Raia wa Guinea Bissau kuchagua rais mpya
Bissau, Guinea-Bissau
Ni uchaguzi wa Kwanza tangu
kufanyika kwa mapinduzi miaka miwili iliopita -ikiwa ni hatua ya hivi karibuni
ya kijeshi ambayo imesaidia kuhakikisha kwamba hakuna raisi aliyechaguliwa
ambaye amefanikiwa kuiongoza Guinea Bissau kwa kipindi chote alichochaguliwa
tangu taifa hilo lijipatie Uhuru wake kutoka kwa Ureno mnamo mwaka 1974.
Kiongozi wa mapinduzi hayo Antonio
Indjai aliikabidhi mamlaka serikali ya raia mnamo mwaka 2012 iliopewa wajibu wa
kuandaa Uchaguzi huo.
Indjai alifunguliwa mashtaka nchini
marekani kwa madai ya kufanya biashara ya mihadarati pamoja na kuwauzia silaha
waasi wa Colombia.Wagombea 13 wanawania wadhfa wa urais.
Iwapo mmoja wao hatashinda kwa wingi
wa kura basi uchaguzi huo utaenda kwa awamu ya pili mnamo mwezi May.
Marekani yaionya Urusi kuhusu Ukraine.
Kiev, Ukraine
Marekani imeonyesha wasiwasi wake kuhusu kile ilichokitaja kama harakati za kundi fulani linalotaka kujitenga ambalo limekuwa likisaidiwa na Urusi kuchochea ghasia mashariki mwa Ukrain.
Kufuatia kutekwanyara kwa vituo vya
polisi katika miji kadhaa ya mashariki mwa Ukrain ,waziri wa maswala ya kigeni
nchini marekani John Kerry amesema kuwa mashambulizi hayo ya watu waliojihami
na silaha za Urusi yalifanyika kwa mpangilio.
Katika mazungumzo yao ya simu na
waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov,Kerry ameitaka Urusi
kusitisha mashambulizi kama hayo la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi.
Urusi imeonya kuwa utumiaji wowote wa
nguvu nchini Ukrain utahujumu harakati za kidiplomasia kumaliza mgogoro huo.
Boko Haram ladaiwa kuwaua watu laki moja
Abuja, Nigeria
Sasa imebainika kuwa wanamgambo wa
kiislamu kazkazini mwa Nigeria wamewaua zaidi ya watu laki moja na arubaini na
tano katika misururu ya mashambulizi juma lililopita.
Sineta wa jimbo la kazkazini
mashariki la Borno Ahmed Zannah ameiambia BBC kwamba mauaji hayo yalifanyika
katika maeneo matatu tofauti yaliopo mashambani.
Amesema kuwa taassi moja ya kutoa
mafunzo ya elimu ndio iliokuwa ya kwanza kulengwa ambapo wanamgambo hao
waliwaua walimu watano kabla ya kuwatekanyara wake zao kadhaa.
Wapiganaji hao wanaoshukiwa kutoka
katika kundi la wanamgambo wa Boko haram baadaye walivamia vijiji viwili katika
eneo la mashambani karibu na mpaka na Cameroon.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment