Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akimsikiliza jambo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Raisi Bw Richad Muyungi mara Baada ya Ufunguzi wa Warsha hiyo jana.y
Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Richad Muyungi akimwambia jambo Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Daniel Nkondola Mara baada ya Ufunguzi wa Warsha hiyo jana.
[Picha zote na Ali Meja Ofisi ya makamu wa Rais]
Monica Sapanjo-
Ofisi ya Makamu wa Rais
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Sazi Salula
amewataka wadau wa sekta ya kilimo nchini hasa wakulima wadogo wadogo kujitahidi
kufahamu athari na changamoto mbalilmbali zinazoikabili sekta hii
kutokana na athari za mabadiliko ya
tabianchi. Alitoa rai hiyo wakati akifungua warsha ya siku mbili ya kitaifa ikihusisha wadau mbalimbali
kuandaa mwongozo wa taarifa za kuhimili
mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za
wakulima na wafugaji nchini.
Aliwaomba wajumbe wa warsha hiyo kutoa maoni yao ya kitaalamu ili kuhakikisha mwongozo unakuwa tayari kwa matumizi ya jamii
za wakulima na wafugaji nchini mapema iwezekanavyo hasa ikinzingatiwa kuwa
athari sasa zimeanza kuwa kubwa sana .
Alisema mwongozo huu ni muendelezo wa juhudi za serikali katika
kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi. "Juhudi hizi
zitaiwezesha nchi kuhimili atahari za mabadiliko haya na kuchangia juhudi za
kimataifa za kupunguza gesijoto" alisema Bwana Salula.
Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais kwa ufadhili wa Serikali ya Japana kupitia UNDP, kwa ajili ya kujadili mwomgozo huu wa kusaidia
wakulima na wafugaji wadogo wadogo kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Washirki wa warsha
hiyo ni kutoka kwenye taasisi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na Ofisi ya
Waziri mkuu, Wizara ya maji, Wizara ya habari na michezo, Wizara ya kilimo na
baraza la Mazingira la Taifa(NEMC, Jumuia ya Wakulima Tanzanaia na asasi
mbalimbali zisizo za kiserikali.
Madhumuni ya mwongozo huu ni kuwasaidia wakulima na
wafugaji kuendeleza shughuli zao za ufugaji
na ukulima katika maeneora ambayo yamebadilika kutokana na mabadiliko ya
tabianchi.
No comments:
Post a Comment