Saturday, December 7, 2013

MABASI YAENDAYO KASI YAANZA KUTUA BONGO...CHEKI MUONEKANO PICHANI..Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara-kivukoni. Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo kasi limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.
 Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.

Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo  huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.

No comments:

Post a Comment