Ndege ya aina ya Boeing 787 inayomilikiwa na Shirika la
ndege la Ethiopia katika uwanja wa Heathrow.
Shughuli katika uwanja wa ndege wa Heathrow zimekwama kwa muda
baada ya ndege moja ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 787
Dreamliner kushika moto.
Safari zote za ndege katika uwanja huo zilisitishwa kuanzia saa kumi na
nusu.Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Heathrow, hakuna abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo wakati wa tukio hilo.
Mapema mwaka huu ndege hamsini aina ya Dreamliners, zilisimamishwa kufanya kazi kutokana na matatizo ya mtambo wa Battery.
Mwezi April, ndege moja ya shirika la ndege la Ethiopia, ambalo limesemekana kuwa ndilo lililopata matatizo katika uwanja wa Heathrow, ilisafiri kutoka Adis Ababa hadi Nairobi kwa mara ya kwanza tangu mwezi Januari.
Picha zilizochapishwa kwenye mtandao wa Kijamii wa Twitter, zimeonyesha ndege moja katika uwanja huo ikiwa imezingirwa na magari ya kuzima moto.
Wafanyakazi wa idara ya kuzima moto ya baraza la mji wa London wamesema kuwa walikuwa tayari kushirikiana na maafisa wa kitengo cha kupambana na mikasa ya moto katika uwanja huo.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment