Rais wa Gambia
Yahya Jammeh ametoa amri kuwa wafanyikazi wote wa umma watafanya kazi siku nne
pekee kwa wiki kuanzia leo Ijumaa . Ijumaa sasa itakuwa siku ya mapumziko sawa
na Jumamosi na Jumapili.
Rais Jammeh anasema iwapo wananchi wa Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki watapata
muda zaidi wa kusali, kushiriki maswala ya kijamii na kulima mashamba yao .
Kwenye taarifa amesema wananchi wa Gambia wanapaswa kurejea mashambani na kupanda
chakula na kuhakikisha wanakula chakula hicho ili taifa hilo liwe tajiri na lenye afya.
Amesema
kuwa mishahara yao
haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu watafanya kazi zaidi ya saa za
kawaida ili kulipiza siku ya tano.
Shule
za kitaifa hazitafunguliwa tena siku ya ijumaa.Sekta za kibinafsi zitafanya
kazi hadi ijumaa lakini hazitaweza kufanya biashara yoyote na serikali siku
hiyo.
Rais
Jammeh mwenye historia ya kuwa na tabia za kustaajabisha, hajawapa wananchi Gambia muda wa
kujiandaa kwa mfumo huo mpya.
Mwaka
2007 alitangaza kuwa anaweza kutibu ungonjwa wa Ukimwi kwa muda wa siku tatu
akitumia mchanganyiko wa dawa za kienyeji. Tamko hilo lililaaniwa na wataalam wa matibabu kote
duniani.
Pia amekuwa akishtumiwa kwa ukiukaji wa haki
za binadam.
Mwaka
jana wafungwa tisa waliokabiliwa na hukumu ya kifo walipigwa risasi na maafisa wa
polisi huku rais Jammeh akiapa kuwaua wafungwa wote waliohukumiwa kifo katika
muda wa wiki kadhaa. Baadaye alisimamisha mauaji hayo baada ya kukosolewa
vikali na jamii ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment