Sunday, September 7, 2014
Friday, September 5, 2014
China yaishawishi A.Kusini kumzuia Dalai Lama
Dalai Lama
Kiongozi wa kiroho wa Tibet,
Dalai Lama, amesitisha ziara yake nchini Afrika Kusini ambako alitarajiwa
kukutana na washindi wenzake wa tuzo ya Nobel,mjini Cape Town mwezi ujao.
Kiongozi huyo ambaye yuko uhamishoni,
alisitisha ombi lake la Viza kuingia Afrika Kusini baada ya maafisa wake kusema
kuwa huenda akanyimwa viza hiyo.Serikali ya Afrika Kusini imekanusha madai ya kumnyima Dalai Lama Visa kutokana na shinikizo kutoka kwa China ambaye ni mshirika wake mkubwa wa kiuchumi.
China inamuona Dalai Lama ambaye hutetea haki za watu wa Tibet kama kiongozi hatari anayetaka kusambaratisha nchi hiyo.
Miaka miwili iliyopita mahakama ilisema kuwa Afrika Kusini ilikiuka sheria kwa kuchelewa bila sababu kumpa Dalai Lama Viza kuingia nchini humo.
kuchelewa huko kulimaanisha kwamba Dalai Lama asingeweza kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya rafiki yake mkubwa askofu mstaafu Desmond Tutu mjini Cape Town.
CHANZO: BBC
SWAHILI
Ajali Mbaya Musoma.....
Miili ya marehemu ikisubiri kutambuliwa.
Mabasi yaliyogongana leo
Basi la Jumanne lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma.
Mpaka sasa inadaiwa zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha huku wengine wameumia vibaya.
endelea kufuatilia zaidi...
Ajali hiyo imehusisha basi la
Mwanza coach lenye namba za usajili T 736 AWJ lililokuwa likitokea Musoma
kwenda Mwanza na basi la J4 lenye namba za usajili T 677 CYC likitokea
Mwanza kwenda Sirari na gari dogo aina ya Land Cruiser ambayo namba zake hazikuweza
kufahamika mara moja kugongana uso kwa uso majira ya saa 5 asabuhi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa
niaba ya Mganga Mkuu,Dakatari wa hospitali hiyo Martini Khani alisema kuna
idadi kubwa ya maiti zilizopokelewa pamoja na majeruhi na idadi kamili ya vifo
na majeruhi itfahamika baadaye.
Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wa
ajali hiyo walisema mabasi hayo ambayo yote yalikuwa kwenye mwendo kasi
yalikutana kwenye daraja dogo katika eneo hilo huku pia gari dogo aina ya Land
Cruiser lililokuwa likitokea Musoma likitaka kulipita basi la Mwanza Coach hali
iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.
ICC yaahirisha kesi ya Rais Kenyatta
Uhuru Kenyatta
Kiongozi wa mashitaka katika
mahakama ya kimataifa ya ICC, Fatou Bensouda, ameiomba mahakama hiyo kuahirisha
kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa muda usiojulikana.
Hii ni baada ya malalamiko kutoka
kwake kuwa Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo katika kuikabidhi
ushahidi unaohitajika kuendesha kesi kwa hiyo ina maana kuwa hana ushahidi wa
kutosha dhidi ya Kenyatta.
Serikali ya Kenya ilitakiwa
kuikabidhi mahakama taarifa za kifedha za Rais Kenyatta pamoja na maelezo
kuhusu mali yote anayomiliki.
Katika uamuzi uliotolewa na mahakama
hiyo Fatou Bensouda amesema kuwa hana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka
Rais Kenyatta ambaye anadaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu
nchini Kenya mwaka 2007.
Zaidi ya watu 1,000 walifariki
katika ghasia hizo. Bensouda amenukuliwa akisema kuwa halitakuwa jambo la
busara kufutulia mbali kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa Kenya haitaki kutoa
ushahidi unaohitajika na mahakama hiyo.
Badala yake aliomba mahakama
kuiahirisha kesi hiyo hadi pale Kenya itakapokubali kutoa ushahidi
unaohitajika.
Kesi dhidi ya Kenyatta ilipaswa
kuanza mapema mwezi Oktoba.
CHANZO: BBC
SWAHILI
Subscribe to:
Posts (Atom)