Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufani
ya Uchaguzi kufuatia mabadiliko ya Katiba yaliyofanywa Jumamosi (Julai 13 mwaka
huu) na kuingiza kamati nyingine mpya.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ametangaza wajumbe wa
kamati hizo leo (Julai 18 mwaka huu) mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji
ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema uteuzi wa wajumbe hao umezingatia maoni ya
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, lakini vilevile amewashukuru wajumbe
walioteuliwa kwa kukubali kutoa mchango wao katika maendeleo ya mpira wa miguu
nchini.
Mbali ya Jaji Luanda ambaye ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Francis Kiwanga (Makamu Mwenyekiti),
Anney Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala. Kamati ya Uchaguzi inaongozwa na
Hamidu Mbwezeleni, Moses Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Mustafa Siyani, Hassan
Dyamwale na Kitwana Manara.
Mwenyekiti Kamati ya Rufani ya
Maadili ni Jaji Steven Ihema, Bi. Victoria Makani (Makamu Mwenyekiti),
Mheshimiwa Mohamed Missanga, Henry Tandau na Mheshimiwa Murtaza Mangungu.
Kamati ya Maadili inaundwa na Bi. Jesse Mguto (Mwenyekiti), Francis Kabwe
(Makamu Mwenyekiti), Profesa Mtambo Madundo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
Mohamed Mpinga na Evod Mmanda.
Profesa Mgongo Fimbo anaongoza
Kamati ya Rufani ya Nidhamu wakati Makamu wake ni Ong’wanuhama Kibuta na
wajumbe ni Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mstaafu Jamal Rwambow. Kamati ya Nidhamu inaongozwa
na Kamishna wa Polisi (CP) Mstaafu Alfred Tibaigana, Mustafa Kambona (Makamu
Mwenyekiti), Mheshimiwa Azzan Zungu, Yusuf Nzowa na Mohamed Msomali.
Pia Kamati ya Utendaji
imefanya mabadiliko katika Kamati ya Waamuzi ambapo Said Nassoro na Charles
Ndagala kutoka Chama cha Waamuzi wanachukua nafasi za Joan Minja na Riziki
Majala. Kamati hiyo inaendelea kuongozwa na Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge,
Omar Kasinde (Makamu Mwenyekiti) wakati mjumbe mwingine ni Mohamed Nyama.
Kamati ya Tiba inaongozwa na
Dk. Paul Marealle wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti itajazwa baadaye na Rais
Tenga. Wajumbe ni Mwanandi Mwankemwa, Anthony Ngome, Frank Mhonda, Kapteni
Joakim Mshanga na Helen Semu.
Rais Tenga alisema mabadiliko
mengine yamefanyika kutokana na waliokuwa wajumbe kuomba kupumzika. Wajumbe
walioomba kupumzika ni Dk. Sylvester Faya, Idd Mtiginjola na Deo Lyatto
Boniface
Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Julai 18, 2013
No comments:
Post a Comment