Mbunge wa jimbo la Ubungo (chadema) John Mnyika akilalamika kuvunjwa kwa baadhi ya kanuni bungeni jana.
WABUNGE wa upinzani jana walizua tafrani bungeni na kusababisha
kikao kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai kuvu njika kabla ya
muda uliokuwa umepangwa.
Wabunge hao wa upinzani walisimama wote kwa pamoja na kuanza
kupiga kelele za kupinga hatua ya Ndugai kuruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.
Profesa Maghembe katika hoja yake ambayo iliungwa mkono na
wabunge wa CCM, alikuwa akipendekeza kuo ndolewa bungeni kwa hoja binafsi
iliyokuwa imewasilishwa mapema na Mbunge Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Mnyika katika hoja yake alikuwa akitaka Bunge lia zimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka ya kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Baada ya Ndugai kuruhusu hoja ya Profesa Maghembe kujadiliwa badala ya hoja ya Mnyika, wabunge wa upi nzani walisimama na kuanza kupiga kelele za kupinga kile walichodai kwamba ni Naibu Spika kuvunja kanuni ambazo anapaswa kuzisimamia.
Ilivyokuwa
Profesa Maghembe aliyekuwa mchangiaji wa kwa nza katika hoja ya Mnyika alitoa kauli kwamba Serikali inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maji jijini Dar es Salaam, hivyo kutaka hoja ya Mnyika iondolewe.
Kabla ya kutamka maneno hayo, tayari wabunge wa upinzani bila kujali vyama vyao walikuwa wameanza kumzomea na kupiga kelele kiasi kwamba maneno yake ya mwisho hayakusikika.
Baada ya hapo alisimama Naibu Spika na kuwataka wabunge watulie ili waanze kuchangia hoja hiyo na alimtaka Mnyika kuzungumza, lakini kabla ya Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisemama na kuanza kuzungumza baada ya Naibu Spika kumruhusu.
“Mheshimiwa Naibu Spika naona mwendelezo wa uvunjwaji wa taratibu na kanuni za Bunge, hoja binafsi zinaratibiwa na kanuni ya 57 na 58,”alisema Mdee na kuongeza;
“Kanuni hizi mbili ukizisomaoi Waziri anatakiwa kueleza kipengele gani kitoke…….”
Kabla Mdee hajamaliza kueleza Naibu Spika, alisimama na kumtaka Mnyika achangie
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu alisimama kutaka utaratibu, lakini Naibu Spika Ndugai alimkatisha kisha akasema “Waswahili wanasema kuchamba kwingi……”
“Wewe ni “Chief Whip” (Mnadhimu Mkuu) upande wa Serikali umetoa hoja na sisi tunachangia hivyo tunachangia sasa,” alisema Naibu Spika na kumwita Mdee aendelee kuchangia.
Hata hivyo, Mdee alikataa na Naibu Spika alimwita Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zarina Madabida kuendelea kuchangia.
“Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru kwa kunipa nafasi na
naipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayoifanya,” alisema Madabida, lakini kabla
hajaendelea baadhi ya wabunge wa upinzani wa lianza kutaka kutoa taarifa na
kusimama wakati Naibu Spika naye amesimama hivyo Bunge kukwama kuendelea kwa
muda.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick We rema alisimama na wakati alipoanza kuzungumza wabunge wote wa upinzani walianza kuimba CCM, CCM, CCM huku wakigonga meza.
Kitendo hicho kilisababisha Jaji Werema kwenda kwenye meza ya Spika ili azungumze na Naibu Spika, lakini ke lele ziliendelea na Ndugai akasema, “Siahirishi Bunge ili Watanzania wajue nani anavuruga na wajue pia mbivu na mbichi.”
Aliwataka wabunge wa liokuwa wakiimba na kupiga kelele kuendelea huku shughuli za Bunge zikiwa zimesimama kwa muda.
Baada ya mazungumzo mafupi kati ya Werema na Ndugai, Naibu Spika alisimama na kuhoji wangapi wanau nga mkono hoja ya Serikali na wangapi wanaikataa hoja ya Mnyika kitendo ambacho hakikueleweka, lakini Ndugai akasema hoja imeondolewa.
“Naliahirisha Bunge nataka Kamati ya Uongozi ya Bunge kukutana,”alisema Ndugai huku wabunge wa upinzani wakiwa wanapiga kelele.
Hata hivyo, Werema alisema kuwa Bunge litamwajibisha, Lissu kwa kutoa lugha ya matusi bungeni.
Mvutano asubuhi
Wakati hayo yakitokea katika katika kikao cha jana asu buhi mvutano mkubwa uliibuka pale baadhi ya wabunge walipokuwa wakilumbana kiasi cha kutoleana maneno ya kashfa, kinyume cha Kanuni za Bunge.
Malumbano hayo yaliwahusisha Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu dhidi ya Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla, mvutano ulitokana na majada wa hoja binafsi ya Kigwangalla.
Katika hoja yake mbunge huyo alilitaka Bunge kupitisha azimio la kuitaka Serikali ianzishe mpango maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha mfuko wa mikopo ya vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo.
Katika mchango wake, Lissu aliishambulia hoja hiyo kwa kusema kuwa haikuwa na msingi wa kuwasaidia vijana na badala yake ilikuwa ni hoja ya ‘kutongozea kura za mwaka 2015’.
Jana Lissu pia alitoa taarifa kwamba hoja hiyo ya Dk Kikwangalla haikuwa na ubinifu kwani wakati akipendekeza kuundwa kwa mfuko wa mikopo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara alisema mfuko wa vijana umekuwapo tangu 1994.
Kutokana na kauli hizo, Kigwangalla alipokuwa akihitimisha hoja yake, alimshambulia Lissu kwa kusema:
“Tundu Lissu ni mnafiki, kazi yake ni kupinga kila kitu kinacholetwa mbele yake hata kama ni kizuri yeye anafanya kazi ya kupinga, lakini nasema kuwa ana matatizo na mimi
Vuta nivute hiyo, ilisababisha wabunge John Mnyika, Moses Machali, Felix Mkosamali, Ester Bulaya na David Silinde kusimama na kupiga kelele za kuomba mwongozo wa Spika.
Hata hivyo, mbunge huyo aliwashambulia wabunge hao kwa kusema “Mheshimiwa Naibu Spika, tulishaambiwa hapa na Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kuwa wanaume wanapozungumza lazima vijana wanyamaze, naomba wabunge wote waliosimama wakae chini niwape dozi.”
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment