Saturday, June 30, 2012
Haya sasa kama ulisoma Kinondoni Muslims toklezea leo.
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wanafunzi waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim (Reunion) zitakazofanyika Jumamosi Juni 30.
Mwenyekiti wa Reunion Bi. Mambo Tambaza alisema katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kutoka ianzishwe mwaka 1966, walimu waliowahi kufundisha shule hiyo na wanafunzi wanasoma watahudhuria.
Makamu Mwenyekiti wa Reunion, Bw. Aboubakar Liongo alisema maandalizi ya sherehe hiyo yamekamilika na sherehe hiyo itaanza saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Cine Club iliyopo Kawe, Dar es Salaam.
Alitoa wito kwa wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza ili kufahamiana na kuangalia uwezekano wa kuisaidia shule hiyo.
"Tumetoa taarifa kwa wanafunzi wote kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, ni matumaini yetu kuwa wengi watahudhuria" alisema Bw. Liongo.
Katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo na wanafunzi wanaosoma wataeleza hali ya kitaaluma katika shule hiyo na msaada wanaohitaji.
kwa hisani ya blogu ya Full shangwe.
Mpaka sasa Waislam hawajapata msimamo juu kushiriki ama kutoshiriki sensa ya mwaka huu. Kigezo kikiwa ni kutokuwepo kwa kipengele cha dini katika dodoso la sensa..... je una maoni? tupia hapo chini..
kuanzia kulia ni Sharif Hussein al Musawa mwenyekiti wa wanazuoni Tanzania, katikati ni Sheikh Mataka na mwisho ni Sheikh Iddy Simba waziri wa zamani wa viwanda na biashara.
Haya tena wanakijiji wenzangu mnaopenda kozi fupi: University of dodoma inatangaza kozi za muda mfupi kuongeza ujuzi na taaluma. ushindwe mwenyewe.
SHORT
COURSE ANNOUNCEMENT ON DATA PROCESSING AND ANALYSIS
|
|
|
|
University
of Dodoma College of Natural and Mathematical
Sciences
School
of Mathematical Sciences Department of Statistics
The
Department of Statistics, School
of Mathematical Sciences
is announcing a short course on “DATA
PROCESSING AND ANALYSIS” that
will be conducted on July 14 –
15, 2012.
Course
Description
This
short course training deals with processing and analysis of raw data collected
from the field. The training enables trainees to know key issues that should be
considered when plan for data processing and analysis. It provides better
insight into feasibility of the analysis to be performed as well as resources
required.
Objective
of the training
The objective of the
training is to improve skills of researchers into different statistical
techniques applied during data processing and analysis and hence practical
interpretation of the result.
Target
Group: Any
interested person.
Participation
Fee: Tshs 120, 000/=
(The amount paid will cover tuition fee, training materials, meals,
refreshments and certificate of attendance. Participants are required to come
with their laptops.
Mode
of payment: All
payments should be done through; Account Name: College of Natural
and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000 – CRDB.
Venue: University of Dodoma , School of Social Sciences (Master Class – MRL-3)
Deadline for
registration and payment: 6th July, 2012
Mode of
Registration: Send
SMS or email indicating your name after making payment using contact below.
Come with paying slip.
Contact: Short course
Coordinators, Department of Statistics, P. O. Box 338 , Dodoma ,
Mobiles: 0787288998 or 0717999012 or 0718453773; E-mail: mtakwimu@yahoo.com or abbasism2003@yahoo.co.uk
Training
Timetable
|
Time
|
Saturday:
July 14, 2012
|
Time
|
Sunday:
July 15, 2012
|
|
|
08:30 - 09:00
|
Registration
|
09:00 - 10:30
|
Session III:
Data Cleaning
|
|
|
09:00 – 09:40
|
Session I:
Overview of Data
|
10:30 - 11:00
|
Break
|
|
|
09:40 – 10:00
|
Break
|
11:00 - 13:00
|
Session III
resume
|
|
|
10:00 – 13:00
|
Session
II: Data management using SPSS
|
13:00 - 14:00
|
Lunch
|
|
|
13:00 - 14:00
|
Lunch
|
14:00 - 16:20
|
Session IV:
Descriptive Data Analysis
|
|
|
14:00 – 17:30
|
Session II:
Resume
|
16:20 - 16:30
|
Closure
|
|
|
|||||
|
|
|
|
|
|
NOTE:
- We invite requests from various interested groups to communicate with us for
the training
to be conducted in their respective places.
- Similar training is planned to be
conducted in Mwanza in August, 2012.
Dr Asha Rose Migiro aagwa rasmi na kupewa shavu jingine la mjumbe maalum wa masuala ya UKIMWI barani Afrika.
Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Naibu
Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro kuwa mjumbe wake
maalum katika masuala yaukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika.
Ban Ki Moon
ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla maalum aliyoiandaa mahsusi kwaajili ya
kumuaga Naibu Katibu Mkuu wake ambaye anahitimisha utumishi wa miaka mitano na nusu katika nafasi yake.
Hafla hiyo imefanyika siku ya alhamisi katika viunga
vya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali
wakiwamo mabalozi na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Ninatangaza
rasmi kwamba ninamteua Dk. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wangu
maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika," alisema Ban
Ki Moon huku akishangiliwa kwa nguvu na wageni
waalikwa.
Akiongea kwa hisia, Ban Ki Moon, ameeleza kwamba ingawa Migiro
alikuwa naibu wake, lakini amekuwa mwalimu kwake kwani amejifunza mengi kwa kipindi alichokaa nae na daima ataendelea kuenzi mchango wake mkubwa.
“ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha
sana, kwa ufupi siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana
kwangu, ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira
magumu na ya hatari, kote ameniwakilisha vema sana, kama mwalimu
wangu, ni kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” akasema Ban Ki
Moon na kushangiliwa.
Akamuelezea Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini
mwanadiplomasia aliyebobea aliyefanya kazi kubwa ngumu na nzito kwa moyo
mkunjufu, uhodari, umakini na uadilifu wa hali ya juu sana.
“ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna
gani alivyochapa kazi kwa nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya
na kuyakamilisha kwa uadilifu wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia
aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda
yake” akabainisha Ban Ki Moon.
Akaongeza “Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu, akiwamo aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Quadaff aliyethubutu hata
kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa amezikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo
watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali. Migiro unaondoka, lakini
Umoja wa Mataifa hautasahau mchango wako. Hapa ni nyumbani kwako, na
nitaendelea kuomba msaada wako na ushirikiano wako, bado nitaendelea
kukuhitaji” akasisitiza Ban Ki Moon.
nae Dk Migiro alimshukuru kiongozi huyo wa umoja wa mataifa na kuita uteuzi wake ni wa heshima na suala la UKIMWI lipo moyoni mwake atalitumikia kwa uwezo wake wote.
"Masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi,
ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba nashukuru kuona kwamba Katibu
Mkuu ameniamini kwamba naweza kumsaidia, naahidi nitalitekeleza
jukumu hilo
kwa heshima kubwa".
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na familia ya Naibu Katibu Mkuu
ikijumuisha mume wake, Profesa Cleophas Migiro, mdogo
wa Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Mtengeti na mtoto wa mwisho
wa Migiro Chansa Jasmin.
Asha-Rose Migiro
anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini
pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu
katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
Jacob Zuma To Buy Presidential Jet Worth 150mil Pound Despite South Africa's Poverty'
Jacob Zuma is in talks
to buy a £165m presidential jet, it was reported, just days after the South
African president warned of growing frustration among the country's poorest
over the government's failure to improve their lives.
The customised Boeing 777 plane seats 300 people and would cost $150m to buy and an additional $80m to be adapted to Mr Zuma's specifications.
The Department of
Defence, which oversees VIP transport, is reportedly considering spending an
additional $28m on a second private plane for Kgalema Motlanthe, the deputy
president.
Defence Secretary Sam
Makhudu Guluybe was on Friday visiting the United States to finalise the sale
with Boeing, according to the Johannesburg Star newspaper.
The newspaper said it
had documents which showed the defence department had negotiated a significant
reduction on the jet's original price of $305m after a deal between Boeing and
another buyer fell through.
The current presidential
jet, known as Inkwazi which means "fish eagle" in Mr Zuma's mother
tongue Zulu, was out of service for much of last year for upgrades and
maintenance.
Mpambanaji Ananilea Nkya atoa msimamo wake juu ya mgomo wa madaktari
Katika nchi yeyote
duniani serikali ndiyo yenye jukumu la kuweka mazingira mazuri
katika hospitali za umma na kuhakikisha kuwa madaktari na wafanyakazi wa
afya wanafanya kazi yao ya kutibu wagonjwa kwa furaha .
Hii ni kwa sababu serikali iliyowekwa madarakani na wananchi moja ya kazi ya kodi inayokusanya kutoka kwa wananchi ni kuhakikisha kuwa hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma ziko katika mazingira mazuri na zinatoa huduma nzuri kwa wananchi.
Mazingira mazuri hospitalini ni pamoja na kuwepo kwa vitanda vya kutosha kwa wagonjwa, madawa ya kutosha na ya viwango bora, vifaa kwa ajili ya kupima na kubaini magonjwa na vifaa na vyumba maalum vya kusaidia watu wanaofanyiwa upasuaji wasipoteze maisha.
Lakini hali ya hosipitali zetu za umma ni hairidhishi. Kwa mfano hospitali ya taifa ya Rufaa Muhimbili ni hospitali madaktari wanalalamika kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya madaktari kushindwa kutimiza wajibu wao wa kuokoa maisha ya wagonjwa.
Kwa mfano hospitali hiyo ina mashine ya MRI ya kupima na kutambua ugonjwa mbali mbali kwenye mwili ikiwa ni pamoja na kwenye ubongo, uti wa mgongo na kifua.
Lakini cha kushangaza mashine hiyo iliyonunuliwa kwa shilingi zisizopungua Bilioni mbili miaka michache iliyopita, inapungukiwa kifaa cha bei ndogo tu cha kuwezesha watoto kupimwa.
Hivyo watoto wenye matatizo yanayohitaji kupimwa kwa mashine hiyo wanalazimika kupelekwa India au Afrika ya Kusini kwa wale wenye uwezo wa kujigharamia vinginevyo kwa maskini walio wengi huishia watoto wenye matatizo makubwa yanayoitaji utambuzi wa mashine hiyo, huishia kufa.
Aidha madaktari wanalalamika jinsi wanavyoshindwa kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na tatizo la koromeo la chakula kuungana na koromeo la hewa. Mabingwa wa upasuaji wa watoto katika hospitali hiyo wanasema kwa upande wao wanajitahidi kuwafanyia watoto hao upasuaji, lakini watoto hao huishia hufariki dunia kutokana na hospitali hiyo ya Rufaa kukosa vifaa maalum vya kuhudumia watoto hao na vyumba maalumu vya kuwaweka baada ya kufanyiwa operasheni.
“Kinauma sana na kinakatisha tamaa sana kuona kwamba mtoto anafanyiwa upasuaji vizuri lakini anapoteza maisha siku chache baadaye kutokana na kukosekana kwa vifaa na mazingira ya kumwezesha kupona baada ya upasuaji”, anasema Dakta Catherine Mungo’ngo, Bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Rufaa ya Taifa.
Kwa mujibu wa bingwa huyo kwa mwaka huu pekee watoto watatu waliozaliwa na tatizo la la koromeo la chakula kuungana na koromeo la hewa ambao walifanyiwa upasuaji Muhimbili, baadaye walikufa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwasaidia kupumulia na chumba maalumu cha kuwafanyia uangalizi baada ya upasuaji.
Aidha anasema watoto kati ya 6 hadi 8 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku, upasuaji huo huahirishwa kutokana na ukosefu wa vifaa , dawa na chumba maalum cha kuwatunzia baada ya upasuaji.
Ni mtu gani mwenye akili timamu ambaye atafurahia kuona kazi anayoifanya haitoi matunda yanayotarajiwa.? Ni Daktari gani atakayeendelea kufurajhia kazi yake wakati lengo lake la kuokoa maisha ya watu linakwamishwa na mambo yanayowezekana kurekebishwa?
Daktari furaha yake ni kutibu mgonjwa na kuona anapona. Lakini Daktari katika hospitali za serikali atafanyaje kazi yake kuepusha vifo visivyo vya lazimakama hana vifaa
vya kufanyia kazi ?
Nionavyo mimi, serikali yetu inapaswa kutafakari tena kwa utulivu na busara kubwa na kuweka mikakati ya kupata suluhisho la kudumu la mgogoro wake na madaktari.
Vinginevyo hata kama wataagizwa madaktari kutoka Ulaya, na wa hapa nchini kufukuzwa kazi au hata kama viongozi wao ‘watashughulikiwa’, tatizo la mazingira ya kazi hospitalini ambalo ni moja ya mambo ya msingi linalosababisha mgomo wa madaktari litakuwa halijashughulikiwa na litaendelea kujirudia hata kama litapoozwa kwa mbinu yoyote ile.
Na ikumbukwe watakaoendelea kuumia zaidi hapa ni wananchi wengi ambao maishayao yanategemea uwajibikaji wa
serikali yao .
Nijuavyo mimi, serikali ya wananchi, madaktari wakiwa ni sehemu ya wananchi, husikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia badala ya kutumia mabavu na vitisho. Mungu ibarikiTanzania .
Ananilea NkyaHii ni kwa sababu serikali iliyowekwa madarakani na wananchi moja ya kazi ya kodi inayokusanya kutoka kwa wananchi ni kuhakikisha kuwa hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma ziko katika mazingira mazuri na zinatoa huduma nzuri kwa wananchi.
Mazingira mazuri hospitalini ni pamoja na kuwepo kwa vitanda vya kutosha kwa wagonjwa, madawa ya kutosha na ya viwango bora, vifaa kwa ajili ya kupima na kubaini magonjwa na vifaa na vyumba maalum vya kusaidia watu wanaofanyiwa upasuaji wasipoteze maisha.
Lakini hali ya hosipitali zetu za umma ni hairidhishi. Kwa mfano hospitali ya taifa ya Rufaa Muhimbili ni hospitali madaktari wanalalamika kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya madaktari kushindwa kutimiza wajibu wao wa kuokoa maisha ya wagonjwa.
Kwa mfano hospitali hiyo ina mashine ya MRI ya kupima na kutambua ugonjwa mbali mbali kwenye mwili ikiwa ni pamoja na kwenye ubongo, uti wa mgongo na kifua.
Lakini cha kushangaza mashine hiyo iliyonunuliwa kwa shilingi zisizopungua Bilioni mbili miaka michache iliyopita, inapungukiwa kifaa cha bei ndogo tu cha kuwezesha watoto kupimwa.
Hivyo watoto wenye matatizo yanayohitaji kupimwa kwa mashine hiyo wanalazimika kupelekwa India au Afrika ya Kusini kwa wale wenye uwezo wa kujigharamia vinginevyo kwa maskini walio wengi huishia watoto wenye matatizo makubwa yanayoitaji utambuzi wa mashine hiyo, huishia kufa.
Aidha madaktari wanalalamika jinsi wanavyoshindwa kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na tatizo la koromeo la chakula kuungana na koromeo la hewa. Mabingwa wa upasuaji wa watoto katika hospitali hiyo wanasema kwa upande wao wanajitahidi kuwafanyia watoto hao upasuaji, lakini watoto hao huishia hufariki dunia kutokana na hospitali hiyo ya Rufaa kukosa vifaa maalum vya kuhudumia watoto hao na vyumba maalumu vya kuwaweka baada ya kufanyiwa operasheni.
“Kinauma sana na kinakatisha tamaa sana kuona kwamba mtoto anafanyiwa upasuaji vizuri lakini anapoteza maisha siku chache baadaye kutokana na kukosekana kwa vifaa na mazingira ya kumwezesha kupona baada ya upasuaji”, anasema Dakta Catherine Mungo’ngo, Bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Rufaa ya Taifa.
Kwa mujibu wa bingwa huyo kwa mwaka huu pekee watoto watatu waliozaliwa na tatizo la la koromeo la chakula kuungana na koromeo la hewa ambao walifanyiwa upasuaji Muhimbili, baadaye walikufa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwasaidia kupumulia na chumba maalumu cha kuwafanyia uangalizi baada ya upasuaji.
Aidha anasema watoto kati ya 6 hadi 8 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku, upasuaji huo huahirishwa kutokana na ukosefu wa vifaa , dawa na chumba maalum cha kuwatunzia baada ya upasuaji.
Ni mtu gani mwenye akili timamu ambaye atafurahia kuona kazi anayoifanya haitoi matunda yanayotarajiwa.? Ni Daktari gani atakayeendelea kufurajhia kazi yake wakati lengo lake la kuokoa maisha ya watu linakwamishwa na mambo yanayowezekana kurekebishwa?
Daktari furaha yake ni kutibu mgonjwa na kuona anapona. Lakini Daktari katika hospitali za serikali atafanyaje kazi yake kuepusha vifo visivyo vya lazima
Nionavyo mimi, serikali yetu inapaswa kutafakari tena kwa utulivu na busara kubwa na kuweka mikakati ya kupata suluhisho la kudumu la mgogoro wake na madaktari.
Vinginevyo hata kama wataagizwa madaktari kutoka Ulaya, na wa hapa nchini kufukuzwa kazi au hata kama viongozi wao ‘watashughulikiwa’, tatizo la mazingira ya kazi hospitalini ambalo ni moja ya mambo ya msingi linalosababisha mgomo wa madaktari litakuwa halijashughulikiwa na litaendelea kujirudia hata kama litapoozwa kwa mbinu yoyote ile.
Na ikumbukwe watakaoendelea kuumia zaidi hapa ni wananchi wengi ambao maisha
Nijuavyo mimi, serikali ya wananchi, madaktari wakiwa ni sehemu ya wananchi, husikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia badala ya kutumia mabavu na vitisho. Mungu ibariki
Executive Director
Tanzania Media Women's Association (TAMWA)
P. O. Box 8981, Sinza-Mori
Dar es Salaam, TANZANIA
Tel: +255-22 2772681 Fax +255 22 2772681 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
Cellphone:+255-754-464-368
Madaktari bingwa watoa tamko
Mkutano wa Madaktari bingwa jana MNH, MUHAS NA ORCI umeamua kuungana rasmi na madaktari wote nchini katika mgomo na kusitisha
utoaji wa huduma zote zikiwemo za dharura Pia wanatoa wito kwa madaktari bingwa wengine kote nchini kuungana katika mgomo huu.
Pia wanalaani vikali vitisho na manyanyaso yanayofanywa na vyombo vya dola (serikali) dhidi ya madaktari na wameitaka serikali kutoa tamko la kuwahakikishia usalama madaktari kote nchini.
Pia kuna haja ya kuweka uwezekano wa kumsafirisha Dr. Ulimboka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi; hivyo zinahitajika $40,000(sawa na takribani tsh milioni sitini na nane 68000000),mpaka sasa madaktari wamechangisha Tsh mil 40..
Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 054.
Pia wanalaani vikali vitisho na manyanyaso yanayofanywa na vyombo vya dola (serikali) dhidi ya madaktari na wameitaka serikali kutoa tamko la kuwahakikishia usalama madaktari kote nchini.
Pia kuna haja ya kuweka uwezekano wa kumsafirisha Dr. Ulimboka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi; hivyo zinahitajika $40,000(sawa na takribani tsh milioni sitini na nane 68000000),mpaka sasa madaktari wamechangisha Tsh mil 40..
Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 054.
UKIMWI unazidi kupata dawa....mhh
Huenda wagonjwa wa
Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa
siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida la Afya Lancet
limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya
ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika
kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini
watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na
kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili
kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa
majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV
kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum
katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston ,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo
wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa
kuimarisha afya ya wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza
utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na
kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya
sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi
na maambukizi bila kujua.
Chanzo: bbc swahili. http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Tamko la Jumuiya ya Madaktari
MWENYEKITI wa Jumuiya ya
Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya usiku wa kumkia juzi, kisha
kutupwa Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote
yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili.
Dk Ulimboka aliokotwa na
wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha akiwa katika Viwanja
vya Klabu ya Leaders, Kinondoni.
Jana, Dk Ulimboka ambaye
amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili huku hali yake ikiwa haijatengemaa vyema,
alitoa kauli akisema ingawa ana maumivu makali anaendelea vizuri ikilinganishwa
na siku ya kwanza.
Dk Ulimboka alitoa kauli
hiyo baada ya kutakiwa aeleze mkasa huo uliomfika wa kukamatwa, kuteswa na
kutupwa msituni.
Hata hivyo, hadi sasa
wingu zito la nani alimteka na watekaji walitaka kujua nini kutoka kwa kiongozi
huyo wa madaktari, bado limetanda.
Siri nzito
Akisimulia mkasa huo
kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema, akiwa katika klabu
hiyo ya Leaders alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alikuwa atokee Tandika na
baada ya kumsubiri ndipo alipofika kwenye klabu hiyo, lakini, alianza kujisikia
vibaya tofauti na siku nyingine na kuongeza; "Yaani sikuwa na amani."
Alisema, "Mara,
katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema
tuagane, wakaja watu kama watano hivi na
bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk
Ulimboka)," alieleza na kuongeza:
"Sijakaa sawa,
nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye
gari nyeusi, lakini halikuwa na namba."
Hata hivyo, jana Dk
Ulimboka hakuonana na mwandishi wa habari hii, badala yake alirekodiwa, na
Mwananchi kupata sauti yake akijibu swali kuhusu hali yake na tukio hilo , baada ya uongozi wa
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kuzuia watu kumwona.
Daktari huyo wa magonjwa
ya binadamu, amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu
(ICU).
"Kidogo najisikia
nafuu ikilinganishwa na nilivyokuja ingawaje, bado nina maumivu makali. Kwa
hivyo, ingependeza niendelee na mapumziko na mtu yeyote anayetaka kuniona
pengine hilo
jambo lisifanyike sasa. Hivi sasa ni vizuri nipumzike," ilisikika sauti
hiyo ya Dk Ulimboka.
Lakini, uchunguzi wa
gazeti hili umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa
madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka
aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo.
Madaktari wanaolinda
eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu
tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi
wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao.
Kiongozi jopo la
madaktari
Katika hatua nyingine,
kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph
Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili
mzima.
“Ingawa kwa sasa
anaendelea vizuri, Dk Ulimboka ameumia sana ,
kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji
hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza:
“Aliumia
mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole
na kichwani na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema.
Alifafanua kwamba,
kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa
ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za
kuokoa maisha yake.
Uongozi wa Moi watoa
neno
Uongozi wa Taasisi ya
Mifupa (Moi) umeeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa
katika chumba cha wagonjwa mahututi cha taasisi hiyo.
Msemaji wa Moi, Almas
Jumaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya hali yake kuendelea vizuri,
lakini haingewezekana kwa waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba
alikolazwa na kumwona Dk Ulimboka.
“Mgonjwa anaendelea
vizuri ukilinganisha na jana (juzi), anaongea, anawatambua watu wanaokwenda
kumwona, lakini utaratibu wa kwenda kumwona kwa ninyi imeshindikana kwa sababu
yupo (ICU) ni chumba chenye utaratibu wake,”alisema Jumaa.
Jumaa aliongeza kwamba
ili mtu aweze kuingia wodini analazimika kuvaa vazi maalumu na mavazi yaliyopo,
yasingetosha, lakini pia wapo watu wanaoendelea kumpatia huduma ya matibabu.
chanzo cha habari: mjengwa.blogspot.com
Friday, June 29, 2012
tigo imewakumbuka wateja wake coco beach kesho
Na Hafidh Kido
Tigo imejipanga kuwapa burudani
wakaazi wa jiji la Dar es Salaam siku ya jumamosi na jumapili mwishoni mwa wiki
hii katika fukwe za coco beach. Lengo likiwa ni kuwaandaa watumiaji wa tigo na
sikukuu ya sabasaba.
Akizungumza na wanahabari katika
hoteli ya serena leo asubuhi afisa habari wa kampuni hiyo ya mawasiliano bi
Alice Maro, amesema kampuni yake imeamua kuwapa burudani nyingi watumiaji wa
mtandao huo lengo likiwa ni kuwa nao karibu na kufahamiana zaidi.
“Mwaka huu tumeamua kuwaletea
burudani nyingi za kutosha, hatutotaka wateja wetu waje tu kufurahi mwisho wa
wiki hii ila tungependa pia wapate fursa ya kupata huduma zetu bora na nafuu
zilizoandaliwa kwa ajili yao .”
Aidha tigo katika kunogesha
shughuli hiyo waeamua kuonyesha fainali za mpira wa miguu za ulaya kati ya Italy na
Hispania siku ya jumapili, sherehe hizo zitasindikizwa na wasanii maarufu
watakaokonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hasa pale wasanii
mahasimu Izzo B pamoja na Roma Mkatoliki watakapopanda jukwaa moja siku hiyo.
“Kilele cha maadhimisho hayo
kitakuwa ni siku ya jumapili na burudani kutoka kwa Juma nature, Roma
mkatoliki, izzo B, Professor J, Mwasiti, Barnabas, Fid Q, Joe Makini na
burudani maalum kutoka kundi la vichekesho la “Ze Comedy,” alisema Alice.
Tigo ni mtandao wa kwanza wa
simu za mkononi Tanzania ulioanza biashara mwaka 1994, na ni mtandao wenye
ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma katika
mokoa yote 26 Tanzania bara na visiwani. Ingawa katika siku za hivi karibuni
kumekuwepo na malalamiko ya mitambo ya mtandao huo kutokuwa mizuri wakati wa
mawasiliano.
Thursday, June 28, 2012
Tusikilize majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu leo kwa faida yetu.
Mwanakijiji mwenzangu, leo jiandae kusikiliza majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu Mizengo Pinda. Kuna mengi yanategemewa kutoka katika kauli ya serikali, watu wana matumaini makubwa kwa huyu mtoto wa mkulima anaweza kuwasaidia katika kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.
Hasa katika suala la mashangingi (magari ya gharama) na mambo mengi ambayo hayana umuhimu katika ofisi za serikali. Kumbuka ofisi ya waziri mkuu ndiyo inayoshikilia asilimia kubwa ya mhimili wa kwanza wa dola, yaani Serikali. Kwani viongozi wengi wanawajibika chini yake kuanzia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa, wenyeviti serikali za mitaa, madiwani na wakurugenzi wa mikoa na wilaya, listi ni ndefu.
Na huko kuna uzembe mwingi unafanyika hasa kwa kudhani wananchi hawana uelewa wa namna ya kuwawajibisha viongozi hao. Juzi mbunge mpya na kijana Joshua Nassari kutoka Arumeru Mashariki aliongea kitu watu wakaona ni cha kijinga. Alihoji ni kwanini wakuu wa mikoa na wilaya wamejazana bungeni kusikiliza bajeti ya ofisi ya waziri mkuu wakati wananchi wapo mikoani wana shida na uwepo wao.
Kwanini wasifuatilie bunge wakiwa ofisini badala yake watumie magari ya serikali,mafuta, malazi na chakula kukaa bungeni tu bila ya shughuli yoyote?
naomba kuwasilisha, Kido Jembeeeeeeeeeeeeeeee.
Hasa katika suala la mashangingi (magari ya gharama) na mambo mengi ambayo hayana umuhimu katika ofisi za serikali. Kumbuka ofisi ya waziri mkuu ndiyo inayoshikilia asilimia kubwa ya mhimili wa kwanza wa dola, yaani Serikali. Kwani viongozi wengi wanawajibika chini yake kuanzia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa, wenyeviti serikali za mitaa, madiwani na wakurugenzi wa mikoa na wilaya, listi ni ndefu.
Na huko kuna uzembe mwingi unafanyika hasa kwa kudhani wananchi hawana uelewa wa namna ya kuwawajibisha viongozi hao. Juzi mbunge mpya na kijana Joshua Nassari kutoka Arumeru Mashariki aliongea kitu watu wakaona ni cha kijinga. Alihoji ni kwanini wakuu wa mikoa na wilaya wamejazana bungeni kusikiliza bajeti ya ofisi ya waziri mkuu wakati wananchi wapo mikoani wana shida na uwepo wao.
Kwanini wasifuatilie bunge wakiwa ofisini badala yake watumie magari ya serikali,mafuta, malazi na chakula kukaa bungeni tu bila ya shughuli yoyote?
naomba kuwasilisha, Kido Jembeeeeeeeeeeeeeeee.
jokes corner
As a family of 5 was having supper, the youngest son asked his father, "What is the difference between IMAGINATION & REALITY?"(father turns and asks mother, "Would you have sex with Mr. Kamau for 1million sh?" Mother:YES why not? (father turns and asks daughter)"Would you have sex with Rudisha for 1m? Daughter; why not? (father then asks elder son) Son would you have sex with Edward for 1m sh? Son; why not. Father: You see my son, we imagine we have 3millionares but reality is we are leaving with two prostitutes and 1 gay.
Tathmini yangu mkutano wa Chadema Dar es Salaam.
wiki kadhaa chama cha demokrasia na
maendeleo CHADEMA,kimefanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya jangwani
jijini Dar es Salaam .
Wametega siku muhimu kwa kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Dar es Salaam walikuwa wakifuatilia mwenendo
wa kesi ya mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika (chadema). Ambae alishitakiwa
na mama Hawa Ng’umbi ambae alikuwa mgombea wa kiti hicho pia kupitia CCM.
Lakini mnyika akashinda kesi hiyo.
Nimegundua kwa muda mrefu
CHADEMA wanaumezea mate mji huu, kwani ni kambi ya ccm na cuf. Hilohalihitaji
mjadala. Nimegundua bado idadi kubwa ya wakaazi wa jiji hili wana mapenzi na ccm
ama cuf, chadema bado kidogo, idadi ya watu niliyoiona leo ni kubwa ila
haifikii ccm wala cuf pindi wanapofanya mikutano yao Dar es salaam.
Hotuba aliyoitoa Mnyika,
mbunge wa Ubungo inaonyesha wazi dhamira ya chadema kutaka kuliteka jiji, pale
alipowahamasisha wana jiji kujiunga na vuguvugu la mabadiliko (movement for
change) linaloendeshwa na chama hicho kwani hata kipindi cha kudai uhuru wazee
na vijana wa jiji hili ndiwo waliokuwa mstari wa mbele.
Mwenyekiti Freeman Mbowe,
katibu mkuu Dr Slaa na mtaalamu wa sheria wa chadema Tundu Lissu, hawakuongea
vitu vipya kama nilivyotegemea zaidi ya kuwahamasisha watanzania kuiangalia
katiba hasa katika vipengele viwili vya mamlaka ya Rais na uhalali wa muungano
baina ya Zanzibar na Tanganyika .
Ugumu wa maisha imeonekana ni
mada anazozipenda katibu mkuu wa chadema Dr Slaa, kwani amekuwa akirudia maneno
hayo kila anapopata nafasi ya kuzungumza na watanzania.
Ibaki tu kuwa lengo la
mkutano wa leo uliopewa kauli mbiu ya ‘VUA GAMBA VAA GWANDA’ ni mkakati wa chadema
kuuteka mji huu na kuwa miongoni mwa ngome zao na kufuta ile dhana ya
ukaskazini. Yaani wanapendwa zaidi mikoa ya kaskazini.
Siku hiyo ya mkutano asubuhi nilikuwa
nikilumbana kwa hoja na katibu wa itikadi na uenezi ccm ndugu Nape Nnauye
katika ukurasa wake wa facebook, nilikuwa nikimwambia ajiangalie sana na chama chake kwani
chadema watawaadhirisha. Watu wanajivua magamba na kuvaa magwanda kwa idadi
kubwa. Akanijibu kumbe ninajua kuwa magamba ndiyo yanayokwenda chadema basi
hawana maana.nikamjibu Kiswahili kinamsumbua?
Kwani waliposema wana-ccm
walioshindwa wajivue magamba, maana yake wakishajivua magamba wanayaacha ccm
hayomagamba na kuwa wasafi. Na chadema kinachukua wana-ccm waliojivua magamba.
Hivyo kwa tafsiri ya harakaharaka waliobaki ccm ndiwo magamba.
Naomba kuwasilisha.
Wabunge wakiukana ubunge wao nami nitaukana utanzania wangu
Na Hafidh kido
Siku zinazidi kusonga bunge la
bajeti linakaribia kuisha, ni kikao ambacho watu tuliowapa dhamana kutuwakilisha
kwa serikali wanajadili mustakabali wetu kiuchumi.
Lakini kuna jambo moja ambalo mpaka
sasa ufumbuzi wake una utata, suala la posho za vikao.
Siku spika wa bunge mama Anne
Makinda, alizungumza na wapiga kura wake wa Njombe kusini, mjini Iringa kuhusu
suala la wabunge kutaka kuachia ubunge kutokana na umaskini, ilinidhihirikia
kuwa mama yule anafanya kila namna kuiweka pembeni hoja ya wabunge vijana juu
ya ubadhirifu wa pesa za umma kwa kulundikiana mafungu yasiyo na tija.
Swali moja lingetosha kumuumbua mama
Makinda, je katika kikao gani nusu ya wabunge ambao ni takriban wabunge 150
katika idadi ya wabunge zaidi ya 300 walipata kumwelezea kadhia hiyo ya
kuandamwa na ufukara kutokana na wao kuchagua kuwa wabunge?
Sawa tuseme alizungumza maoni ya
jumla baada ya kupata malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa vijana wake, lakini
kwa namna alivyokuwa akiongea katika luninga siku ile ni wazi yeye alivaa joho
la uwakilishi wa ufukara unaowaandama wabunge. Hata kufikia kusema kwa miaka
yote aliyokuwa mbunge hajafanikiwa kujenga hata nyumba yake mwenyewe, anajidai
kumuiga Nyerere.
Hakuonekana kusikitishwa na kauli
hizo bali alitaka kuonekana shujaa kwa wabunge walafi wasiokuwa na shukurani
wala huruma kwa wananchi maskini wasiojua watakula nini wala watapata wapi
nauli ya kufika kibaruani ili wakamenyeke kwa ajili ya mlo wa siku moja ‘kesho
ina Mungu.’
Spika Makinda kwa madaha kabisa
aliwaambia wananchi wa jimbo lake ambao wengi ni maskini kuwa hivi sasa nusu ya wabunge
wa bunge la Tanzania
wanataka kuacha ubunge kutokana na kulipwa malipo madogo.
Hakuishia hapo bali aliendelea kusema
kwa miaka ijayo wabunge wenye taaluma zao hawatagombea tena ubunge ikiwa malipo
yataendelea kuwa hivi kwasababu ubunge ni eneo la umaskini wa kutupwa kabisa.
Angalia kituko hiki, mama huyo
mwenye heshima zake anaongea maneno hayo mbele ya wananchi ambao nusu yake
hawana ajira, na wenye ajira wanalipwa mishahara isiyozidi laki nne kwa mwezi
bila ya marupurupu ya chakula, usafiri wala nyumba. Halafu anawatetea wabunge
ambao wanalipwa mishahara ya shilingi milioni mbili na nusu kwa mwezi, pesa ya
mafuta ya gari, wanalipwa posho ya shilingi 80,000/= kwa kikao, wakiwa Dodoma wanalipwa posho ya
kujikimu shilingi 70,000/= kwa siku.
Kwa mwaka tuseme vikao vyote vya
bajeti viwe ni miezi mitano, yaani tukiviunganisha kwa pamoja. Na vikao vingine
vya kawaida vikiunganishwa vyote viwe ni miezi miwili, maana yake kwa mwaka
wanakutana kwa miezi saba mfululizo (tukiunganisha) ambapo katika kipindi hicho
cha miezi saba kwa siku mbunge akienda Dodoma akihudhuria kikao au asihudhurie
ana shilingi 80,000/= kibindoni ya kujikimu, akihudhuria analipwa shilingi
70,000/= ya kikao maana yake anapata shilingi 350,000/= kwa siku tano za vikao
tu, posho za kujikimu zinalipwa wiki nzima ambazo ni shilingi 560,000/=,
ukijumlisha malipo ya wiki tu ni shilingi 910,000/= Kwa mwezi ni zaidi ya
shilingi milioni tatu na laki sita mara miezi saba ni zaidi ya milioni ishirini
na tano.
Kumbuka hiyo ni posho ya vikao tu
sijaingiza posho ya mafuta, kadhalika sijaingiza mfuko wa jimbo, kadhalika
sijaingiza wale wabunge ambao wapo katika kamati za bunge ambao nao wana vikao
vyao vya kikamati, posho za safari na mambo mengine pale inapohitajika,
kadhalika sijaingiza mishahara ambayo kwa mwaka ni milioni thalathini. Halafu
unatuambia ubunge ni dimbwi la ufukara, tukuelewe vipi?
Fikiria mtanzania ambae analipwa
laki na nusu kwa mwezi hakuna posho wala safari zitakazomfanya awe na kipato
kingine. Anafanya kazi kuanzia asubuhi na mapema mpaka jioni giza linapoingia. Mtu huyu ukiunganisha
mshahara wake wa laki na nusu kwa mwaka ni milioni moja na laki nane, pesa
ambayo mbunge anaipata kwa wiki mbili tu.
Sijakataa mbunge kuacha shughuli
ambayo anadhani itamtia umaskini, sasa hawa ambao tayari ni maskini je wafanye
nini?
Ndipo nikasema ikiwa wabunge
watakana dhamana tulizowapa wakatutetee ili kwa pamoja tuondokane katika dimbwi
la ufukara matokeo yake wanataka kuwa matajiri peke yao, basi na sisi kwakuwa
tayari tu maskini itabidi tuukane utanzania wetu ili tukimbilie ulaya kama
wakimbizi wa kisomali, Kinyarwanda ama warundi ili tupokewe tupewa hifadhi
katika mataifa tajiri nasi tuwe na nafuu ya maisha kama ambavyo watanzania
wengi huishi hivyo nchini uingereza, ubelgiji, na nchi nyingi za bara la
Amerika na Australia. Wenyewe wanaita kujilipua.
Swali moja kwa mama Makinda, hivi
hao wabunge anaosema wana taaluma zao ni kitu gani kilichowafanya waache
kulitumikia taifa lao kulingana na taaluma walizonazo kama
uanasheria, uinjinia, udaktari, ualimu ama uhasibu na badala yake wakakimbilia
bungeni ambako hakuna maana yoyote?
Hakuna kitu kibaya katika maisha ya
msomi kama kushindwa kuchagua, tamaa ni maradhi mabaya sana katika taifa changa linalohitaji
uzalendo na kujitolea kwingi kwa faida ya wote.
Najua nitaonekana kichaa ama sijui
ninachozungumza, mara nyingine maelezo ya wabunge yanaweza kuwa na mantiki kwa
namna moja ama nyingine. Kitendo cha kuwajaza mapesa wabunge ndicho kinachowapa
kiburi na kutaka zaidi, siku zote anaepata kingi haridhiki lakini anaepata
kidogo hujifunza kuweka ili kimfae baadae.
Kwa mfano kipindi cha awamu ya
kwanza ubunge ulikuwa ni kazi ya hiyari, wala watu hawakutumia mapesa mingi
kupata nafasi ya ubunge, tofauti na sasa ni biashara na ndiyo maana baada ya
wabunge kuona biashara inapunguza mvuto wanadai nyongeza ya kingi; wapo wazee
ambao walikuwa wabunge na mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza sijui
serikali ina mpango nao gani, lakini wanaishi maisha ya chini kabisa.
Hii inaonyesha wazi walikuwa
wakiwatumikia watanzania kwa moyo wote na si kutaka kujilimbikizia mali na kusahau
kilichowapeleka bungeni. Tazama watu wanazusha hoja binafsi kwa kununuliwa.
Tajiri mmoja tu anaweza kumnunua mbunge na kumwambia peleka hoja hii
ikajadiliwe, ikipita tu nakuandalia tumilioni kadhaa. Vitu hivi vipo tusikatae.
Maneno ya wazee waasisi wa nchi hii
hata siku moja hayawezi kuanguka, walisema kiongozi akiingia kwa rushwa hata
siku moja hatoweza kuongoza kwa ufanisi kwani itabidi aanze kuwaridhisha wale
waliompatia fedha kuingia madarakani.
Ubunge ni biashara na ndiyo maana
wanaanza kuona hasara, fikiria mtu anakwenda kukopa mamilioni ya fedha,
nyingine anakwenda kuomba kwa wafanyabiashara wakubwa ambao malipo yao ni kufuata kila
wanachokitaka pindi ukishika madaraka.
Na ndiyo maana baadhi ya ‘wabunge
maslahi’ wanaanza kuona hali ni ngumu, miaka mitano inakwisha hajarudisha hata
nusu ya alichopoteza, na bado hajamaliza madeni huku wale watu waliomfadhili
wanataka kulipwa fadhila kwa mambo ambayo kwa nafasi yake ya ubunge hawezi
kuyatimiza, hapo ndipo anapojuta na kuona ubunge ni mzigo.
Naamini mtu ambae ameingia bungeni
kwa njia safi na halali hata siku moja hawezi
kuwa na majuto, kwani kwa hali za watanzania malipo wanayoyapata wabunge ni
makubwa sana
hakuna mfanyakazi yeyote anaeweza kuyapata hata awe mkurugenzi.
Tafadhali rejea mchanganuo wa pesa
wanazopata wabunge wetu halafu linganisha na maisha ama pesa unazopata kwa
mwezi. Hata msomaji akiwa ni mkurugenzi wa shirika lolote ima la umma ama la
binafsi hawezi kufikia pesa anazopata mbunge.
Halafu leo wanakwenda kutuambia
kiasi wanachopata kinawatia umaskini.
Yaani sijapata kusikia upumbavu
namna hii tangu nimezaliwa, hivi hawa wabunge wetu wanatuonaje sisi watanzania.
Nauliza kwa nia njema tu wala si kwa kebehi, leo hii kila mtu anatamani kuishi
maisha anayoishi mbunge halafu wanakuja kutuambia ubunge unawatia ufukara
wanajua kweli fukara wa kitanzania anapata shilingi ngapi kwa siku?
Naishia hapa nisije kutukana bure.
Naomba kuwasilisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)