addax Energy SA ilipima mafuta hayo na kujiridhisha kuwa yalikuwa chini

ya viwango vinavyotakiwa.

Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali imechukua hatua zifuatazo:

1. meiagiza PICL pamoja
I
YARUDISHWE yalikotoka,

2. Imeiagiza EWURA ichukuwe hatua stahiki za KISHERIA dhidi
ya Kampuni ya Addax Energy SA,

3. PICL ichukuwe hatua zinazotakiwa dhidi ya Kampuni ya Addax
Energy SA kulingana na MKATABA, na

4. Imeziagiza PICL pamnoja na EWURA kuhakikisha kuwa hali hii
haijirudii tena hapa nchini.

Aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwahakikishia wananchi
kuwa kutopokelewa kwa mafuta hayo yaliyo chini ya viwango
HAKUTAATHIRI upatikanaji wa mafuta ya dieseli nchini kwa kuwa kwa
sasa kuna mafuta ya kutosha.

Katibu Mkuu
Dar es Salaam, Desemba 28, 2012

Vilabu 14 vinavyoshiriki ligi ya mpira wa miguu Tanzania bara vinadai pesa zao ndiyo waanze mzunguko wa pili.


Release No. 203
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 28, 2012

KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUU
Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.

Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.

TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.

OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.

Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, December 28, 2012

Unaweza ukahisi Mbunge huyu wa Tanzania anafanya nini hapo?


Mheshimiwa Nimrod Mkono (Mb) akipita kati kati ya msitu mkubwa akiwaongoza Waandishi wa habari na wadau wengine akiwaonnesha mipango na maeneo ya maendeleo anayofanya na anayokusudia kufanya katika Jimbo lake la Musoma vijijini mkoani Mara. msitu huo ni mkubwa na wenye miti yenye miiba lakini alipita, akipita mipenyo na wakati mwingi kulazimika kutambaa chini katika mstu mnene. Nyuma ya mhe.mkono kuna mtu mwingine unaonekana mkono wake tu kwa mbali sana. Kufanya kazi na Mheshimiwa huyu unatakiwa kuwa jasiri. 

Picha na Jacob Malihoja 

Twaha Shekue 'messi' wa Coastal Union B kushoto akijaribu kumtoka mchezaji wa Azam Fc B Dizana Yarouk katika fainali ya Uhai Cup. Ambapo Azam walichukua kikombe.

Eeeeh Mungu mpe umri huyu kijana maana anapiga mpira balaaaaa... pia ni mcheza wa Coastal kubwa amepandishwa katika dirisha dogo, hivyo tegemea kuona maajabu yake mzunguko wa pili ligi kuu bara. Kadalika ni nahodha wa timu ya taifa vijana chini ya miaka 17........

my president,help me to see the future....


Azam noma..... yaani noomaaaa bi maaana nooma..


KIU Dar es Salaam kinazidi kunuka....

for more information go to www.dailynews.co.tz

The falling hero.. Gen Schwarzkopf


Jan. 12, 1991 file photo, Gen. H. Norman Schwarzkopf stands at ease with his tank troops during Operation Desert Storm in Saudi Arabia.



H. Norman Schwarzkopf, the retired general credited with leading U.S.-allied forces to a victory in the first Gulf War, has died at age 78, a U.S. official confirmed to ABC News.

He died today in Tampa, Fla., a U.S. official told the Associated Press.
Schwarzkopf, sometimes called "Stormin' Norman" because of his temper, actually led Republican administrations to two military victories: a small one in Grenada in the 1980s and a big one as de facto commander of allied forces in the Gulf War in 1991.
"'Stormin' Norman' led the coalition forces to victory, ejecting the Iraqi Army from Kuwait and restoring the rightful government," read a statement by former Secretary of State Colin Powell, who was chairman of the Joint Chiefs of Staff during the Gulf War. "His leadership not only inspired his troops, but also inspired the nation."
Schwarzkopf's success during what was known as Operation Desert Storm came under President George H.W. Bush, who said today through his office that he mourned "the loss of a true American patriot and one of the great military leaders of his generation."
"Gen. Norm Schwarzkopf, to me, epitomized the 'duty, service, country' creed that has defended our freedom and seen this great nation through our most trying international crises," Bush said. "More than that, he was a good and decent man -- and a dear friend."
Bush's office released the statement though Bush, himself, was ill, hospitalized in Texas with a stubborn fever and on a liquids-only diet.
Schwarzkopf, the future four-star general, was born Aug. 24, 1934, in Trenton, N.J. He was raised as an army brat in Iran, Switzerland, Germany and Italy, following in his father's footsteps to West Point and being commissioned as a second lieutenant in 1956.
Schwarzkopf's father, who shared his name, directed the investigation of the Lindbergh baby kidnapping as head of the New Jersey State Police, later becoming a bridgadier general in the U.S. Army.
The younger Schwarzkopf earned three Silver Stars for bravery during two tours in Vietnam, gaining a reputation as an opinionated, plain-spoken commander with a sharp temper who would risk his own life for his soldiers.
"He had volunteered to go to Vietnam early just so he could get there before the war ended," said former Army Col. William McKinney, who knew Schwarzkopf from their days at West Point, according to ABC News Radio.
In 1983, as a newly-minted general, Schwarzkopf once again led troops into battle in President Reagan's invasion of Granada, a tiny Caribbean island where the White House saw American influence threatened by a Cuban-backed coup.
But he gained most of his fame in Iraq, where he used his 6-foot-3, 240-pound frame and fearsome temper to drive his troops to victory. Gruff and direct, his goal was to win the war as quickly as possible and with a focused objective: getting Iraq out of Kuwait.
"If it had been our intention to take Iraq, if it had been our intention to destroy the country, if it had been our intention to overrun the country, we could have done it unopposed," he said at a military briefing in 1991.
He spoke French and German to coalition partners, showed awareness of Arab sensitivities and served as Powell's operative man on the ground.
Powell today recalled Schwarzkopf as "a great patriot and a great soldier," who "served his country with courage and distinction for over 35 years."
"He was a good friend of mine, a close buddy," Powell added. "I will miss him."
Schwarzkopf retired from the Army after Desert Storm in 1991, writing an autobiography, becoming an advocate for prostate cancer awareness, serving on the boards of various charities and lecturing. He and his wife, Brenda, had three children.
Schwarzkopf spent his retirement in Tampa, home base for his last military assignment as commander-in-chief of U.S. Central Command.