Mehdi Jomaa alikuwa waziri wa viwanda hadi alipoteuliwa kama
waziri mkuu.
Wanasiasa nchini Tunisia wamefikia
makubaliano kuhusu waziri mkuu mpya baada ya mazungumzo kati ya chama tawala
cha Ennahda na upinzani.
Mehdi Jomaa, waziri wa viwanda,
ataongoza serikali ya mpito hadi uchaguzi utakapofanyika mwaka ujao.
Jina la Bwana Mehdi lilikuwa moja
kati ya majina ya watu sita walioteuliwa kushikilia wadhifa huo katika
mazungumzo yaliyofanyika siku ya Jumamosi.
Mgogoro wa kisiasa Tunisia umekuwa
ukitokota tangu kuuawa kwa wanasiasa wawili wakuu mapema mwaka huu.
Uteuzi huo ni sehemu ya makubaliano
yaliofikiwa Alhamsi ambapo wanasiasa waisilamu wenye msimamo wa kadri
watakabidhi mamlaka ili kumaliza mgogoro huo wa kisiasa.
Mauaji ya mwanasiasa Chokri Belaid
mnamo mwezi Februri na mwenzake wa upinzani Mohammed Brahmimwezi Julai
yalicochea maandamano dhidi ya serikali.
Chama cha Ennahda kililaani mauaji
hayo. Lakini upinzani umekituhumu kwa kukosa kuwachukulia hatua wanasiasa
waisilamu wenye itikadi kali ambao huenda walihusika na mauaji hayo.
Mgogoro wa kisiasa uliofuata mauaji
hayo, umetishia kusambaratisha kipindi cha mpito ambacho kilianza baada ya
maandamano ya kiraia yaliyopindua serikali ya aliyekuwa Rais Zine al Abidine
Ben Ali mwanzoni mwaka 2011.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment