Wednesday, July 10, 2013

UN yawachokonoa Vatican.

Umoja wa mataifa umeitaka vatican kutoa maelezo kuhusu kesi elfu moja ambapo viongozi wa dini katika kanisa hilo wamewanyanyasa watoto .
Ombi hilo kutoka kwa kamati ya umoja huo inayosimamia haki za watoto linajiri miezi sita kabla ya wawakilishi wa kanisa katoliki kufikishwa mbele ya umoja wa mataifa kujibu mashtaka ya kashfa ya unyanyasaji wa watoto ambayo yamekumba kanisa hilo katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.
Umoja huo pia unataka habari zaidi kuhusu usadizi uliotolewa kwa waathiriwa pamoja na kisa chochote ambapo wahusika walinyamazishwa.
Mapema mwaka huu kiongozi wa kanisa katholiki duniani papa Francis alisema hatua ya kanisa hilo kukabiliana na unyanyasaji wa kingono utaimarisha sifa zake.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment