Hii ni blogu yangu mpya na tutaangazia mambo mengi ya kijamii, tegemea picha nyingi na taarifa za kutosha kutoka katika jamii. nitatumia elimu yangu na uzoefu wa miaka sita katika taaluma ya uandishi wa habari kuwawezesha kupata kile mnachostahili.
nimekuwa nikiandika mambo mengi na kutoa picha nyingi katika ukurasa wangu wa facebook, lakini nimeona ninabanwa na nafasi. hivyo nimeamua kuja huku ili nijimwagemwage. karibuni waungwana mkiniunga mkono nitashukuru sana na nikikosea nipo tayari kukosolewa. kawaida sipendi kusifiwa ila kupongezwa nafurahi. ahsante.
alaa unashangaa kwanini nimejiita jembe? ni kutikana na uwezo wa kifaa hicho kuchimbua, nami nimejipa lakabu hiyo ili kuonyesha uwezo wangu katika kutifua, kuchimba na kupalilia.... jembeeeeeeeeeee..
tupo pamoja mwana habariii!
ReplyDelete