TOKYO, Japan
Daktari mmoja aamua kufanya kile
ambacho hakikutegemewa na wengi, kwa kupachika kamera kwa siri katika vyoo
vilivyoko katika hospitali anayofanyia kazi na kufanikiwa kuwa chungulia
wagonjwa wapatao 100 walipokuwa wakijisaidia na idadi hiyo ni watu wazima na
watoto.
Dokta Lam Hoe Yeoh almaarufu Robin
mwenye umri wa miaka 61 anayetokea BansteadSurrey,anatuhumiwa kwa makosa 30
yakiwemo makosa mawili ya kuchungulia watoto na kuwarekodi,na makubwa Zaidi ni
yanayo karibia kua ya kingono.
Inaelezwa kwamba alikamatwa mapema
mwaka huu akiwa katika hospitali binafsi ya St Anthony iliyoko kaskazini .
Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo ameiahirisha mpaka September 16 mwaka huu
wakati ambapo dokta Yeoh atakapoyakabili mashtaka,na yaelezwa dokta huyo
anashikiliwa lupango.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment