Huenda wagonjwa wa
Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa
siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida la Afya Lancet
limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya
ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika
kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini
watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na
kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili
kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa
majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV
kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum
katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston ,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo
wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa
kuimarisha afya ya wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza
utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na
kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya
sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi
na maambukizi bila kujua.
Chanzo: bbc swahili. http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment