Thursday, June 28, 2012

Tathmini yangu mkutano wa Chadema Dar es Salaam.




wiki kadhaa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,kimefanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam. Wametega siku muhimu kwa kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Dar es Salaam walikuwa wakifuatilia mwenendo wa kesi ya mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika (chadema). Ambae alishitakiwa na mama Hawa Ng’umbi ambae alikuwa mgombea wa kiti hicho pia kupitia CCM. Lakini mnyika akashinda kesi hiyo.

Nimegundua kwa muda mrefu CHADEMA wanaumezea mate mji huu, kwani ni kambi ya ccm na cuf. Hilohalihitaji mjadala. Nimegundua bado idadi kubwa ya wakaazi wa jiji hili wana mapenzi na ccm ama cuf, chadema bado kidogo, idadi ya watu niliyoiona leo ni kubwa ila haifikii ccm wala cuf pindi wanapofanya mikutano yao Dar es salaam.

Hotuba aliyoitoa Mnyika, mbunge wa Ubungo inaonyesha wazi dhamira ya chadema kutaka kuliteka jiji, pale alipowahamasisha wana jiji kujiunga na vuguvugu la mabadiliko (movement for change) linaloendeshwa na chama hicho kwani hata kipindi cha kudai uhuru wazee na vijana wa jiji hili ndiwo waliokuwa mstari wa mbele.

Mwenyekiti Freeman Mbowe, katibu mkuu Dr Slaa na mtaalamu wa sheria wa chadema Tundu Lissu, hawakuongea vitu vipya kama nilivyotegemea zaidi ya kuwahamasisha watanzania kuiangalia katiba hasa katika vipengele viwili vya mamlaka ya Rais na uhalali wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.

Ugumu wa maisha imeonekana ni mada anazozipenda katibu mkuu wa chadema Dr Slaa, kwani amekuwa akirudia maneno hayo kila anapopata nafasi ya kuzungumza na watanzania.

Ibaki tu kuwa lengo la mkutano wa leo uliopewa kauli mbiu ya ‘VUA GAMBA VAA GWANDA’ ni mkakati wa chadema kuuteka mji huu na kuwa miongoni mwa ngome zao na kufuta ile dhana ya ukaskazini. Yaani wanapendwa zaidi mikoa ya kaskazini.

Siku hiyo ya mkutano asubuhi nilikuwa nikilumbana kwa hoja na katibu wa itikadi na uenezi ccm ndugu Nape Nnauye katika ukurasa wake wa facebook, nilikuwa nikimwambia ajiangalie sana na chama chake kwani chadema watawaadhirisha. Watu wanajivua magamba na kuvaa magwanda kwa idadi kubwa. Akanijibu kumbe ninajua kuwa magamba ndiyo yanayokwenda chadema basi hawana maana.nikamjibu Kiswahili kinamsumbua?

Kwani waliposema wana-ccm walioshindwa wajivue magamba, maana yake wakishajivua magamba wanayaacha ccm hayomagamba na kuwa wasafi. Na chadema kinachukua wana-ccm waliojivua magamba. Hivyo kwa tafsiri ya harakaharaka waliobaki ccm ndiwo magamba.

 Naomba kuwasilisha.

No comments:

Post a Comment