Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi
ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa
mamlakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa
wingi wa kura, Mohammed Morsi.
Viongozi duniani wamepokea kwa
tahadhari matukio yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Ujerumani, Guido Westerwelle, amewaambia waandishi kwamba anaangalia kwa umakini
hatua iliyochukuliwa na jeshi la Misri.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Uingereza , William Hague, amesema Uingereza haiungi mkono uvamizi huo wa
kijeshi lakini haina budi kuitambua hatua hiyo na kusogea mbele. Hata hivyo
alikataa kulishutumu jeshi kwa kumpindua Morsi akisema ni uvamizi ulioungwa
mkono na watu wengi.
Mfalme Abdalla wa Saudia ametuma
ujumbe wa hongera kwa kaimu rais wa Misri akisema kwamba uteuzi wake unajiri
katika wakati muhimu.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah
al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile
Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa
Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Ishara ya mapenzi iliyochorwa angani
kwa kutumia ndege za kijeshi kuwataka wananchi kupatana
Hatua hiyo inakuja baada ya siku
nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na
chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa
kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood
kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha
nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema
kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo
atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga
bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa
hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya
huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi
mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment