Saturday, June 30, 2012

Kuumbwa na kujiumbua..........


Hapo vipi?


Tutafika lini huku?


Haya sasa kama ulisoma Kinondoni Muslims toklezea leo.


Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wanafunzi waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim (Reunion) zitakazofanyika Jumamosi Juni 30.

Mwenyekiti wa Reunion Bi. Mambo Tambaza alisema katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kutoka ianzishwe mwaka 1966, walimu waliowahi kufundisha shule hiyo na wanafunzi wanasoma watahudhuria.

Makamu Mwenyekiti wa Reunion, Bw. Aboubakar Liongo alisema maandalizi ya sherehe hiyo yamekamilika na sherehe hiyo itaanza saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Cine Club iliyopo Kawe, Dar es Salaam.

Alitoa wito kwa wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza ili kufahamiana na kuangalia uwezekano wa kuisaidia shule hiyo.

"Tumetoa taarifa kwa wanafunzi wote kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, ni matumaini yetu kuwa wengi watahudhuria" alisema Bw. Liongo.

Katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo na wanafunzi wanaosoma wataeleza hali ya kitaaluma katika shule hiyo na msaada wanaohitaji.


kwa hisani ya blogu ya Full shangwe.

Redds Miss Ubungo Irine Sizari akiwapungia watazamaji mkono wa pongezi jana usiku, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo. mh inamana huyo ndiyo mrembo kuliko wote katika jimbo la Mnyika?


Mpaka sasa Waislam hawajapata msimamo juu kushiriki ama kutoshiriki sensa ya mwaka huu. Kigezo kikiwa ni kutokuwepo kwa kipengele cha dini katika dodoso la sensa..... je una maoni? tupia hapo chini..

kuanzia kulia ni Sharif Hussein al Musawa mwenyekiti wa wanazuoni Tanzania, katikati ni Sheikh Mataka na mwisho ni Sheikh Iddy Simba waziri wa zamani wa viwanda na biashara.

Unamiliki gari? Toa maoni yako katika picha hii, jana hiyo maeneo ya Kinondoni Mwembe jini.


Haya tena wanakijiji wenzangu mnaopenda kozi fupi: University of dodoma inatangaza kozi za muda mfupi kuongeza ujuzi na taaluma. ushindwe mwenyewe.


SHORT COURSE ANNOUNCEMENT ON DATA PROCESSING AND ANALYSIS



  University of Dodoma College of Natural and Mathematical Sciences 
 School of Mathematical Sciences Department of Statistics

The Department of Statistics, School of Mathematical Sciences is announcing a short course on “DATA PROCESSING AND ANALYSIS” that will be conducted on July 14 – 15, 2012.

Course Description
This short course training deals with processing and analysis of raw data collected from the field. The training enables trainees to know key issues that should be considered when plan for data processing and analysis. It provides better insight into feasibility of the analysis to be performed as well as resources required.

Objective of the training
The objective of the training is to improve skills of researchers into different statistical techniques applied during data processing and analysis and hence practical interpretation of the result.

Target Group: Any interested person.
Participation Fee: Tshs 120, 000/= (The amount paid will cover tuition fee, training materials, meals, refreshments and certificate of attendance. Participants are required to come with their laptops.

Mode of payment: All payments should be done through; Account Name: College of Natural and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000 – CRDB.

Venue: University of Dodoma, School of Social Sciences (Master Class – MRL-3)
Deadline for registration and payment: 6th July, 2012
Mode of Registration: Send SMS or email indicating your name after making payment using contact below. Come with paying slip.

Contact: Short course Coordinators, Department of Statistics, P. O. Box 338, Dodoma, Mobiles: 0787288998 or 0717999012 or 0718453773; E-mail: mtakwimu@yahoo.com or abbasism2003@yahoo.co.uk

Training Timetable

Time
Saturday: July 14, 2012
Time
Sunday: July 15, 2012


08:30 - 09:00
Registration
09:00 - 10:30
Session III: Data Cleaning


09:00 – 09:40
Session I: Overview of Data
10:30 - 11:00
Break


09:40 – 10:00
Break
11:00 - 13:00
Session III resume


10:00 – 13:00
Session II:  Data management using SPSS
13:00 - 14:00
Lunch


13:00 - 14:00
Lunch
14:00 - 16:20
Session IV: Descriptive Data Analysis


14:00 – 17:30
Session II: Resume
16:20 - 16:30
Closure








NOTE: - We invite requests from various interested groups to communicate with us for the training
    to be conducted in their respective places.
-    Similar training is planned to be conducted in Mwanza in August, 2012.

Nimekukabidhi Bara loooote la Afrika utembee mpaka uchoke... ni kama Ban Kin Moon anamueleza mama Migiro.


Mama Migiro akitoa neno la shukurani baada ya kuteuliwa mjumbe maalum wa UKIMWI arani Afrika, katika hafla ya kumuaga UN Marekani.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon, akizungumza jambo wakati wa hafla ya kumuaga naibu wake Asa-Rose Migiro.


Dr Asha Rose Migiro aagwa rasmi na kupewa shavu jingine la mjumbe maalum wa masuala ya UKIMWI barani Afrika.


Na Mwandishi Maalum

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Naibu Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro kuwa  mjumbe wake maalum katika masuala yaukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika. 

Ban Ki Moon ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla maalum aliyoiandaa mahsusi kwaajili ya kumuaga  Naibu Katibu Mkuu wake ambaye anahitimisha  utumishi wa  miaka mitano na nusu   katika nafasi yake.


Hafla hiyo imefanyika   siku ya alhamisi katika viunga vya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na wageni waalikwa  mbalimbali wakiwamo mabalozi na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

“Ninatangaza rasmi kwamba ninamteua Dk.  Asha- Rose Migiro kuwa  mjumbe wangu maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani  Afrika," alisema Ban Ki Moon huku akishangiliwa kwa nguvu na wageni waalikwa.


Akiongea kwa hisia, Ban Ki Moon, ameeleza kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu wake, lakini amekuwa mwalimu kwake kwani amejifunza mengi kwa kipindi alichokaa nae na daima ataendelea kuenzi mchango wake mkubwa.

“ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha sana,  kwa ufupi siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira magumu na ya hatari,  kote ameniwakilisha vema sana, kama  mwalimu wangu, ni kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” akasema  Ban Ki Moon na kushangiliwa.

Akamuelezea  Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia  aliyebobea aliyefanya kazi kubwa ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari, umakini na uadilifu wa hali ya juu sana.

“ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya na  kuyakamilisha kwa uadilifu wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha Ban Ki Moon.

Akaongeza “Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu,  akiwamo aliyekuwa  Rais wa Libya Muammar  Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa amezikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali. Migiro  unaondoka, lakini Umoja wa  Mataifa hautasahau mchango wako. Hapa ni nyumbani kwako, na nitaendelea kuomba msaada wako na ushirikiano wako, bado nitaendelea kukuhitaji” akasisitiza Ban Ki Moon.

nae Dk Migiro alimshukuru kiongozi huyo wa umoja wa mataifa na kuita uteuzi wake ni wa heshima na suala la UKIMWI lipo moyoni mwake atalitumikia kwa uwezo wake wote.

"Masuala ya  ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba nashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu ameniamini kwamba naweza kumsaidia, naahidi nitalitekeleza  jukumu  hilo kwa heshima  kubwa".

Hafla hiyo pia imehudhuriwa  na familia ya Naibu Katibu Mkuu ikijumuisha  mume wake, Profesa  Cleophas Migiro,  mdogo wa  Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina  Mtengeti na mtoto wa  mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.

Asha-Rose Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.

hili ndilo dege Boeing 777 analotaka kununua Rais Jacob Zuma, litakaloigharimu serikali ya Afrika ya Kusini Pound Milioni 150. sio mtaalamu wa mahesabu pound moja ni Tsh za madafu 2459 zidisha mara milioni 150.


Jacob Zuma To Buy Presidential Jet Worth 150mil Pound Despite South Africa's Poverty'


Jacob Zuma is in talks to buy a £165m presidential jet, it was reported, just days after the South African president warned of growing frustration among the country's poorest over the government's failure to improve their lives.

The customised Boeing 777 plane seats 300 people and would cost $150m to buy and an additional $80m to be adapted to Mr Zuma's specifications.
The Department of Defence, which oversees VIP transport, is reportedly considering spending an additional $28m on a second private plane for Kgalema Motlanthe, the deputy president.

Defence Secretary Sam Makhudu Guluybe was on Friday visiting the United States to finalise the sale with Boeing, according to the Johannesburg Star newspaper.

The newspaper said it had documents which showed the defence department had negotiated a significant reduction on the jet's original price of $305m after a deal between Boeing and another buyer fell through.

The current presidential jet, known as Inkwazi which means "fish eagle" in Mr Zuma's mother tongue Zulu, was out of service for much of last year for upgrades and maintenance. 

<

Mpambanaji Ananilea Nkya atoa msimamo wake juu ya mgomo wa madaktari


Katika nchi  yeyote duniani serikali ndiyo  yenye  jukumu la kuweka mazingira mazuri katika hospitali za umma na kuhakikisha kuwa madaktari na wafanyakazi  wa afya  wanafanya kazi yao ya kutibu wagonjwa  kwa  furaha .

Hii  ni kwa sababu serikali  iliyowekwa  madarakani na wananchi moja ya kazi ya   kodi inayokusanya kutoka kwa wananchi   ni  kuhakikisha kuwa  hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma ziko katika mazingira mazuri na zinatoa huduma nzuri kwa wananchi.

Mazingira mazuri hospitalini ni pamoja na  kuwepo kwa vitanda vya kutosha kwa  wagonjwa,  madawa ya kutosha na ya viwango bora, vifaa kwa ajili ya kupima na kubaini magonjwa na vifaa  na vyumba maalum vya kusaidia watu  wanaofanyiwa upasuaji  wasipoteze maisha.

Lakini hali ya hosipitali zetu za umma ni hairidhishi.   Kwa mfano hospitali ya taifa ya   Rufaa Muhimbili ni hospitali  madaktari wanalalamika kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya madaktari  kushindwa kutimiza wajibu wao wa  kuokoa maisha ya wagonjwa.

Kwa mfano  hospitali hiyo ina   mashine  ya MRI  ya kupima na kutambua ugonjwa  mbali mbali  kwenye mwili ikiwa ni pamoja na kwenye   ubongo, uti wa mgongo na kifua.

Lakini  cha kushangaza mashine hiyo  iliyonunuliwa kwa  shilingi zisizopungua Bilioni mbili miaka michache iliyopita,  inapungukiwa  kifaa cha bei ndogo  tu cha    kuwezesha  watoto kupimwa.

Hivyo watoto wenye matatizo yanayohitaji kupimwa kwa mashine hiyo  wanalazimika kupelekwa India au Afrika ya Kusini kwa wale wenye uwezo  wa kujigharamia  vinginevyo kwa maskini walio wengi  huishia  watoto wenye matatizo makubwa yanayoitaji utambuzi wa mashine hiyo, huishia kufa. 

Aidha  madaktari wanalalamika   jinsi wanavyoshindwa kuokoa maisha ya watoto   wanaozaliwa na tatizo la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa. Mabingwa wa upasuaji  wa watoto katika hospitali hiyo  wanasema kwa upande wao wanajitahidi kuwafanyia  watoto hao upasuaji, lakini watoto hao huishia  hufariki dunia  kutokana na hospitali hiyo ya Rufaa kukosa  vifaa maalum vya kuhudumia watoto hao na vyumba maalumu vya kuwaweka  baada ya kufanyiwa operasheni. 

“Kinauma sana  na kinakatisha tamaa sana kuona kwamba mtoto anafanyiwa   upasuaji vizuri lakini anapoteza maisha siku chache baadaye kutokana na kukosekana kwa vifaa na mazingira ya kumwezesha  kupona baada ya upasuaji”, anasema  Dakta Catherine Mungo’ngo, Bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Rufaa ya Taifa.

Kwa mujibu wa bingwa huyo kwa mwaka huu pekee watoto watatu  waliozaliwa na tatizo la la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa ambao  walifanyiwa upasuaji  Muhimbili,    baadaye  walikufa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwasaidia kupumulia na chumba maalumu  cha kuwafanyia uangalizi baada ya upasuaji.

Aidha anasema watoto  kati ya 6 hadi 8 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku, upasuaji huo huahirishwa kutokana na ukosefu wa vifaa , dawa na chumba maalum cha kuwatunzia baada ya upasuaji.

Ni mtu gani mwenye akili timamu  ambaye atafurahia  kuona kazi anayoifanya  haitoi  matunda yanayotarajiwa.?  Ni Daktari gani  atakayeendelea kufurajhia kazi yake wakati lengo lake la kuokoa maisha ya watu  linakwamishwa  na  mambo yanayowezekana  kurekebishwa?

 Daktari furaha yake ni kutibu mgonjwa na kuona anapona. Lakini Daktari katika hospitali za  serikali  atafanyaje kazi yake kuepusha vifo  visivyo vya lazima kama hana vifaa vya kufanyia kazi ?  

Nionavyo mimi,  serikali yetu inapaswa kutafakari tena kwa utulivu na busara kubwa  na kuweka mikakati ya kupata suluhisho la kudumu la mgogoro  wake na madaktari.

Vinginevyo hata kama wataagizwa  madaktari kutoka Ulaya, na wa hapa nchini kufukuzwa kazi au hata kama viongozi wao ‘watashughulikiwa’,  tatizo la  mazingira ya kazi  hospitalini ambalo ni moja  ya  mambo ya msingi   linalosababisha mgomo wa madaktari   litakuwa halijashughulikiwa  na litaendelea kujirudia  hata kama litapoozwa   kwa mbinu yoyote ile.

 Na ikumbukwe watakaoendelea kuumia zaidi hapa ni wananchi wengi  ambao maisha yao yanategemea uwajibikaji wa serikali yao.
Nijuavyo mimi, serikali  ya wananchi, madaktari wakiwa ni sehemu ya wananchi, husikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia badala ya kutumia mabavu na vitisho.  Mungu ibariki Tanzania.
 
Ananilea Nkya
Executive Director
Tanzania Media Women's Association (TAMWA)
P. O. Box 8981, Sinza-Mori
Dar es Salaam, TANZANIA
Tel: +255-22 2772681 Fax +255 22 2772681 E-
mail:ananilea_nkya@yahoo.com
Cellphone:+255-754-464-368


Madaktari bingwa watoa tamko


Mkutano wa Madaktari bingwa jana MNH, MUHAS NA ORCI  umeamua kuungana rasmi na madaktari wote nchini katika mgomo na kusitisha utoaji wa huduma zote zikiwemo za dharura Pia wanatoa wito kwa madaktari bingwa wengine kote nchini kuungana katika mgomo huu.

Pia wanalaani vikali vitisho na manyanyaso yanayofanywa na vyombo vya dola (serikali) dhidi ya madaktari na wameitaka serikali kutoa tamko la kuwahakikishia usalama madaktari kote nchini.

Pia kuna haja ya kuweka uwezekano wa kumsafirisha Dr. Ulimboka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi; hivyo zinahitajika $40,000(sawa na takribani tsh milioni sitini na nane 68000000),mpaka sasa madaktari wamechangisha Tsh mil 40..

Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 054.

Hawa ndio waliopenya nafasi ya tano bora kati ya washiriki 12 waliopanda jukwani wa kwanza kushoto ni Amisa Zuber, SArah Utiku, Naomi James ,Winfreda Felix na Catherine Mfupi


Mshindi wa taji la Miss Redd's 2012 mkoa wa Iringa Naomi James kati kati akiwa na mshindi wa pili Sarah Utiku na Catherine Mfupi ambaye ni mshindi wa tatu mara baada ya kutangazwa usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Highlands mjini Iringa


UKIMWI unazidi kupata dawa....mhh


Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.

Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.

Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.

Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.

Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.

Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa.

Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.

Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.
Chanzo: bbc swahili.   http://www.bbc.co.uk/swahili/habari 

Tamko la Jumuiya ya Madaktari


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya usiku wa kumkia juzi, kisha kutupwa Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili.

Dk Ulimboka aliokotwa na wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha akiwa katika Viwanja vya Klabu ya Leaders, Kinondoni.

Jana, Dk Ulimboka ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili huku hali yake ikiwa haijatengemaa vyema, alitoa kauli akisema ingawa ana maumivu makali anaendelea vizuri ikilinganishwa na siku ya kwanza.

Dk Ulimboka alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa aeleze mkasa huo uliomfika wa kukamatwa, kuteswa na kutupwa msituni.
Hata hivyo, hadi sasa wingu zito la nani alimteka na watekaji walitaka kujua nini kutoka kwa kiongozi huyo wa madaktari, bado limetanda.

Siri nzito
Akisimulia mkasa huo kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema, akiwa katika klabu hiyo ya Leaders alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alikuwa atokee Tandika na baada ya kumsubiri ndipo alipofika kwenye klabu hiyo, lakini, alianza kujisikia vibaya tofauti na siku nyingine na kuongeza; "Yaani sikuwa na amani."

Alisema, "Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk Ulimboka)," alieleza na kuongeza:

"Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini halikuwa na namba."

Hata hivyo, jana Dk Ulimboka hakuonana na mwandishi wa habari hii, badala yake alirekodiwa, na Mwananchi kupata sauti yake akijibu swali kuhusu hali yake na tukio hilo, baada ya uongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kuzuia watu kumwona.

Daktari huyo wa magonjwa ya binadamu, amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).

"Kidogo najisikia nafuu ikilinganishwa na nilivyokuja ingawaje, bado nina maumivu makali. Kwa hivyo, ingependeza niendelee na mapumziko na mtu yeyote anayetaka kuniona pengine hilo jambo lisifanyike sasa. Hivi sasa ni vizuri nipumzike," ilisikika sauti hiyo ya Dk Ulimboka.

Lakini, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo.

Madaktari wanaolinda eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao.

Kiongozi jopo la madaktari

Katika hatua nyingine, kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili mzima.

“Ingawa kwa sasa anaendelea vizuri, Dk Ulimboka ameumia sana, kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza:

“Aliumia mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole na kichwani na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema.

Alifafanua kwamba, kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha yake.

Uongozi wa Moi watoa neno

Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (Moi) umeeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha taasisi hiyo.

Msemaji wa Moi, Almas Jumaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya hali yake kuendelea vizuri, lakini haingewezekana kwa waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba alikolazwa na kumwona Dk Ulimboka.

“Mgonjwa anaendelea vizuri ukilinganisha na jana (juzi), anaongea, anawatambua watu wanaokwenda kumwona, lakini utaratibu wa kwenda kumwona kwa ninyi imeshindikana kwa sababu yupo (ICU) ni chumba chenye utaratibu wake,”alisema Jumaa.

Jumaa aliongeza kwamba ili mtu aweze kuingia wodini analazimika kuvaa vazi maalumu na mavazi yaliyopo, yasingetosha, lakini pia wapo watu wanaoendelea kumpatia huduma ya matibabu.

chanzo cha habari: mjengwa.blogspot.com

Friday, June 29, 2012

wametoklezea.... wakuvanga na mwasiti, sijua nani anataka mwenzie aingie fani yake?


Mwasiti na mzee wa kurasa nao walikuwepo..


Hizi ni ofisi za idara ya habari MAELEZO. mtaa wa Samora Dar es salaam, ukiona hivi mwandishi ujue siku hiyo hakuna kazi ya kukopi na kupest, lazma uanze kutumia ujuzi wako..... ila kwa wale makanjanja si habari njema.


Dada Alice Maro, akizungumza na wanahabari. katikati ni mchekeshaji Wakuvanga aka mama bele.... leo asubuhi Serena Hotel zamani Sheraton Hotel


Seminor on Marketing for non-marketing executives. hosted by {TMCC} Tanzania Marketing Communication Conference, Bank Of Tanzania Conference Hall. today Morning.


Huyu ni jembe nae, anaitwa dada Jade Keane Communication manager Push Mobile Media Ltd. Ndiyo raha ya kutembea unakutana na watu wengi, huyu ni raia wa kigeni ila nilisahau kumuuliza anatoka nchi gani, si unajua watanzania tunaamini waafrika wote ni sawa? Leo hiyo ukumbi wa mikutano BOT.


Jembe nami sikuwa nyuma, kikoloni nakijuajua. nafuatilia mjadala wa wasomi, bank kuu ya Tanzania leo asubuhi.


Rodgers Mbaga, Mkurugenzi wa kampuni ya Marketing Initiatives LTD. akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya siku moja kujadili masuala ya masoko katika makampuni yanayoendeshwa na viongozi wasio na uelewa wa masoko. leo Benki kuu ya tanzania.


Jembe ephraem Mafuru, akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya uelewa wa masoko Tanzania.


tigo imewakumbuka wateja wake coco beach kesho


Na Hafidh Kido

Tigo imejipanga kuwapa burudani wakaazi wa jiji la Dar es Salaam siku ya jumamosi na jumapili mwishoni mwa wiki hii katika fukwe za coco beach. Lengo likiwa ni kuwaandaa watumiaji wa tigo na sikukuu ya sabasaba.

Akizungumza na wanahabari katika hoteli ya serena leo asubuhi afisa habari wa kampuni hiyo ya mawasiliano bi Alice Maro, amesema kampuni yake imeamua kuwapa burudani nyingi watumiaji wa mtandao huo lengo likiwa ni kuwa nao karibu na kufahamiana zaidi.

“Mwaka huu tumeamua kuwaletea burudani nyingi za kutosha, hatutotaka wateja wetu waje tu kufurahi mwisho wa wiki hii ila tungependa pia wapate fursa ya kupata huduma zetu bora na nafuu zilizoandaliwa kwa ajili yao.”

Aidha tigo katika kunogesha shughuli hiyo waeamua kuonyesha fainali za mpira wa miguu za ulaya kati ya Italy na Hispania siku ya jumapili, sherehe hizo zitasindikizwa na wasanii maarufu watakaokonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hasa pale wasanii mahasimu Izzo B pamoja na Roma Mkatoliki watakapopanda jukwaa moja siku hiyo.

“Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa ni siku ya jumapili na burudani kutoka kwa Juma nature, Roma mkatoliki, izzo B, Professor J, Mwasiti, Barnabas, Fid Q, Joe Makini na burudani maalum kutoka kundi la vichekesho la “Ze Comedy,” alisema Alice.

Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania ulioanza biashara mwaka 1994, na ni mtandao wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma katika mokoa yote 26 Tanzania bara na visiwani. Ingawa katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko ya mitambo ya mtandao huo kutokuwa mizuri wakati wa mawasiliano.


Thursday, June 28, 2012

Tusikilize majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu leo kwa faida yetu.

Mwanakijiji mwenzangu, leo jiandae kusikiliza majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu Mizengo Pinda. Kuna mengi yanategemewa kutoka katika kauli ya serikali, watu wana matumaini makubwa kwa huyu mtoto wa mkulima anaweza kuwasaidia katika kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.

Hasa katika suala la mashangingi (magari ya gharama) na mambo mengi ambayo hayana umuhimu katika ofisi za serikali. Kumbuka ofisi ya waziri mkuu ndiyo inayoshikilia asilimia kubwa ya mhimili wa kwanza wa dola, yaani Serikali. Kwani viongozi wengi wanawajibika chini yake kuanzia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa, wenyeviti serikali za mitaa, madiwani na wakurugenzi wa mikoa na wilaya, listi ni ndefu.

Na huko kuna uzembe mwingi unafanyika hasa kwa kudhani wananchi hawana uelewa wa namna ya kuwawajibisha viongozi hao. Juzi mbunge mpya na kijana Joshua Nassari kutoka Arumeru Mashariki aliongea kitu watu wakaona ni cha kijinga. Alihoji ni kwanini wakuu wa mikoa na wilaya wamejazana bungeni kusikiliza bajeti ya ofisi ya waziri mkuu wakati wananchi wapo mikoani wana shida na uwepo wao.

Kwanini wasifuatilie bunge wakiwa ofisini badala yake watumie magari ya serikali,mafuta, malazi na chakula kukaa bungeni tu bila ya shughuli yoyote?

naomba kuwasilisha, Kido Jembeeeeeeeeeeeeeeee.

Jembe langu Charles Shola, likipokea cheti kuonyesha amekamilisha shahada yake ya uzamili nchini Urusi.


kama kweli wewe ni mwenyeji wa Tanga niambie msikiti huu unaitwaje.


Unapokuwa mwanahabari ni lazima ukubali kukaa na watu kama hawa. hasa vibaraza vya kahawa vinakuwa na habari nyingi, jambo moja usikubali wakugundue wewe ni mgeni, watakuwa mabubu. usiniulize kwanini.


jokes corner

As a family of 5 was having supper, the youngest son asked his father, "What is the difference between IMAGINATION & REALITY?"(father turns and asks mother, "Would you have sex with Mr. Kamau for 1million sh?" Mother:YES why not? (father turns and asks daughter)"Would you have sex with Rudisha for 1m? Daughter; why not? (father then asks elder son) Son would you have sex with Edward for 1m sh? Son; why not. Father: You see my son, we imagine we have 3millionares but reality is we are leaving with two prostitutes and 1 gay.

Unajua Maalim Seif Sharif Hamad na Iasmail Jusssa ni marafiki wa zamani/ hiyo ni miaka ya thamanini wakati Seif alipotoka gereza la Mbwela kutumikia kifungo cha uhaini. Jussa upande wa kulia na Seif kati kati.


Wkija kututembelea hujidai kufanana na sisi.


How do we nurture their talents?


Hapa nani anamuomba mwenzie? kikwete anataka kura,kijana anataka kula.


Utajiri uliolaaniwa.


Tathmini yangu mkutano wa Chadema Dar es Salaam.




wiki kadhaa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,kimefanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam. Wametega siku muhimu kwa kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Dar es Salaam walikuwa wakifuatilia mwenendo wa kesi ya mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika (chadema). Ambae alishitakiwa na mama Hawa Ng’umbi ambae alikuwa mgombea wa kiti hicho pia kupitia CCM. Lakini mnyika akashinda kesi hiyo.

Nimegundua kwa muda mrefu CHADEMA wanaumezea mate mji huu, kwani ni kambi ya ccm na cuf. Hilohalihitaji mjadala. Nimegundua bado idadi kubwa ya wakaazi wa jiji hili wana mapenzi na ccm ama cuf, chadema bado kidogo, idadi ya watu niliyoiona leo ni kubwa ila haifikii ccm wala cuf pindi wanapofanya mikutano yao Dar es salaam.

Hotuba aliyoitoa Mnyika, mbunge wa Ubungo inaonyesha wazi dhamira ya chadema kutaka kuliteka jiji, pale alipowahamasisha wana jiji kujiunga na vuguvugu la mabadiliko (movement for change) linaloendeshwa na chama hicho kwani hata kipindi cha kudai uhuru wazee na vijana wa jiji hili ndiwo waliokuwa mstari wa mbele.

Mwenyekiti Freeman Mbowe, katibu mkuu Dr Slaa na mtaalamu wa sheria wa chadema Tundu Lissu, hawakuongea vitu vipya kama nilivyotegemea zaidi ya kuwahamasisha watanzania kuiangalia katiba hasa katika vipengele viwili vya mamlaka ya Rais na uhalali wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.

Ugumu wa maisha imeonekana ni mada anazozipenda katibu mkuu wa chadema Dr Slaa, kwani amekuwa akirudia maneno hayo kila anapopata nafasi ya kuzungumza na watanzania.

Ibaki tu kuwa lengo la mkutano wa leo uliopewa kauli mbiu ya ‘VUA GAMBA VAA GWANDA’ ni mkakati wa chadema kuuteka mji huu na kuwa miongoni mwa ngome zao na kufuta ile dhana ya ukaskazini. Yaani wanapendwa zaidi mikoa ya kaskazini.

Siku hiyo ya mkutano asubuhi nilikuwa nikilumbana kwa hoja na katibu wa itikadi na uenezi ccm ndugu Nape Nnauye katika ukurasa wake wa facebook, nilikuwa nikimwambia ajiangalie sana na chama chake kwani chadema watawaadhirisha. Watu wanajivua magamba na kuvaa magwanda kwa idadi kubwa. Akanijibu kumbe ninajua kuwa magamba ndiyo yanayokwenda chadema basi hawana maana.nikamjibu Kiswahili kinamsumbua?

Kwani waliposema wana-ccm walioshindwa wajivue magamba, maana yake wakishajivua magamba wanayaacha ccm hayomagamba na kuwa wasafi. Na chadema kinachukua wana-ccm waliojivua magamba. Hivyo kwa tafsiri ya harakaharaka waliobaki ccm ndiwo magamba.

 Naomba kuwasilisha.

Wabunge wakiukana ubunge wao nami nitaukana utanzania wangu



Na Hafidh kido

Siku zinazidi kusonga bunge la bajeti linakaribia kuisha, ni kikao ambacho watu tuliowapa dhamana kutuwakilisha kwa serikali wanajadili mustakabali wetu kiuchumi.

Lakini kuna jambo moja ambalo mpaka sasa ufumbuzi wake una utata, suala la posho za vikao.

Siku spika wa bunge mama Anne Makinda, alizungumza na wapiga kura wake wa Njombe kusini, mjini Iringa kuhusu suala la wabunge kutaka kuachia ubunge kutokana na umaskini, ilinidhihirikia kuwa mama yule anafanya kila namna kuiweka pembeni hoja ya wabunge vijana juu ya ubadhirifu wa pesa za umma kwa kulundikiana mafungu yasiyo na tija.

Swali moja lingetosha kumuumbua mama Makinda, je katika kikao gani nusu ya wabunge ambao ni takriban wabunge 150 katika idadi ya wabunge zaidi ya 300 walipata kumwelezea kadhia hiyo ya kuandamwa na ufukara kutokana na wao kuchagua kuwa wabunge?

Sawa tuseme alizungumza maoni ya jumla baada ya kupata malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa vijana wake, lakini kwa namna alivyokuwa akiongea katika luninga siku ile ni wazi yeye alivaa joho la uwakilishi wa ufukara unaowaandama wabunge. Hata kufikia kusema kwa miaka yote aliyokuwa mbunge hajafanikiwa kujenga hata nyumba yake mwenyewe, anajidai kumuiga Nyerere.

Hakuonekana kusikitishwa na kauli hizo bali alitaka kuonekana shujaa kwa wabunge walafi wasiokuwa na shukurani wala huruma kwa wananchi maskini wasiojua watakula nini wala watapata wapi nauli ya kufika kibaruani ili wakamenyeke kwa ajili ya mlo wa siku moja ‘kesho ina Mungu.’

Spika Makinda kwa madaha kabisa aliwaambia wananchi wa jimbo lake ambao wengi ni maskini kuwa hivi sasa nusu ya wabunge wa bunge la Tanzania wanataka kuacha ubunge kutokana na kulipwa malipo madogo.

Hakuishia hapo bali aliendelea kusema kwa miaka ijayo wabunge wenye taaluma zao hawatagombea tena ubunge ikiwa malipo yataendelea kuwa hivi kwasababu ubunge ni eneo la umaskini wa kutupwa kabisa.

Angalia kituko hiki, mama huyo mwenye heshima zake anaongea maneno hayo mbele ya wananchi ambao nusu yake hawana ajira, na wenye ajira wanalipwa mishahara isiyozidi laki nne kwa mwezi bila ya marupurupu ya chakula, usafiri wala nyumba. Halafu anawatetea wabunge ambao wanalipwa mishahara ya shilingi milioni mbili na nusu kwa mwezi, pesa ya mafuta ya gari, wanalipwa posho ya shilingi 80,000/= kwa kikao, wakiwa Dodoma wanalipwa posho ya kujikimu shilingi 70,000/= kwa siku.

Kwa mwaka tuseme vikao vyote vya bajeti viwe ni miezi mitano, yaani tukiviunganisha kwa pamoja. Na vikao vingine vya kawaida vikiunganishwa vyote viwe ni miezi miwili, maana yake kwa mwaka wanakutana kwa miezi saba mfululizo (tukiunganisha) ambapo katika kipindi hicho cha miezi saba kwa siku mbunge akienda Dodoma akihudhuria kikao au asihudhurie ana shilingi 80,000/= kibindoni ya kujikimu, akihudhuria analipwa shilingi 70,000/= ya kikao maana yake anapata shilingi 350,000/= kwa siku tano za vikao tu, posho za kujikimu zinalipwa wiki nzima ambazo ni shilingi 560,000/=, ukijumlisha malipo ya wiki tu ni shilingi 910,000/= Kwa mwezi ni zaidi ya shilingi milioni tatu na laki sita mara miezi saba ni zaidi ya milioni ishirini na tano.

Kumbuka hiyo ni posho ya vikao tu sijaingiza posho ya mafuta, kadhalika sijaingiza mfuko wa jimbo, kadhalika sijaingiza wale wabunge ambao wapo katika kamati za bunge ambao nao wana vikao vyao vya kikamati, posho za safari na mambo mengine pale inapohitajika, kadhalika sijaingiza mishahara ambayo kwa mwaka ni milioni thalathini. Halafu unatuambia ubunge ni dimbwi la ufukara, tukuelewe vipi?

Fikiria mtanzania ambae analipwa laki na nusu kwa mwezi hakuna posho wala safari zitakazomfanya awe na kipato kingine. Anafanya kazi kuanzia asubuhi na mapema mpaka jioni giza linapoingia. Mtu huyu ukiunganisha mshahara wake wa laki na nusu kwa mwaka ni milioni moja na laki nane, pesa ambayo mbunge anaipata kwa wiki mbili tu.

Sijakataa mbunge kuacha shughuli ambayo anadhani itamtia umaskini, sasa hawa ambao tayari ni maskini je wafanye nini?

Ndipo nikasema ikiwa wabunge watakana dhamana tulizowapa wakatutetee ili kwa pamoja tuondokane katika dimbwi la ufukara matokeo yake wanataka kuwa matajiri peke yao, basi na sisi kwakuwa tayari tu maskini itabidi tuukane utanzania wetu ili tukimbilie ulaya kama wakimbizi wa kisomali, Kinyarwanda ama warundi ili tupokewe tupewa hifadhi katika mataifa tajiri nasi tuwe na nafuu ya maisha kama ambavyo watanzania wengi huishi hivyo nchini uingereza, ubelgiji, na nchi nyingi za bara la Amerika na Australia. Wenyewe wanaita kujilipua.

Swali moja kwa mama Makinda, hivi hao wabunge anaosema wana taaluma zao ni kitu gani kilichowafanya waache kulitumikia taifa lao kulingana na taaluma walizonazo kama uanasheria, uinjinia, udaktari, ualimu ama uhasibu na badala yake wakakimbilia bungeni ambako hakuna maana yoyote?

Hakuna kitu kibaya katika maisha ya msomi kama kushindwa kuchagua, tamaa ni maradhi mabaya sana katika taifa changa linalohitaji uzalendo na kujitolea kwingi kwa faida ya wote.

Najua nitaonekana kichaa ama sijui ninachozungumza, mara nyingine maelezo ya wabunge yanaweza kuwa na mantiki kwa namna moja ama nyingine. Kitendo cha kuwajaza mapesa wabunge ndicho kinachowapa kiburi na kutaka zaidi, siku zote anaepata kingi haridhiki lakini anaepata kidogo hujifunza kuweka ili kimfae baadae.

Kwa mfano kipindi cha awamu ya kwanza ubunge ulikuwa ni kazi ya hiyari, wala watu hawakutumia mapesa mingi kupata nafasi ya ubunge, tofauti na sasa ni biashara na ndiyo maana baada ya wabunge kuona biashara inapunguza mvuto wanadai nyongeza ya kingi; wapo wazee ambao walikuwa wabunge na mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza sijui serikali ina mpango nao gani, lakini wanaishi maisha ya chini kabisa.

Hii inaonyesha wazi walikuwa wakiwatumikia watanzania kwa moyo wote na si kutaka kujilimbikizia mali na kusahau kilichowapeleka bungeni. Tazama watu wanazusha hoja binafsi kwa kununuliwa. Tajiri mmoja tu anaweza kumnunua mbunge na kumwambia peleka hoja hii ikajadiliwe, ikipita tu nakuandalia tumilioni kadhaa. Vitu hivi vipo tusikatae.

Maneno ya wazee waasisi wa nchi hii hata siku moja hayawezi kuanguka, walisema kiongozi akiingia kwa rushwa hata siku moja hatoweza kuongoza kwa ufanisi kwani itabidi aanze kuwaridhisha wale waliompatia fedha kuingia madarakani.

Ubunge ni biashara na ndiyo maana wanaanza kuona hasara, fikiria mtu anakwenda kukopa mamilioni ya fedha, nyingine anakwenda kuomba kwa wafanyabiashara wakubwa ambao malipo yao ni kufuata kila wanachokitaka pindi ukishika madaraka.
Na ndiyo maana baadhi ya ‘wabunge maslahi’ wanaanza kuona hali ni ngumu, miaka mitano inakwisha hajarudisha hata nusu ya alichopoteza, na bado hajamaliza madeni huku wale watu waliomfadhili wanataka kulipwa fadhila kwa mambo ambayo kwa nafasi yake ya ubunge hawezi kuyatimiza, hapo ndipo anapojuta na kuona ubunge ni mzigo.

Naamini mtu ambae ameingia bungeni kwa njia safi na halali hata siku moja hawezi kuwa na majuto, kwani kwa hali za watanzania malipo wanayoyapata wabunge ni makubwa sana hakuna mfanyakazi yeyote anaeweza kuyapata hata awe mkurugenzi.

Tafadhali rejea mchanganuo wa pesa wanazopata wabunge wetu halafu linganisha na maisha ama pesa unazopata kwa mwezi. Hata msomaji akiwa ni mkurugenzi wa shirika lolote ima la umma ama la binafsi hawezi kufikia pesa anazopata mbunge.
Halafu leo wanakwenda kutuambia kiasi wanachopata kinawatia umaskini.
Yaani sijapata kusikia upumbavu namna hii tangu nimezaliwa, hivi hawa wabunge wetu wanatuonaje sisi watanzania. Nauliza kwa nia njema tu wala si kwa kebehi, leo hii kila mtu anatamani kuishi maisha anayoishi mbunge halafu wanakuja kutuambia ubunge unawatia ufukara wanajua kweli fukara wa kitanzania anapata shilingi ngapi kwa siku?


Naishia hapa nisije kutukana bure.

Naomba kuwasilisha.