Wednesday, June 12, 2013

Bajeti ya Tanzania kesho, tutarajie nini?

Masikio na macho ya Watanzania kesho yataelekezwa hapa Dodoma ambako kauli ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa itakuwa na thamani kubwa.

Ni siku ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu, hasa kutokana na utarabu mpya wa kujadili bajeti za Serikali kwa kuanza na wizara na kumalizia na Bajeti Kuu ya mwaka wa fedha 2013/14.

Dk Mgimwa ndiye aliyebeba siri ya mafanikio katika bajeti iliyopita, na mipango iliyopo katika bajeti ijayo, ili wananchi waweze kuona kama watajikwamua katika lindi la umaskini.

Ni bajeti katikati ya kipindi cha pili cha cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete; zikiwa zimesalia bajeti mbili kiongozi huyo kuondoka kuwapisha wengine.

Ratiba inaonyesha kuwa kesho wabunge wataingia bungeni kwa kuanza na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, na maswali ya kawaida kabla ya Waziri mwenye dhamana ya Mipango kusoma mwelekeo wa uchumi.

Itakapotimu saa 10 jioni, Waziri wa Fedha atasoma bajeti yake, ikiwa ni sambamba na kusomwa kwa bajeti nyingine za nchi wanachama wa Afrika Mashariki – Kenya, Uganda, Rwanda, Rwamda na Burundi.

Kama nilivyodokeza hapo juu, bajeti ya safari hii inakuja kwa mtindo tofauti, kwa kuwa tayari wizara zote 32 zimekwishawasilisha bajeti zao na kupitishwa na bunge.

Karibu bajeti zote ukiachia bajeti ya Maji na ile ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, ndizo zilizopata misukosuko kiasi cha kufanyiwa marekebisho ya kuongezewa fedha kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wabunge.

Kutokana na mabadiliko hayo, Dk Mgimwa anatarajia kusawazisha bajeti yeke ili kuondoa nakisi iliyotokea baada ya wizara hizo mbili kuongezewa fedha ambayo hazikuwa zimepangwa awali.

Pamoja na umuhimu wake, sasa iko wazi kuwa kwa kuwa bajeri za wizara zimekwishapitisha, hakuna uwezekano tenma wa bajeti kukwamishwa, kinachotarajiwa ni kauli za ndiyooooooo kutoka walio wengi, na hata ikitolewa ya hapana itakuwa ya wachache ambayo haitakuwa na athali kubwa.

Itakumbukwa kuwa bajeti ya kesho ndiyo inayofungua milango ya kuanza kutumika kwa fedha ambazo zilishapitishwa kwenye wizara.

Matarajio ni kwamba katika muda wa siku saba ambao itajadiliwa mfululizo, mambo mbalimbali yatazungumzwa, ikiwa ni sehemu ya kuboresha au kuwekea mkazo yale yaliyojadiliwa katika bajeti za wizara.

Hatutarajii wabunge kuzigeuka ndimi zao au kumsurubu Mgimwa yuleyule waliyemsifia. Nani atakuwa wa kwanza kusema siungi mkono wakati alishiriki katika kupitisha bajeti zingine za nyuma?

Ukiacha wale wa Kambi ya Upinzani ambao mara nyingi wamekuwa wakipinga, wale wabunge waliogonga vifua na kutangaza kupinga bajeti za wizara, wataibuka tena kupinga baejeti kuu?

Mathalan, kina Luhwaga Mpina (Kisesa –CCM), Deo Filikunjombe (Ludewa CCM), Kangi Lugola (Mwibara-CCM) na Ally Keisy (Nkasi Kaskazini wataibuka kusapoti madai yao ya awali, au wamekwishatulizwa?

Nimetolea mfano wabunge hao ambao wakati wote wamekuwa hawakubaliani na masuala ya ‘ndiyoooo’ ‘ badala yake wamekuwa wakijitosa kukosoa sera za chama chao hadharani bila woga, pale wanapobaini kuna tatizo.

Mfano mzuri ni kuwa, mwaka jana Filikunjombe alipinga hadharani bajeti hiyo kwa sauti ya juu ‘hapana’; pia mwaka huu alipinga bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini siku chache zilizopita alimwaga sifa kwa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.

Mbunge huyo machachali bungeni alimwaga sifa hizo kwa na kuwakumbusha mawaziri wengine kuiga mfano wa waziri huyo katika kugawa rasilimali za nchi kwa watu wote. 0757649789
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment