UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
NA TANZANIA
PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)
04/02/2013
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba baada ya
kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na Tanzania
Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:
1. TANZANIA PREMIER
LEAGUE BOARD
(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi
matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa
nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa
chini:
NAFASI INAYOGOMBEWA
|
S/N0.
|
JINA
|
MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Hamad Yahya Juma
|
2.
|
Yusufali Manji
|
|
|
|
|
MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Said Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake
kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
|
MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI
(Management Committee)
|
1.
|
Kazimoto Miraji Muzo
|
|
2.
|
Omary Khatibu Mwindadi
|
(b) Mwombaji uongozi Ndg. Christopher
Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL
Board Ibara ya 28(2) kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya
Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe
wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.
2. SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea
wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa
chini:
NAFASI
|
S/No.
|
JINA
|
RAIS WA TFF
|
1.
|
Athumani Jumanne Nyamlani
|
2.
|
Jamal Emily Malinzi
|
|
MAKAMU WA RAIS WA TFF
|
|
|
2.
|
Ramadhan Omar Nassib
|
|
3.
|
Wallace Karia
|
|
MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)
|
|
|
1.
|
Kalilo Samson
|
|
2.
|
Salum Hamis Umande Chama
|
|
|
|
|
Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)
|
1.
|
Jumbe Oddessa Magati
|
2.
|
Mugisha Galibona
|
|
3.
|
Samwel Nyalla
|
|
4.
|
Vedastus F.K Lufano
|
|
|
|
|
Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
|
1.
|
Epaphra Swai
|
|
|
|
Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)
|
|
|
1.
|
Elley Simon Mbise
|
|
2.
|
Omar Walii Ali
|
|
|
|
|
Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)
|
1.
|
Ahmed Idd Mgoyi
|
2.
|
Yusuf Hamis Kitumbo
|
|
|
|
|
Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)
|
|
|
1.
|
Blassy Mghube Kiondo
|
|
2.
|
Seleman Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake
kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
|
|
|
|
|
Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)
|
1.
|
David Samson Lugenge
|
2.
|
John Exavery M. Kiteve
|
|
3.
|
Lusekelo E. Mwanjala
|
|
|
|
|
Kanda ya 8 (
|
1.
|
James Patrick Mhagama
|
2.
|
|
|
|
|
|
Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)
|
1.
|
Athuman Kingome Kambi
|
2.
|
Francis Kumba Ndulane
|
|
3.
|
Zafarani Mzee Damoder
|
|
|
|
|
Kanda ya 10 (
|
1.
|
Hussein Zuberi Mwamba
|
2.
|
Stewart Ernest Masima
|
|
|
|
|
Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)
|
|
|
1.
|
Riziki Juma Majala
|
|
2.
|
Twahil Twaha Njoki
|
|
|
|
|
Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
|
1.
|
|
2.
|
Khalid Abdallah Mohamed
|
|
3.
|
Kusianga Mohamed Kiata
|
|
|
|
|
Kanda ya 13 (
|
1.
|
Alex Crispine Kamuzelya
|
2.
|
Juma Abbas Pinto
|
|
3.
|
Muhsin Said Balhabou
|
(b) Waombaji uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea
nafasiwalizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i) Ndg. Omary Mussa
Nkwarulo anayeonba
kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7)
kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi
anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(ii) Ndg. Michael Richard
Wambura anayeonba
kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFFhakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura
alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama
wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg.
Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka Katiba
ya TFF na Katiba ya FIFA.
(iii) Pia
Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu
uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya
29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu
wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati
hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya
usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).
(iv) Ndg. Abdallah Hussein
Musa anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na
ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa
kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(v) Ndg. Mbasha
Matutu anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu)hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7)
kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi
dhidi ya mgombea mwenzake.
(vi) Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara)hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF kwa
kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.
(vii) Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka awe na uzoefu
wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na
pia hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu
majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na
malengo ya TFF.
(viii) Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF
na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu
ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.
(ix) Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya)hakukidhi
matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7)
kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya
TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba.
(x) Ndg. Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa
maelezo ya umri wake na vyeti vya elimu havikubaliani.
(xi) Ndg.
Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani)hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi
za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa hakuhudhuria usaili.
(xii) Ndg. Omary Isack
Abdulkadir anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam)hakukidhi
matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi
maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu
Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa
uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa
TFF.
(xiii) Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu
ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana
ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
3. Usaili uliofanyika kwa
waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL
Board.
4. Uchaguzi wa TPL Board
utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika tarehe 24
Februari 2013 jijini Dar es salaam .
Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
No comments:
Post a Comment