Monday, July 8, 2013

Jana nilikutana na wanafunzi takriban 20 niliosoma nao Kampala ingia uone picha.Huyu anaitwa A

Huyu anaitwa Makih Assa Hassan, ndiye mwenyekiti wa watanzania wasomao KIU Kampala.
Kushoto kwangu ni Dickson Daniel, alikuwa katibu wangu kipindi nikiwa Mwenyekiti wa watanzania chuoni, kulia kwangu ni Ipyana, yeye alikuwa mwananchi wa kawaida tu lakini alipata kuwa kiongozi kwenye jumuiya ya vijana wa umoja wa mataifa chuoni. Inamana yeye alikuwa na cheo kikubwa kuliko sisi maana aliongoza chuo kizima sisi tuliongoza watanzania tu.

.
 Mike na mkewe walipewa heshima ya kukata keki, huyu ni Mmarekani mweusi ambaye yupo Tanzania akijitolea kwenye masuala ya huduma kwa waliopata ajali. Ni rafiki wa Mwalimu Nyembo.

 Utamu wa keki ikatwe vipande vipande, hasa viwe vidogo ikiwa kubwa huwezi kuifaidi itakuchafua.

 Dickosn naye alikuja na dada zake ni mimi tu niliacha kuenda na ndugu na rafiki zangu.

Sherehe ilifana sana, tulizungumza, tulikula, kucheza na kunywa mambo mazuri kama haya hutokea mara chache sana.
KIDOJEMBE
MBALAMWEZI BEACH
MSASANI, DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment