MATUMAINI ya
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho la Soka
nchini (TFF), Michael Wambura, yametoweka rasmi leo baada ya Kamati ya Uchaguzi
ya TFF, ikiwa chini ya Deogratius Lyato, kumtupa nje.
Sababu zilizomuondoa
katika mchakato huo wa uchaguzi wa ni ule ule wa kupeleka mambo ya soka katika
mahakama za kawaida, sambamba na kukosa uadilifu. Aidha, wagombea wa Urais,
Jamal Malinzi na Athumani Nyamlani wao wamepita, huku nafasi ya Makamu wa Rais
sasa ikibaki kuwaniwa na Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Mbali na Wambura,
wagombea wa nafasi mbalimbali ukiwamo Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wapatao 1o
nao wametupwa nje, akiwamo mwandishi wa habari za michezo, Shafii Dauda,
aliyetupwa kwasababu za kudanganya umma baada ya kuenguliwa katika Uchaguzi wa
IDFA.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo mchana, Lyato alisema Wambura ameondolewa katika
mchakato wa Uchaguzi huo kwa madai ya siku zote, yakiwamo uadilifu na kuwahi
kupeleka masuala ya soka, klabu ya Simba, katika Mahakama za kawaida, hivyo
kujitilia gundu la kutupwa nje kila anapojaribu kuota nafasi za uongozi.
Alisema kuwa
wapinzani wake, Wallace Karia na Ramadhan Nassib, sasa wamepeta kuelekea kwenye
Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24, ambapo pia katika nafasi ya Urais,
wagombea Malinzi na Nyamlani nao wakipeta, huku Omary Mussa Nkwarulo naye
akiwekwa kando kwasababu za
kukosa ufahamu katika nafasi anayoomba ya kuwania Urais wa Shirikisho hilo.
Mbali na matokeo
hayo, Kamati ya Uchaguzi imewapitisha wagombea wa nafasi ya Bodi ya Ligi,
Yusuph Manji na Hamad Yahya Juma kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
huku Said Mohamed akipita kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati wajumbe
waliopitishwa ni Kazimoto Miraji na Omary Khatib.
Alisema kwa
ujumla kila aliyewekwa kando katika uchaguzi ametolewa kwa kutokidhi vigezo
kwenye Kanuni na Katiba wa TFF, vikiwamo elimu, uadilifu ama mkanganyiko
ulitokea katika fomu za maombi ya kupitishwa kwenye mchakato huo.
Mbali na Wambura
ambaye ametolewa kwasababu za kupeleka soka mahakamani, lakini wapo ambao nao
wametupwa nje, akiwamo waliomba kugombea nafasi za Ujumbe wa Kamati ya
Utendaji, wakiongozwa nao Abdalla Mussa, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja,
Iliud Mvella,Farid Nahdi, Hassan
Hassanoo, Omary Isaac na Shafii Dauda.
“Wajumbe
waliopitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe ni pamoja na Alex Kamuzelya, Juma Pinto,
Muhsin Said Balhabou, waliopitishwa katika Kanda ya 13, ambayo ni jiji la Dar
es Salaam, huku Davis Mosha, Khalid Abdallah, Kusianga Mohamed waliopitishwa
kwa Kanda ya 12 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga.
“Wajumbe wengine
waliopitishwa kwa Kanda ya 11 ni Riziki Juma na Twahil Twaha, huku nafasi ya
kutoka Kanda ya 10 ya Mkoa wa Dodoma na Singida, wakati Kanda ya 9 ambayo ni
Mtwara na Lindi ikienda kwa Athuman Kambi, Francis Kumba, Zafarani
Damoder, huku Kanda ya 8
kwa mikoa ya Ruvuma na Njombe, ikichukuliwa na James Mhagama, Stanley Lugenge,”
alisema.
Lyato aliwataja
wengine kuwa ni kutoka Kanda ya 7 ambayo ni Iringa na Mbeya, ikienda kwa Davis
Samson, John Exavery na Lusekelo Mwanjala, wakati Kanda ya 6 ilienda kwa Blassy
Mghube, Selemani Bandiho Kameya, wakati Kanda ya 5 ambayo ni Tabora na Kigoma wametangazwa
Msafiri Mgoi na Yusuph Kitumbo.
Wengine
waliopitishwa Kanda ya 4 wakiwa ni Elley Simon, Omary Ally, wakitoka mikoa ya
Arusha na Manyara, wakati Kanda ya 3 ambayo ni mikoa ya Shinyanga na Simiyu
imeenda kwa Epaphra Swai, huku Kanda ya 2 ikienda kwa Jumbe Magali, Mugisha
Garibona, Samuel Nyalla, Vedastus
Lufano hawa wakipitishwa huku wakitoka mikoa ya Mwanza na Mara, wakati Kanda 1
ikiwa na mikoa ya Kagera na Geita na kupitishwa Kalilo Samson na Salum Hamis
Umande.
Uchaguzi wa TFF
umepangwa kufanyika Februari 24, wakati ule wa Bodi ya Ligi ukitarajiwa
kufanyika Februari 22, ambapo patashika ya kuelekea kwenye tukio hilo ukizidi kupamba moto.
Kumalizika kwa
mchakato huo wa usaili, sasa unasababisha kuweka msuguano zaidi kwa nafasi
mbili za Malinzi na Nyamlani, kutokana na mvuto wao katika soka nchini.
Chanzo:
Handeni Kwetu.
No comments:
Post a Comment