Saturday, September 1, 2012

Niseme tu ukweli wa moyo hawa watoto wa mitaani wananichafua roho yangu. Wilaya ya Ilala ipo wapi isiangaze jicho lake kwa watoto hawa? Hili ni eneo la Fire Kariakoo asubuhi hii.

 Tazama mtoto huyu ameegamia gari likiwa katika foleni, dereva akiondoa gari kwanguvu atasalika huyu?


 Tazama hawa, wote wawili ni watoto chini ya miaka kumi, lakini wamepewa mtoto mwenzao wambebe katikati ya barabara magari yanapita kwa nguvu. Hatari hii inafumbiwa macho tu...

Hawa ni wazazi wa watoto hawa, wamekaa upande wa pili wa barabara wanasubiri kuona watoto wao wamepewa chochote halafu wanazichukua pesa hizo. Hawakamatwi hawa wazazi namna hii kwa uzembe na uzururaji, ambao hawana ulemavu wa aina yoyote.

No comments:

Post a Comment