Haya ndiyo makaburi ya famila ya Mzee Mandela yaliyozua vurugu kubwa za kifamilia.
Huku rais mstaafu wa Afrika Kusini
Nelson Mandela akiendelea kuugua mjini Pretoria, jamaa zake wamejikuta kwenye
malumbano kuhusu mgogoro ambao umejitokeza wazi kwenye vyombo vya habari.
Badhi ya jamaa za familia
wamemshtaki mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla, katika juhudi za kutaka kufukua
maiti za wanawe watatu wa Mandela ili wawazike katika makaburi ya Qunu, ambako
Mandela anataka azikwe.
Na Mgogoro kuhusu kutaka kuwafukua
wafu hao ni ishara ya mgawanyiko mkubwa katika familia kubwa ya Mandela, wake
zake watatu , watoto sita na wajukuu 17 na vitukuu
12 . Kulingana na baadhi ya viongozi wa kijamii, wakati familia yake inapoendelea kuzozana , roho ya Mandela haiwezi kuwa na amani.
12 . Kulingana na baadhi ya viongozi wa kijamii, wakati familia yake inapoendelea kuzozana , roho ya Mandela haiwezi kuwa na amani.
Jamaa kumi na sita wa familia ya
Mandela pamoja na viongozi wa kijamii wiki jana walipewa idhini ya muda na
mahakama kufukua maiti hao na kuwapeleka katika mji wa
Qunu, ambako makaazi ya Mandela yapo.
Qunu, ambako makaazi ya Mandela yapo.
Lakini
Mandla Mandela, ambaye kulingana na vyombo vya habari, alihamisha maiti hao
umbali wa kilomita 22 kutoka mji wa wa Qunu hadi nyumbani kwake eneo la Mvezo
mnamo mwaka 2011, anapinga uamuzi huo.
Maiti hao ni pamoja na Makgatho
Mandela, babake Mandla aliyefariki kutokana na ugonjwa wa ukiwmi, mwaka 2005
pamoja na ndugu zake, Thembekile, aliyefariki katika ajali ya barabarni na
mwanawe wa kwanza aliyefariki akiwa na miezi tisa, walizikwa kwenye makaburi
yaliyokaribiana.
Watatu hao walifukuliwa bila ya
idhini ya familia yote ya Mandela na viongozi wa kijamii wa ukoo wa AbaThembu
ambao pia ni ukoo wa Mandela.
Wanaamini kuwa roho ya Mandela, ina
sumbuka hivi sasa kutokana na mzozo kwenye familia yake na ndio maana roho yake
haikatiki.
Watu kumi na sita ni mashahidi
katika kesi ya kuomba mahakama idhini ya kufukua maiti hao, akiwemo mkewe
Mandela, Graca Machel, mwanawe Mandela Makaziwe na viongozi wakuu wa ukoo wa
AbaThembu.
Kinachohojiwa zaidi kwenye mzozo huu
ni nani atachukua nafasi ya Mandela kama kiongozi wa familia?
Viongozi wa kijamii walimteua Mandla
kama kijana mwenye umri mkubwa zaidi kuweza kuchukua nafasi ya Mandela, na
kumkabidhi jukumu la chifu Zwelivelile wa ukoo wa Thembu.
Pia ni mbunge katika chama tawala
ANC.
Lakini wengi katika familia
wanaonekana kutopendezwa na miendeno yake, akiwemo Makaziwe, mwanawe Mandela wa
kike.
Mpango wake wa kutaka kufungua
makavazi katika shamba ambalo makaburi hayo yapo, imewaacha wengi vinywa wazi
katika familia hiyo.
Katika
mgogoro mwingine, wanawe wa kike na wakubwa wa Mandela, Makaziwe na Zenani
wameenda mahakamani wakitaka kuwanondoa wasaidizi watatu wa Mandela kutoka
katika kampuni za baba yao.
Wawili hao wanataka umiliki wa
kampuni hizo ambazo ni za thamani ya mamilioni ya dola.
Wiki jana Makaziwe aliandaa mkutano
wa dharura wa kijamii ambapo inasemekana Mandla alilaaniwa vikali kwa kuhamisha
maiti za jamaa zake bila idhini.
Baadhi wanaamini kuwa Mandela lazima
asuluhishe mzozo huu kabla ya ya kifo chake.
Moja ya imani za kitamaduni nchini
Afrika Kusini ni kuwa mtu huwa hafi wakati ana mambo yanayomsubiri
kuyasuluhisha.
Baadhi wanaamini kuwa badhi ya mambo
ambayo bado hajakamilika kwa Mandela ni kuweza kusuluhisha migogoro hii ndani
ya familia pamoja na kuipatanisha familia take.
Mandela alistahili kuafikiana na
familia yake kabla ya kufukua miili za jamaa zake.
Wajumbe wa ukoo wa AbaThembu,
wameandaa mkutano wa dharura mjini Qunu baadaye mwezi huu kusuluhisha mizozo
hiyo.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment