Kiongozi wa mashtaka katika mahakama
ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, amesema kuwa mashahidi wawili wametupilia
mbali ushahidi wao katika kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Bi Bensouda alisema mashahidi
nambari 5 na 426 wamefutilia mbali ushahidi wao kwa sababu za waswasi kuhusu
usalama wao.
"kwa kifupi, inaonekana kuwa
wasiwasi wa shahidi nambari tano, wameogopa sana kuhusu usalama wao na kuwa
athari za kutoa ushahidi wake huenda zikawa na madhara makubwa kwa maisha yake
na kwa hivyo akaamua kufutia mbali ushahidi wake.'' alisema Bensouda kwa ujumbe
wake kwa majaji mnamo Jumanne.
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka,
ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili msimamo
wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.
"upande wa mashtaka umefanya
mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa
wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo
hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, ''
aliongeza kusema Bi Bensouda said.
Hata hivyo mwendesha mashtaka
aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya
mtuhumiwa.
Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza
kusikilizwa Novemba 12.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment