Sunday, February 24, 2013

Huu ndiwo urafiki wa kweli kwenye shida na raha. Jakaya Kikwete ashiriki mazishi ya baba yake M7 Uganda.

 Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akimpa pole mke wa Rais wa Uganda Yoweri Museven mama Janet Museven katika mazishi ya baba mkwe wake nchini Uganda.

Rias Kikwete akiwa na Rais Museven jana katika mazishi ya baba wa Rais huyo wa Uganda.

 Rais Kikwete akitoa heshima za mwisho katika jeneza la mzee Amos Kaguta (97) baba yake Rais Yoweri Kaguta Museven aliefariki wiki iliyopita nchini Uganda.

Rais Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la mzee Amos Kaguta wakati wa mazishi yake kwenye kijiji cha Rwakitura magharibi mwa Uganda jana.

Picha zote kwa hisani ya mpiga picha wa Ikulu Fred Maro.

Rais Jakaya Kikwete alishiriki mazishi hayo alipopita Uganda akiwa njiani kurudi nyumbani akitokea nchini Ethiopia, ambapo wakuu wa nchi za Afrika ukanda wa maziwa makuu walikuwa wakitia saini mpango wa umoja wa mataifa wa amani, usalama na ushirikiano katika nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,mjini Addis Ababa.

No comments:

Post a Comment