Jaji nchini Afrika Kusini hii leo
anatarajiwa kutoa uamuzi ikiwa mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius,
anayetuhumiwa kwa mauaji ya mchumba wake, anaweza kuachiliwa kwa dhamana.
Mwanariadha huyo anakanusha kosa la mauaji
akisema kuwa alimpiga risasi Reeva Steenkamp akidhania kuwa alikuwa jambazi.
Upande wa utetezi unasema kuwa ushahidi huo
wenye utata na uliotolewa na mmoja wa polisi umeweza kuhujumu upande wa
mashtaka.
Hata hivyo upande wa mashtaka unasema kuwa
kuna hofu kuwa Pistorius huenda akakosa kufika mahakamani ikiwa ataachiliwa kwa
dhamana.
Pistorius anatarajiwa kurejea katika mazoezi
wiki ijayo,ikiwa atapewa dhamana.
Kocha wake aliyasema hayo alipowasili
mahakamani kwa siku ya nne ya kusikiliza kesi ya dhamana dhidi ya Pistorius.
Mnamo Alhamisi polisi walimbadilisha jasusi
aliyekuwa anachunguza kesi hiyo na kuweka polisi mwingine baada ya taarifa
kujitokeza kuwa polisi huyo mwenyewe alikuwa anakabiliwa na kesi ya jaribio la
mauaji.
Jasusi mkuu wa Afrika Kusini Luteni,
Vineshkumar Moonoo, ndiye atachunguza kesi hiyo sasa.
Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa
Pistorius alifyatua risasi nne katika bafu yake iliyokuwa imefungwa huku
marehemu Steenkamp akiwa ndani. Aligongwa kichwani , kwenye paja na mkononi.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment