Saturday, February 16, 2013

Poleni wadau nilipotea kidogo,

Ndugu zangu,

Maisha ni magumu sana, na kutafuta kuna njia nyingi. Mtaona kwa muda mrefu sikuwa nikiwapasha habari zinazojiri ulimwenguni.

Naam nilikuwa katika harakati za kutafuta, nilikuwa na ziara ya wiki moja kanda ya ziwa. Nilikwenda mji wa Mwanza na baadae nikaenda Bukoba.

Nitaleta picha nyingi ziwe zawadi kwenu, lakini kubwa nitaandika muhtasari wa safari yangu iwe mwanga kwa watanzania wengine wanaoipenda nchi yao. Safari ya Mwanza imenisaidia kukamilisha Mkoa mmoja wa kanda hiyo ambao sikuwa nimeutembelea.

Kwa sasa nimebakisha mikoa kadhaa ya kanda ya kusini na nyanda za juu kusini. Lakini kanda zote zilizobaki nimeshazitembelea. Kanda ya kati, nimetembea mikoa yote, kanda ya mashariki, nimetembea mkoa yote, kanda ya kaskazini pia nimemaliza.

Nikiwa mdogo nilipanga kuitembea nchi nzima halafu niandike kitabu, nikikamilisha hizo kanda mbili za kusini na nyanda za juu kusini Mungu akipenda nitaandika kitabu kuhusu Tanzania.

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
16 Feb, 2013
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment