Tangazo la kuzaliwa mwana mfalme likitolewa katika kasri la Birmingham. |
Ujumbe wa heri njema umeendelea
kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa
tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.
Mwanamfalme William na mkewe Kate
,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa
kwanzaJumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na
takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini
hajapewa jina.
Katika taarifa fupi William,amesema
wana furaha isiyo na kifani.
Baadaye leo jeshi la Uingereza
linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40
hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.
Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa
mwanamfalme huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na
moja ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la
Buckingham, zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na
habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron, alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana
kwa Uingereza.
Naye wawiri mkuu wa Australia, Kevin
Rudd, alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola,
huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William baada ya
kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment