Thursday, June 28, 2012

Tusikilize majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu leo kwa faida yetu.

Mwanakijiji mwenzangu, leo jiandae kusikiliza majumuisho ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu Mizengo Pinda. Kuna mengi yanategemewa kutoka katika kauli ya serikali, watu wana matumaini makubwa kwa huyu mtoto wa mkulima anaweza kuwasaidia katika kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.

Hasa katika suala la mashangingi (magari ya gharama) na mambo mengi ambayo hayana umuhimu katika ofisi za serikali. Kumbuka ofisi ya waziri mkuu ndiyo inayoshikilia asilimia kubwa ya mhimili wa kwanza wa dola, yaani Serikali. Kwani viongozi wengi wanawajibika chini yake kuanzia mawaziri,wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa, wenyeviti serikali za mitaa, madiwani na wakurugenzi wa mikoa na wilaya, listi ni ndefu.

Na huko kuna uzembe mwingi unafanyika hasa kwa kudhani wananchi hawana uelewa wa namna ya kuwawajibisha viongozi hao. Juzi mbunge mpya na kijana Joshua Nassari kutoka Arumeru Mashariki aliongea kitu watu wakaona ni cha kijinga. Alihoji ni kwanini wakuu wa mikoa na wilaya wamejazana bungeni kusikiliza bajeti ya ofisi ya waziri mkuu wakati wananchi wapo mikoani wana shida na uwepo wao.

Kwanini wasifuatilie bunge wakiwa ofisini badala yake watumie magari ya serikali,mafuta, malazi na chakula kukaa bungeni tu bila ya shughuli yoyote?

naomba kuwasilisha, Kido Jembeeeeeeeeeeeeeeee.

No comments:

Post a Comment