Balozi
Joel M Nheleko wa Swaziland
nchini Ubeligiji, ambaye alikuwa Rais wa Mabalozi wa Afrika nchini Ubeligiji
aliyemaliza muda wake, akimkabidhi Balozi wa Tanzania Dk. Diodorus Kamala mfuko
wenye vitendea kazi kama ishara ya kumkabidhi Urais wa Mabalozi wa Afrika
Ubeligiji jijini Brussels
juzi. (Na Mpiga Picha Wetu)
Balozi wa Tanzania
nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala ameteuliwa na mabalozi wa nchi za Africa wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo kuwa
Mwenyekiti wao.
Balozi
Kamala amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini Ubeligiji, Joel
Nheleko aliyemaliza muda wake. Tanzania
itashikilia kiti hicho kwa muda wa miezi sita hadi Julai 1, 2013.
“Nimefurahi
kupewa heshima hii, na naamini nitaitumia fursa hii kufahamiana vizuri na
mabalozi wenzangu na kuvutia fursa za kiuchumi kwa nchi yetu,” alisema Balozi
Kamala.
Wakati
huo huo, juzi mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa Tanganyika ,
walimchagua Balozi Kamala kuwa mwenyekiti wao.
Nchi wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi ,
Rwanda , Tanzania , Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia .
Nchi hizi zimeunganisha nguvu kutafuta
wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya Bonde la Ziwa Tanganyika , ambapo eneo la bonde
hili lenye wakazi wastani wa milioni 40 wanalenga kuliendeleza kwa ajili
ya kujenga miundombinu, kurahisisha usafiri na usafirishaji, kujenga reli mpya
na kuendeleza utalii.
Chini
ya mpango huu wanalenga pia kuboresha viwanja vya ndege vya nchi wanachama vya
Mbala, Kalemie, Bujumbura ,
Kigoma na Kasanga kwa nia ya kurahisisha usafiri wa anga katika ukanda huu.
Dk.
Kamala amekabidhiwa jukumu la kuratibu mpango huu na kwa pamoja watatafuta
fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya mradi huu.
No comments:
Post a Comment