Rais wa Nigeria Muhammadu
Buhari,amewafuta kazi wakuu wa jeshi la angani,wanamaji na nchi kavu.
Inaaminika kuwa rais huyo mpya wa
Nigeria amewatimua maafisa hao wakuu jeshini kwa 'kushindwa' kukabiliana na
kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Hatua hii haikuwashangaza
wachanganuzi wa maswala ya kiusalama nchini humo kwani rais Buhari ambaye
mwenyewe ni jenerali mstaafu alikuwa ameahidi wapiga kura katika uchaguzi mkuu
uliopita kuwa ataitokomeza kabisa kundi hilo la Boko Haram.
Zaidi ya watu 220 wameuawa katika
kipindi cha siku 10 tu zilizopita
Habari hii ya kutimuliwa wakuu
imetangazwa siku chache tu baada ya mkuu wa jeshi Jenerali Kenneth Minima
kusema kuwa
''ongezeko la mashambulizi
yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuwatisha wanajeshi ambao yamkini wamewabana
Boko Haram''
Jenerali huyo alisema kuwa kundi
hilo limeanza kushambulia watu walioko sokoni na katika majumba ya ibada kwani
wameshindwa kupambana na wanajeshi.
Zaidi ya watu 220 wameuawa katika kipindi
cha siku 10 tu zilizopita kufuatia mashambulizi ya mabomu na ya kujitolea
mhanga.
Shambulizi la hivi punde zaidi
lilitokea katika mji wa Fotokol ulioko karibu na Cameroon ambapo takriban watu
13 walipoteza maisha yao jumapili.
Viongozi wakuu wapya wa jeshi
wanatarajiwa kutangazwa muda mchache ujao.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment