Mjuu wake Nelson Mandela, Mandla ,
amewatuhumu jamaa zake kuwa na njama ya kutaka udhibiti wa mali ya babu yake
rais wa zamani wa Afrika Kusini.
Matamshi yake yanakuja baada ya
mahakama kuamuru kuwa mabaki ya wanawe Mandela kufukuliwa na kuzikwa nyumbani
kwa Mandela katika kijiji cha Qunu.
Mnamo Jumatano polisi walifukua
mabaki ya wanawe Mandela nyumbani kwa Mandla kufuatia agizo la mahakama baada
ya kuwasilisha malalamiko yao mahakamani.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94,
yungali hali mahututi hospitalini lakini madaktari wamedhibiti hali yake.
Rais Jacob Zuma alitoa taarifa baada
ya kumtembelea mzee Mandela hospitalini mjini Pretoria.
Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu
kati ya familia ya Mandela juu ya urithi wake lakini imekithiri huku hali yake
ya kiafya ikiendelea kuwa mbaya zaidi.
Mzozo huu wa hivi karibuni kuhusu
makaburi unatokana na hoja ya wapi azikwe Mandela akifariki.
Stakabadhi zilizowasilishwa
mahakamani wiki jana zilionyesha kuwa anatumia mashine ya kupumua.
Alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi
Juni baada ya kuugua maradhi ya mapafu.
Mkewe amesema kuwa Mandela wakati
mwingine anasumbuka lakini hajalalamika kusema anahisi uchungu wowote.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment