MONROVIA,
Liberia
Wakati
ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuumiza vichwa vya wanasayansi walio wengi juu ya
namna ya kuboresha tiba ya majaribio ya Zimapp,mengi yameendelea kuibuka juu ya
ugonjwa huu.
Kuna taarifa kua madaktari wasio na
mipaka( medical charity Médecins Sans Frontières ) wamekosoa uwajibikaji wa
umoja wa mataifa pamoja na shirika la afya duniani WHO suala la ugonjwa wa
Ebola huko Africa Magharibi.
Mkurugenzi wa madaktari hao wasio na
mipaka Brice de la Vigne,ameeleza namna ugonjwa wa Ebola na unavyoenezwa
unavyochukuliwa ni sawa na hakuna juhudi yoyote ama kwakifupi ni sifuri
kiutendaji kwa wadau hao wakuu .
Kufuatia shutuma hizo shirika la
Afya duniani haikukaa kimya na hivyo walisimama na kujitetea, na hivyo msemaji
wa W.H.O alisema shirika lake limejitahidi kuongeza idadi ya wahudumu wa afya
na mipango pamoja na usambazaji wa wataalamu hao katika maeneo yaliyoathiriwa
na ugonjwa huo,hivyo si kweli kwamba hawajafanya kitu chochocte.
Shirika hilo la Afya ulimwenguni
W.H.O limetoa takwimu ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola
Africa Magharibi kwamba kufikia sasa inazidi kuongezeka na kufikia zaidi ya
wafu elfu kumi na watatu.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment