Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
amemtaka balozi wake nchini Zimbabwe kukoma kutoa matamshi hadharani baada ya
kukosolewa na rais Robert Mugabe.
Zuma, aliyekuwa mpatanishi mkuu
katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2008-2009 nchini Zimbabwe, alisema ni yeye
pekee anayeruhusiwa kutoa matamshi yoyote kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika
Julai tarehe 31.
Balozi wake Lindiwe Zulu, wiki jana
alisema kuwa maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe hayaonekani
kuridhisha.
Rais wa Zimbabwe ndiye alimtaka Zuma
kumkomesha balozi wake dhidi ya kutoa matamshi kama hayo hadharani.
Rais Mugabe ananuia kuendelea
kuongoza nchi hiyo hata baada ya kuitawala kwa miaka 33 na atamenyana na waziri
mkuu wake Morgan Tsvangirai.
Mahasimu hao wa jadi wamekuwa
wakigawana mamlaka tangu mwaka 2009, chini ya mkataba ulioafikiwa kwa usaidizi
wa rais Zuma.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment