Na Hafidh Kido
Tigo imejipanga kuwapa burudani
wakaazi wa jiji la Dar es Salaam siku ya jumamosi na jumapili mwishoni mwa wiki
hii katika fukwe za coco beach. Lengo likiwa ni kuwaandaa watumiaji wa tigo na
sikukuu ya sabasaba.
Akizungumza na wanahabari katika
hoteli ya serena leo asubuhi afisa habari wa kampuni hiyo ya mawasiliano bi
Alice Maro, amesema kampuni yake imeamua kuwapa burudani nyingi watumiaji wa
mtandao huo lengo likiwa ni kuwa nao karibu na kufahamiana zaidi.
“Mwaka huu tumeamua kuwaletea
burudani nyingi za kutosha, hatutotaka wateja wetu waje tu kufurahi mwisho wa
wiki hii ila tungependa pia wapate fursa ya kupata huduma zetu bora na nafuu
zilizoandaliwa kwa ajili yao .”
Aidha tigo katika kunogesha
shughuli hiyo waeamua kuonyesha fainali za mpira wa miguu za ulaya kati ya Italy na
Hispania siku ya jumapili, sherehe hizo zitasindikizwa na wasanii maarufu
watakaokonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hasa pale wasanii
mahasimu Izzo B pamoja na Roma Mkatoliki watakapopanda jukwaa moja siku hiyo.
“Kilele cha maadhimisho hayo
kitakuwa ni siku ya jumapili na burudani kutoka kwa Juma nature, Roma
mkatoliki, izzo B, Professor J, Mwasiti, Barnabas, Fid Q, Joe Makini na
burudani maalum kutoka kundi la vichekesho la “Ze Comedy,” alisema Alice.
Tigo ni mtandao wa kwanza wa
simu za mkononi Tanzania ulioanza biashara mwaka 1994, na ni mtandao wenye
ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma katika
mokoa yote 26 Tanzania bara na visiwani. Ingawa katika siku za hivi karibuni
kumekuwepo na malalamiko ya mitambo ya mtandao huo kutokuwa mizuri wakati wa
mawasiliano.
No comments:
Post a Comment