Rais wa Marekani Barack Obama ambaye yuko katika
ziara yake ya Afrika, amesifu nchi ya Senegal kwa kuwa moja ya nchi
zenye demokrasia thabiti barani Afrika.
Pia aliisifu kwa kuwa na mtindo wa kusuluhisha migogoro kwa mazungumzo na mashauriano, wala sio kwa njia ya ghasia.
Alisema kuwa Afrika kama bara limepiga hatua kubwa upande wa demokrasia katika miaka ya hivi karibuni.
Obama atazuru Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua sana na amelazwa hospitalini.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanamuombea Mandela pamoja na familia yake.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment