Meneja huduma kwa wawekezaji Revocatus Abegas akijibu maswali ya wanahabari leo asubuhi.
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimetaja nchi kumi zinazoongoza kwa
uwekezaji nchini Tanzania ambapo nchi iliyoongoza ni Uingereza yenye miradi 934
nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari
MAELEZO jijini leo katika utaratibu wa wasemaji wa asasi za serikali kukutana
na wanahabari, meneja uhusiano wa TIC Pendo Gondwe amesema wawekezaji wa kigeni
wanaiingizia serikali fedha nyingi za kigeni na ajira kwa wazawa.
Akitaja nchi hizo kumi zenye miradi mingi nchini idadi yake kwenye
mabano, Pendo alisema, “Nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini ni Uingereza
yenye miradi (934), China (455), India (365), Kenya inashika nafasi ya tano
ikiwa na miradi (455) lakini faida yake si kubwa kama India.
Aidha nafasi ya tano inashikiliwa na USA (218), Uholanzi (162), Afrika
Kusini (208), wakati Canada inashika nafasi ya nane ikiwa na miradi (195),
Ujerumani (146) na Italy inashika nafasi ya kumi ikiwa na miradi (86).
Kwa mujibu wa Pendo mwaka jana 2012 TIC869 kutoka mataifa mbalimbali
iliyotoa ajira 174,000, iliyokuwa na faida ya dola za kimarekani milioni 11
elf.
Katika hatua nyingine ripoti ya kituo hicho inaweka wazi kuwa miradi
iliyoongoza kwa kusajiliwa ni Kilimo, utalii, usafirishaji, majengo ya biashara
na viwanda.
“Hiyo ndiyo miradi mitano iliyoongoza kwa mwaka jana, lakini idadi ya
wawekezaji 869 mchanganuo wake ni kama ifuatavyo watanzania wamesajili miradi
450, wageni kwa ujumla wamesajili miradi 219 na miradi iliyosajiliwa kwa
ushirikiano wa wenyeji na wageni ‘joint venture’ ni 192.
“Miradi yote hiyo imezalisha ajira 93,000 na miradi hiyo imeleta faida ya
dola za kimarekani mil 8505,” alisema Pendo Gondwe meneja uhusiano wa TIC.
HAFIDH KIDO
9 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment