Saturday, September 1, 2012



Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe akiwa na baadhi ya viongozi wa Tawi la Chadema DMV aliopowasili siku ya Ijumaa Aug 31, 2012, kwenye uwanja wa kimataifa Dulles Airport, kwaajili ya mkutano uliofanyika leo Siku ya Jumamosi Spet 1,2012 .

Mkutana huo uliaza rasmi saa 4:PM (Kumi za Jioni) Wageni rasmi wamkutano huo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe Joseph Mbilinyi ADDR. Addr: 9670 Baltimore Ave. College Park. MD 20740

Sensa yasogezwa mbele...


Na : Tiganya Vincent-  MAELEZO-Dar es salaam

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeongeza mbele tarehe za kumaliza kazi ya sensa ya watu na makazi hadi Jumamosi ya tarehe 8 septemba mwaka huu ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliyebaki anahesabiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo(jana) na Kamishna wa Sensa kutoka NBS Hajjat Amina Mrisho Said wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali yaliyohusu kazi nzima ya kuhesabu watu na makazi inaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Alisema kuwa ni vema wananchi ambao hawajafikiwa na makarani wa sensa watoe taarifa katika Ofisi za Serikali za Mitaa au Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuhesabiwa.


Hajjat Amina alisema taarifa zinazotakiwa ni pamoja na taarifa za wanakaya waliolala katika kaya yao usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti mwaka huu.


Alitoa wito kwa wale ambao hawajaandikishwa hadi hivi sasa wanatakiwa watume taarifa kwa namba 2122724, 0754583415, 2129622 ,0713335429,0713574622 na 0713312699 .


Hajjat aliongeza kuwa katika taarifa watakazopeleka ni vema wakaeleza mitaa au kijiji au kitongoji gani walipo ili iwe rahisi kwa NBS kutambua karani mhusika na kumwelekeza afanye kazi hiyo.


Aidha , Kamishna hiyo alisema kuwa malipo ya makarani yalishafanyika kwa awamu ya kwanza kulingana na mkataba na wanataraji kuwalipa awamu ya pili mara baada ya kazi zao kuhakikiwa na wasimamizi wao.


Aliongeza kuwa kwa wasimamizi watalipwa baada ya kazi zao kukamilika na kuhakikiwa na waratibu katika ngazi za wilaya.


Kuhusu malipo ya wenyeviti wa vijiji , vitongoji na mitaa ,alisema fedha zao wasishapelekwa siku nyingi na maelekezo ya namna ya kuzigawa yalipelekwa kwa waratibu wa Sensa wa mikoa na wilaya ambao walipaswa kuwa wameshalipa ili kuepuka manung’uniko.


Katika hatua nyingine Kamishna wa Sensa huyo amewaonya kuwa Karani yoyote atakayechakachua taarifa na ikathibitika hilo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa NBS inafuatilia taarifa kutoka Dodoma eneo la Kisasa kuwa kuna Karani amekwenda kwenye kaya lakini alikuwa haulizi maswali.


Wakati huo huo Kamishna wa Sensa Hajjat Amina alisema kuwa wale viongozi wengi waliokuwa wakiwa hamasisha wenzao wasihesabiwe , wamehesababiwa kwa hiari baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kuacha taarifa muhimu zilizohitajiwa ikiwemo zile zilihitajika katika madodoso. Kwa wale ambao hawakuwakuta waliweka alama maalum ili wawarudie mara ya pili.

Kumbe Pinda ujanja wote amefundishwa na huyu mzee?


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwalimu wake, John Kasalamimba wakati walipokutana Mjini Mpanda jana, Agust 30,2012.Mwalimu Kasalamimba alimfundisha Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1960 darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Kibaoni wilayani Mlele, Mpanda.
                                Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Dah Jembe langu hili limeshahamia Madrid... namkubali sana huyu mtu..... ndio ilikuwa engine ya Chelsea hii..


Mtaani kwetu, uwe tajiri uwe maskini. Ukiamka kitu cha kwanza unachofikiria ni namna gani uatapata maji...



Niseme tu ukweli wa moyo hawa watoto wa mitaani wananichafua roho yangu. Wilaya ya Ilala ipo wapi isiangaze jicho lake kwa watoto hawa? Hili ni eneo la Fire Kariakoo asubuhi hii.

 Tazama mtoto huyu ameegamia gari likiwa katika foleni, dereva akiondoa gari kwanguvu atasalika huyu?


 Tazama hawa, wote wawili ni watoto chini ya miaka kumi, lakini wamepewa mtoto mwenzao wambebe katikati ya barabara magari yanapita kwa nguvu. Hatari hii inafumbiwa macho tu...

Hawa ni wazazi wa watoto hawa, wamekaa upande wa pili wa barabara wanasubiri kuona watoto wao wamepewa chochote halafu wanazichukua pesa hizo. Hawakamatwi hawa wazazi namna hii kwa uzembe na uzururaji, ambao hawana ulemavu wa aina yoyote.

Soma habari ya mechi leo Coastal Vs Young African..

Nilichojifunza mchezo wa leo kati ya Coastal Union na Yanga uwanja wa taifa.

Ndugu zangu,

Siku zote husemwa mficha maradhi kifo kitamuumbua, leo nimeshuhudia timu yangu ya Coastal Union ikifungwa goli mbili moja na vijana wa jangwani. Hakuna mtu ambae alishuhudia mechi ile ya leo na kushindwa kuwamwagia sifa vijana wa Coastal.

Hakika walicheza kandanda ya kufurahisha sana na ya kutia hamasa sisi washabiki kutegemea mambo mengi mazuri kwa msimu ujao wa 2012/2013.

Kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya thamanini vijana wa Coastal walimiliki mpira, wakatoa pasi za uhakika na chenga zenye kuonekana kiasi mashabiki wa Yanga wakawa kimya kabisa. Hata goli lililofungwa kipindi cha kwanza cha mchezo na Razak Khalfan, lilikuwa la kiufundi na hata namna walivyoweza kuzuia mashambulizi ya Bahanuzi kila mtu alifurahi.

Hata kipindi cha pili kilipoanza bado uhai wa Coastal ulionekana hasa katika upande wa viungo na beki zote za kulia na kushoto ingawa kulikuwa na uhai mdogo katika safu ya umaliziaji lakini inaweza kurekebishika.

Tatizo lilikuwa kwa golikipa wa Coastal Juma Mpongo, bado anaonekana ana wasiwasi na anapangua sana kuliko kudaka mipira. Tatizo hili ni dogo ikiwa kocha wa magolikipa Bakari Shime, atafanya maamuzi ya haraka lakini litakuwa kubwa kama ataendelea namna hii katika ligi kuu.

Tuende katika mada ya msingi, upo upinzani mkubwa katika klabu ya coastal Union iliyo na makazi yake mjini Tanga barabara ya 11. mashabiki asilimia thamanini hawamtaki kocha, naam Juma Mgunda kocha mkuu wa timu hiyo hatakiwi hata kidogo na mashabiki wa wagosi wa kaya.

Na leo nimegundua makosa mengi ya kocha huyo, timu ilikuwa katika nafasi nzuri sana ya kushinda, lakini makosa madogomadogo yaliyotoa upenyo kwa Mbuyu Twite kupiga shuti na mchezaji wa coastal Jamal, kujifunga kwa kichwa wakati akijaribu kuokoa hatari hiyo; yaliwapumbaza wachezaji wa Coastal maana kwa dakika mbili walikosa nguvu hasa baada ya kujiona wapo pungufu baada ya mchezaji mwenzao Jerry Santo kupewa kadi nyekundu kwa kumtukana mwamuzi.

Lakini badala yake Kocha alitakiwa kusimama na kuwaambia wachezaji wasijali kujifunga ama timu pinzani kusawazisha ni moja ya mchezo. Lakini hakufanya hivyo bali aliendelea kukaa katika benchi la wachezaji wa akiba bila kusema lolote. Kazi kubwa alikuwa akifanya kocha msaidizi Habib Kondo, ambae alionekana kusimama muda wote wa mchezo.

Kocha wa timu pinzani hakika alionyesha uwepo wake, hakukaa hata kidogo mbali ya timu yake kuwa nyuma kwa goli moja na kuonekana kuelemewa lakini bado alikuwa akiwapigia kelele wachezaji wake na kuwaita kuzungumza nao kila alipopata nafasi. Hilo sikuliona kwa kocha wetu mchezaji wa zamani wa Coastal Union Juma Mgunda.

Hakujaharibika kitu, lakini ipo haja kukaliwa kikao kwa mashabiki wote nchi nzima kujadili suala hili. Maana nimesikia mashabiki wa Dar es Salaam wanamtaka kocha na mashabiki wa Tanga hawamtaki, kwakuwa mashabiki wa Tanga ndiwo wanaokaa na wachezaji kwa muda mwingi wanaweza kuwashawishi kwa maneno ama kuwarubuni wauze timu ili ionekane kocha hafai. Na hii ni mbaya sana kwa mustakabali wa klabu hasa ikizingatiwa tunaingia katika msimu mpya muda si mrefu.

Rai yangu ni kukaliwa kikao ambacho kitaamua nini cha kufanya maana nimesikia mpaka wiki iliyopita katika mechi ya kirafiki baina ya Polisi Dodoma na Coastal kocha alitaka kupigwa na mashabiki mpaka ikabidi kupewa ulinzi wa polisi.

Hatutafika popote kama tutaendelea na msuso huu, nimeshangaa sana timu imekuja kutoka Tanga bila viongozi wa juu wala kikundi cha ngoma ambacho mara nyingi hujitolea kuja kwa nauli zao….. Tafakari maneno haya mpenzi wa Coastal..

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
1/09/2012