Wednesday, December 10, 2014

Ziara ya naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira

 Ofisa Uhusiano wa kampuni ya SBS, Geofrey Kanenge  (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) (wa pili kushoto)  kuhusu udhibiti wa utiririshaji wa maji taka yatokanayo na usafishaji wa mapipa yenye kemikali unavyofanywa na kampuni hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Mtwara.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (katikati) akipata maelezo kuhusu ubanguaji wa korosho kutoka kwa Uongozi wa Kiwanda cha Micronix  kilichopo mkoani Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mkoani humo.

 Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kukagua hali ya Mazingira ya viwanda  aliyoifanya mkoani Mtwara.

Eneo la bwawa la asili la Mdenga lililofukiwa kinyume cha sheria na kampuni ya SBS inayojishughulisha na urejelezaji wa taka mkoani Mtwara na kusababisha uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.


No comments:

Post a Comment