Maafisa wanne wa polisi na raia
wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar
es salaam Tanzania.
Shambulizi hilo limetokea katika
kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam.
Polisi wanasema kuwa wavamizi hao
walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.
Waliwafyatulia risasi maafisa wa
polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Kwa mujibu na raia wanoishi karibu
na kituo hicho,makabiliano ya risasi yalidumu kwa zaidi ya saa moja.
Uchunguzi unaendelea kujua nani
aliyetekeleza shambulizi hilo
Mkuu wa polisi Ernest Mangu
amethibitisha uvamizi huo akisema askari 4 na raia 3 wameaga dunia.
Hadi sasa haijabainika iwapo kuna
majeruhi.
Aidha amesema kuwa walipora handaki
ya kituo hicho na kuiba bunduki za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.
Hakuna aliyekamatwa kufuatia
shambulizi hilo
Hakuna aliyekamatwa kufuatia
shambulizi hilo japo maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.
Kulikuwa na matone ya damu nje ya
kituo hicho cha polisi dalili kuwa waliojeruhiwa walikuwa wakijaribu kutafuta
msaada.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza
shambulizi hilo japo bwana Mangu anasema kuwa ni mapema mno kusema kuwa
shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi.
Hii si mara ya kwanza kwa kituo cha
polisi kuvamiwa, mwaka uliopita kundi la watu waliokuwa wamejihami lilivamia
kituo cha polisi na kukimbilia mwituni.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment